Watanzania wameyakataa kabisa majiko ya umeme, hivi ni ujinga au ushamba?

Hii sasa ndio JF tuliyoizoea, sio ya kina Mashamba
 
Hii trauma tumerithi hatujachagua kuwa nayo. Mimi nilitumia nguvu nyingi kujishawishi kutumia birika la umeme nidhani kuwa kila baada ya kuchemsha maji litakuwa limetumia zaidi ya unit 12 au zaidi kichwani na mawazoni mwangu.

Uhalisia sasa khaaaaaaaah 😂 😂 😂 😂

Yaani mfano una unit 2. 20 kwenye mita yako yapo saa hii. Ukitumia hii birika yangu ya kuchemshia maji kutoka ubaridi hadi yaanze kutokota na kuwa ya moto kabisa linatumia. 0.12 units. Yaani kwenye hizo units 2. 20 toa 0.12. ni zaidi ya kidogo.

Tokea pale aiseee nikasema ni vema kutazama mambo kisayansi na sio kihisia utapiga sana hatua.
 
kweli mleta mada unashida kichwani

Toeni elimu kwanza kupitia mitaala mashuleni kwani kizazi Cha sasa kinachokunya nyikani(porini) kinachosubiria world bank kupitia mrisho mpoto wahamaishe nyumba ni choo (choo za masinki)

Leo Hii uzungumzie umeme wapikie hivi uko siriazi wewe

Je swali la msingi miundombinu ya makazi pia yakoje
 
Wachache watakuelewa mkuu
 
Kuna kitu kingine pia kuhusu utamaduni wa wake zetu wa kiswahili anabandika maji jikoni kisha anaenda nje kusikiliza umbeya na marafiki zake hii imekaaje kiusalama?tuachane na ishu ya gharama
Kuunguza vitu
 
Sio kweli chakula kukosa ladha ni ubovu wa mpshi na sababu sio multi cooker. Nina tumia multicooker na electric cooker za kawaida . MAPISHI NI SANAA KAMA SANAA NYINGINE MKUU
Okay, ivi multi cooker na Pressure cooker ipi Bora?
 
Zile hometheater ya sony ni watt 100 (mia) mziki mnene poa kabisa ila ina watt mia,kwa kweli jiko la umeme halina matumizi mabaya ya umeme labda sasa uchemshie maharagwe au maji ya kuoga au ya kunywa ila kwa ujumla ni nishati nafuu,nakuunga mkono
 
Okay, ivi multi cooker na Pressure cooker ipi Bora?
Kama Pressure cooker ni ya umeme ni Multcooker kwasababu hupika aina nyingi za vyakula kwa mfano hupika huchemsha huoka hukaanga.
Ila iliwa ni Pressure cooker ya kawaida isiyo ya umeme huchemsha zaidi .

Pia kuna Rice cooker hizi ni special kwa ubwabwa tyuuuu
Kwenye matumizi ya Umeme Mult purpose cooker ina matumizi madogo mno ya Umeme
 
Hii multi cooker naskia chakula kinakua hakina ladha
Uongo mkubwa sana niko nazo mbili yaani nyumbani tulishasahau kupikia baadhi ya vyakula kwenye mkaa, mfano maharage , nyama, ndizi , mihogo , magimbi n.k ni mwendo wa multicooker
 
Nilikuwa na rice cooker enzi za 2014 nilikuwa napika hadi ugali , maharage na njugu ili yaive ni kuongeza maji moto maana maji yakiisha inabadili kwenda warm
 
Okay kwahyo kumbe Kwenye vifaa vya umeme multi cooker Haina mpinzani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…