Watanzania wengi maskini wanafia ndani kwa kukosa matibabu

Mkuu unajua leo hii hali, mbona sasa imezoeleka!!?,,nikujihangaikia si wenyewe kadri tuwezavyo na mungu muweza anatulinda.
 
Sasa kama amesaidia ndio ajitangaze hapa,wacha upuuzi wako wa kibongo kulaumu kila kitu.
 
Serikali ya ccm ndiyo umetufikisha hapa aisee! Kwa ufisadi wanaoufanya mungu awalaani aisee
 
Makasiriko ya nini mkuu, umejuaje kama yeye ana uwezo wa kiuchumj kusaidia?
 
Kwani bima ya afya ni Bure? Si mpaka uchangie kila mwaka. Mtu anakosa hela ya kula na umuongezee mzigo/mchango wa bima ya afya!
maskini ana aga dunia kitandani kwa kukosa fedha ya matibabu akiwa na Samsung Galaxy ya laki 8 dah, na wengine iphone ya m4.

Inashangaza mno, kwamba kipaumbele ni vitu laxury au afya?

huruma haijawahi kumsitiri au kunusuru afya au uhai wa mtu kwa uhakika, labda awe mjanja kama kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi.

Mgonjwa ana simu kali kuliko ya doctor, yet hawezi kumudu gharama za matibabu na wala hana bima πŸ’
 
Unaongelea wenye iphone ya 4m, unadhani watanzania wangapi wanamilili simu ya milioni 4?
Humu jf kwenyewe wenye jeuri ya kumiliki simu ya milioni 4 ni wachache mnoo.

Na maelezo ya jamaa amegusia watu wa vipato vya chini, mtu ambe hata kula yake tabu, mtu anaefanya kazi vibarua, anaweza kupata kazi 3 ama 4 katika wiki, kwa malipo ya elfu 10-15 kwa siku, hiyo hiyo ale yeye na mkewe, atizame wazazi wake, matibabu, usafiri n.k, huyu mtu anawezaje kulipia bima.
Achana na vijijini hapa mjini daslam tu. Kuna watu vipato haviruhusu kulipa bima.
 
Umeandika kama vile huishi Tanzania
 
achana na iphone,
nenda muhimbili au amana uone wagonjwa wa kawaida kabisa hawana bima wala hawana uwezo wa kagharamia matibabu yao but simu walizonazo iwe Tecno, Infinix au sumsang ni za gharama mno kuliko hata za madaktari wanao wahudumia halafu ati huyo mtu ni maskini?


nadhani makosa ni kutokujua kipaumbele katika maisha yetu ni nini.
Wengi tunakimbilia vitu luxury kuliko afya na uhai.

Huyo maskini yuko radhi ajikakamue kununua smartphone mbovu kwa elfu 90 , huku akipuuza bima ya afya ya elf70.

Akiugua,
anakuja kutia huruma na kimbwelambwela hapa πŸ’
 
Umeandika kama vile huishi Tanzania
Naishi Tanzania,
na ni kiongozi wa wananchi ambae kwenye suala la Afya kipaumbele changu cha kwanza katika awamu ijayo ni kuhakikisha, iwe iwavyo kila familia jimboni inakua na bima ya afya,

wanafunzi wa chule kuanzia chekechea had secondary, kama kiongozi wao nitaona namna ambavyo wazazi, wadau wa afya jimboni na tasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa na serikali tunaweza kusaidia kila mtoto nae awe na bima ya afya.

Hakuna haja ya kutia huruma hapa wakati ukiuza gunia moja tu la alizeti unaweza kupata bima ya afya ya mwaka mzima πŸ’
 
mkulima mdogo wa mazao ya chakula huko kijijini anatoa wapi iphone? achilia tu hata uwezo wa kulipia hiyo bima ya afya! unaujua umaskini wa watanzania waishio vijijini au unaongea porojo za kisiasa?
 
Bima ya afya kwa 70k??

We umeamua kudivert ujumbe wa mleta mada kwa sababu unazozijua mwenyewe.

Mleta mada kazungumzia masikini ambao vipato vyao kwa siku havieleweki.
We unabadilisha mada unasema mara iphone ya milioni 4, mara sijui kimeenda kimerudi, infinix sijui nini.. Kwa dunia ya sasa simu sio luxury, simu ni hitaji la muhimu pia, zipo za luxury, lakini hizi za mawasiliano tu ni muhimu na kuna watanzania hata hizo infinix za 90 elfu hawana, wanatumia kiswaswadu cha tecno kina rubber band kila kona.

Sasa huyu umuambie mambo ya bima, anaipatia wapi laki 2 kasoro, tena ya pamoja, kulipa bima?

Mkuu au wewe ni chawa wa watawala nini??
 
Watanzania wengi wanakufa kwa kisukari, nahisi kisukari yaweza kua sababu #1 kwa vifo nchini. Na tatizo kubwa ni sababu watu wengi hawana elimu ya wale nini waache nini, bongo kila mtu ni "piga ugali 80% mbona 20%" wanapiga wanga asubuhi hadi usiku, nutrition ni kitu nadhani kingefundishwa shuleni kila mtu aelewe kua kula vibaya ni kitu kitakuua vibaya sana. Nimeona watu wengi wana kisukari wanabadilisha mlo kisukari kinapotea kabisa wanaishi vizuri tu.
 
Nami nilikuwa natiririka na habar yake nione alifanya Nini ila nasikitika nilichotegemea sikukiona.
 
Kwamba hujui maisha harisi ya mtanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…