Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati?

Zitto ahsante kwa maelezo maana tumejitahidi kuwaelimisha siku hizi mbili tunaonekana ni wapingaji

Nyumbani kwangu pia kuna mwanafunzi wa uchumi naye anafagili nikampa shule akakaa sawa inabidi nimuongezee na hizi notes ili aelewe uchumi wa dunia kabla hajajitosa kwenye fani chuokikuu nwakan

Uchumi wa kati

Binafsi kipato changu kilikuwa 264000 jumlisha faida ni 547000 lkn leo nina 223000 pekee

Biashara tatu zimeanguka kwa vyuma kukaza halafu unasema pato letu la mtanzania linakua!!? İtabidi uwe kichaa ili uelewe


Kama kikwete angeongoza awamu ya tano basi nchi ingekuwa inakaribia dola 2500 maana mzee wa msoga ile anaingia akakutana na ukame+ njaa ikaleta mgawo wa umeme uliosababisha mafuta kupanda kisha infalation ikalipuka na imports zikaongezeka na kuangusha value ya sh dhidi ya dola hivi vitu vyote magu hakukuvkkuta bali amekuta kila sehemu kuna mipango na hela standby ila kauli zake zikasababosha inflation kupanda kidogo pamoja na sh kuporomoka kwa wawekezaji kuondoa mitaji yao Tz na wengine kugoma kuja kuwekeza na wengine kuuchuna kuangalia huku fedha zikipumua( magu angekuwa na akili kama watu wa pwani ambao wao wanajua kutafuta hela na matumizi ya hela ambayo ni kuonekana unatumia mpaka watu wajue hela ipo
 
"wakati tumetumia Shilingi 1.8 Trilioni kwenye matumizi ya kununua Ndege 11 zinazotumiwa na 5% ya Watanzania, katika miaka 5 tumetumia Shilingi Trilioni Moja tu kwenye matumizi ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinazotegemewa na 67% ya Watanzania. Bajeti hii ya Kilimo ni 0.6% ya Bajeti yote ya Tanzania kwa miaka 5."

800 billion nawaza ingewafanyia mengi sana wakulima, wafugaji na wavuvi.
 
Kama ni uchumi wa kati through GDP Tanzania imefikia na kupita muda mrefu tu, tatizo ni kutumia vipimo vya mabeberu badala ya vyetu.

Mkulima wa chini analima si chini ya hector 2 on average na wengi wanazidisha hiyo. Kama ni mkulima mzuri yield yake ni 5 ton/h na anavuna on average two to three times annually, hizo bidhaa zake kwa bei ya soko zinaweza kabisa vuka dolla 1000.

Wakulima wengi wanatumia chakula chao wenyewe, wana mifugo yao wenyewe, wengine wanauza maziwa hizi ni expenditure and income ambazo hazipo reflected kwenye GDP kama vile ilivyo bidhaa za kwenye black market, wakati uchumi wa mkulima ni halali.

Serikali ya Tanzania inagawa thousands of hectors for free kila mwaka kwa wakulima wafugaji na wawekezaji ata kama kuna malipo ni way below market value (watu hao hao wakitumia ardhi waliopewa kuombea mikopo kama shamans) hizi initiative ni either sehemu ya government expenditure au investments in the GDP equation maana worth billions zinazalisha, and yet this economic activities is not reflected in the GDP.

Mapato ya wakulima wanayopata nje ushirika hakuna anaejua, savings za wakulima hakuna anaejua, huko mipakani si ajabu warundi, wanyarwanda, wazambia, wamalawi, wakenya wanaleta hela nyingi sana ndani ya nchi katika masoko ambayo income yake hatujui wala multiplier effect yake is not quantified in the economy.

Tukiweza rasimisha hii mifumo GDP ya Tanzania inaweza fika $2000 easily. Asilimia kubwa ya wafanyakazi wa serikali wa kima chini before tax annually they earn more than $2000 na awana chochote. Je mkulima mwenye asset ya ardhi na mifugo avuki kiwango icho hii nchi ni tajiri kushinda nyingi za africa.
 
Natak niulize tu,iv ikitokea hyo rate ikashuka na kufikia may b $1000 tutatolewa tena kweny hyo wanayoita uchumi wa kati?
 
Hata US yenye GDP ya $62,000 more than 2/3 of the population don’t earn that much ndio maana kwenye GDP kuna debate kubwa sana kwenye maswala ya income distribution maskini wa Qatar uwezi mfananisha na wa US in terms of quality of life and opportunities to life chances.

Vilevile uwezi mfananisha mkenya wa chini taifa ambalo kwa madai ya GDP ni tajiri kushinda Tanzania. Wakati mtanzania wa chini ambae maisha mjini yakimshinda anaweza rudi kijijini na kupata ardhi ya kulima wananchi wengi wa mataifa ya Africa waliotuzidi GDP hawana hizo option ukiwa maskini you are stuck there kilichobaki ukimbie nchi (ndio maana mtanzania utamuona alikuwa kwenye mtumbwi uliozama kwenye bahari ya Italy au kafungiwa kwenye camp ya ukimbizi Spain shida hizo hatuna za kufika Europe ikabidi upoteze maisha yako).

Nchi nyingi za africa ukiwa maskini huna namna tofauti na mtanzania sisi tunapokea wanyarwanda, warundi, wakongo na wamalawi kila siku wanaokuja Tanzania kama safe heaven lakini sisi atuendi huko hii nchi ni tajiri serikali inaweza tumia value ya usable land reserve as income na GDP ikapaa sio lazima tuige formula zao we got to value things in our contexts.
 
Tanzania ina rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani na kama siyo CCM kuzitumia vibaya mda huu Tanzania ingekuwa ni Nchi tajiri kuliko South Africa German hata America na ungekuwa kwenye uchumi wa juu zaidi hata kuliko India china korea japan England, chini ya CCM pesa zote za maendeleo zinatumika kukandamiza demokrasia kuwahujumu kuwadhoofisha wapinzani.
 
Natak niulize tu,iv ikitokea hyo rate ikashuka na kufikia may b $1000 tutatolewa tena kweny hyo wanayoita uchumi wa kati?
Ndiko tunaenda tena mda si mrefu kwani Tanzania ilizoea misaada na ukiwa na uchumi wa kati misaada hupungua sana
 
We are rich than the GDP wanayotuonyesha maisha ya maskini wa Tanzania ni far better kushinda maskini wa Nigeria na South Africa nchi zinazo ongoza kwa GDP africa huko ukiwa maskini utaji JJ hakuna ardhi.

Nyie tusifanye mchezo hizo nchi ukisikia kuna maskini mjomba ni kasheshe kuna documentary unaangalia kuna watu huko asia wanavizia ngozi za kuku zinazotupwa kwenye migahawa ndio wakale na familia zao mpaka mtu unasema duh. Wakati machinga akiamua kwenda kulima kesho ardhi anapata tatizo letu sisi ni lege lege tu.

wacha Magu awatie adabu kidogo watu wafanye kazi.
 

Huu ndio ufafanuzi wa kiuchumi tunaouhitaji. Asante Bw. Zito.
 
Nchi zingine ulipo ndipo umefika ndipo utafia milele ukikwama huna pa kwenda, ni tofauti na Tanzania ambapo kuna Ardhi nyingi haina mtumiaji ukirudi kijijini maisha yanaendelea kama kawaida
 
expand...
Kwa tafasiri nyingine ni kwamba ni vyema watanzania mkaendelea kuonyesha unyonge wenu, msifanye kazi kwa kujituma, msijenge miundombinu kwa ajili yenu ili world bank iwaonee huruma na kuwapa mikopo ya mashariti nafuu, ili wakubwa wa walete misaada kwa ajili ya maendeleo yenu. Eti huyu naye anastahili hata 1% ya kura zenu!!
 
Nchi zingine ulipo ndipo umefika ndipo utafia milele ukikwama huna pa kwenda, ni tofauti na Tanzania ambapo kuna Ardhi nyingi haina mtumiaji ukirudi kijijini maisha yanaendelea kama kawaida
Umeona kiongozi huo ndio ukweli wenyewe sisi atuwezi kuwa chini ya wakenya sijui wa S.A kama tungekuwa na upimaji wetu wa GDP.

Watanzania wana privilege kubwa sana. Halafu mijitu aitaki kuchangamkia fursa ndio maana mzee baba anasema hapa kazi tu na asiefanya kazi asile no charity under Magu he is a conservative at heart.

Magu anachofanya ni kuwajengea fursa wakulima ambazo watu awaelewi kwanza kwa kujaribu kuhakikisha wanapata access ya masoko (you know what they say; built it and they will come).

Miaka kumi tu nyuma mpunga wa Songea, mahindi Rukwa, mananasi Geita to name a few of farm produce hizo bidhaa zilikuwa zina haribika kisa wafanya biashara kufuata bidhaa hizo sehemu kutokana na miundombinu walikuwa wanaoshida.

Hizi fujo za Magufuli za miundombinu ni kutaka kuwapa hao watu access ya masoko na kuwapa wafanyabiashara food for thought unaweza fika sehemu yoyote Tanzania. Hizo faida inaweza zisionekane leo but hila ni kazi ambayo lazima ifanyike na hakuna aliyekuwa yupo tayari au mtu sahihi zaidi ya Magu.

Najua wewe sio shabiki wa Magufuli vile and to be honest ana mapungufu yake but he is a genius I am telling you sio kwa faida yangu na wewe hila kwa Tanzania ya baadae anachofanya akimaliza kujenga mazingira sahihi uchumi wa Tanzania utapaa watu watashangaa baada ya miaka 10-15 if not soon.

Issue ni Tanzania ya kesho sio Magu (personal issues watu waweke pembeni) miaka 5 mingine ya Magu will be something else he has tricks under his sleeves.
 
Mkuu watu wanakuona katuni hapa JF

Huwezi kujenga hoja ,wewe umekaa kushabikia vyama tu ccm au chadema

Wetu wengi humu JF ni wasomi na wataalamu


Punguza umbea na ushabiki,kama hujasoma uchumi kaa kimya
 
Povu la nini
Mkuu elimu yako ni ndogo kwenye uchumi
.
Ahaaa umesoma na zitto udsm lakini yeye ana Firsr clasa wewe una Pass
Mmmh
 
Watetezi wa CCM mitandaoni wengi hawajui kusoma vizuri wao kazi yao ni kukariri zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM tu
Huwa nawaona kule youtube, kwakweli youtube wameiteka lakini huku jf wanajificha wapi? Wengi wao hawana hoja zaidi ya matusi, chuki na kejeli.
 
Acha taarabu,Jibu mambo ya uchumi haya
.unadhani mambo ya Forced labour haya
 
Kwani huwezi fikiria lolote?
 
Hivyo ukiwa kama kiongozi na mwana uchumi unashauri serikali ichukue hatua zipi ili kufikia lengo hiyo 2025..??
Wahusika huwa hawapo tayari kupokea mawazo yenye tija kama hayo, wanataka kile mtu awapigie makofi na kuwaimbia pambio za sifa.
 
political rubbish
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…