Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Watatu walioteuliwa Ukuu wa Wilaya, akiwemo Japheth Maganga wadaiwa kukataa uteuzi

Narudia hakuna mtu mwenye future na malengo atakae kubali nafasi za kuteuliwa ambazo hauna uhakika nao siku unaamka asubuh umetenguliwa kiufupi siasa ina wenyewe na sio wote wanaweza kuwa wanasiasa wamefanya maamuzi mazuri sana hao viongozi wanastahili pongezi.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Zamani nyakati za Nyerere mkuu wa Wilaya akiwa anaitwa Area Comissioner kilikuwa ni cheo chenye heshima sana. Mpaka mtu uteuliwe kuwa Area Comissioner lazima uwe ni mtu wa shoka sana. Lakini siku hizi, dah!
Sikuhizi ukiwa kada tu unayeonekana onekana kwenye matukio muhimu unaweza lamba hiko cheo.
 
Hzi nafasi zinawafaa "ma-jobless" (hasa wale chawa wa chama) sio kwa watu wenye kipato cha kueleweka!
 
Kwa heshima ya ma DC naomba nisikutajie mshahara wao, utashangaa!. Mshahara wa top boss wao, rais wa JMT ni TZS. 9,500,000,
From DC to president kuna gap ya ngazi 10!. Mkurugenzi wa halmashauri ana mshahara mkubwa kuliko DC, mbunge ana mshahara mkubwa kuliko DC!. Hivyo kimshahara DC ni Bwana mdogo sana!. Mimi na kijikampuni changu cha PPR, namsaidia Samia kuwalipa mishahara ma dc wake kadhaa!. Ila pamoja na mshahara kiduchu wa DC, ana marupurupu mengi na posho nyingi zikiwemo posho za vikao, na posho za safari.
P
Asante mkuu. Lakini hiyo 9.5mil si msukuma mwenzetu ndiye alijiwekea kutaka tujue ni mtakatifu sana asiye mlafi? Sidhani kama huyu wa sasa amejipangia kimshahara kidogo hivyo.

Hata hivyo cheo cha DC kwa sasa kinaonekana kunajisika sana maana ufunguo wa engine ya wilaya uko mikononi mwa DED na timu yake ya wataalamu. DC wamebaki na wataalamu wa nyuki na wanyamapori tu😀
 
Mapinduzi na mabadiliko ya viongozi wa vyama huru vya kitaaluma kama CWT, TLS, Chama cha Madaktari Tanganyika n.k yanatakiwa ili kuweza kushutua mamlaka husika
Tatizo wameingiziwa mamluki wa TISS
 
MaDC wengi njaa tupu na ombaomba wa kutupwa. Wengine wanatembeza bakuli kwenye NGOs kuomba hela ya mafuta na service ya gari.

Kwa mtu mwenye steady stream(s) of income hawezi kukubali uDC tena huko nanjirinji ndanindani.

UDC sio kazi ya heshima maana unaweza kufutwa suddenly tena bila hata kuambiwa kwanini umefurushwa
Ila si ni ajira ya kudumu?
 
Mmesahau yule meneja wa Tigo nadhani kanda ya ziwa alichomoa UDC wa Ankali..?
huyo yuko sekta binafsi
Mwalimu mtumishi wa Umma unakataa uteuzi wa Mh Rais???!
Bossi wako?Mwajiri Mkuu wa Watumishi?
Wamedandia mtumbwi wa vibwengo vibaya mno

Kitawakuta kitu
Kwani walimu wote ni waajiliwa wa serikali .....!!? Kama mtu haitaki hiyo kazi kwa nini umlazimishe? Na uteuzi unatakiwa umcosult Mteuliwa kabla ya kumtangaza. Huo ndio ustaarabu. Hii ya kuteua watu bila ridhaa yao ni uhuni na inaonyesha ni jinsi gani CCM wanavyofikiri wamemiliki wananchi.
 
Kwa heshima ya ma DC naomba nisikutajie mshahara wao, utashangaa!. Mshahara wa top boss wao, rais wa JMT ni TZS. 9,500,000,
From DC to president kuna gap ya ngazi 10!. Mkurugenzi wa halmashauri ana mshahara mkubwa kuliko DC, mbunge ana mshahara mkubwa kuliko DC!. Hivyo kimshahara DC ni Bwana mdogo sana!. Mimi na kijikampuni changu cha PPR, namsaidia Samia kuwalipa mishahara ma dc wake kadhaa!. Ila pamoja na mshahara kiduchu wa DC, ana marupurupu mengi na posho nyingi zikiwemo posho za vikao, na posho za safari.
P
Ila we msukuma mjeuri sana! Kwamba unamsaidia Rais kuwalipa mshahara maDC wake kadhaa! 😅😅🤭
 
Kwa bahati nzuri sana safari hii wamepatikana watu ambao watakuwa mfano kwenye swala hili ili tusiendelee tena kuwa tunabishana bishan humu mitandaoni. Uteuzi wa mamlaka ya Rais huwa siyo hiari, ni lazima. Sema kuna ile room ya kuweza kutao udhuru na kuomba ateuliwe mtu mwingine ila SIYO KUKATAA. Bahati nzuri safari hii imepatikana sample ili tusiendelee tena kuwa tunabishana humu mitandaoni.
Baba nyumbani anakua-sign jukumu la kwenda shamba ukavune mpunga umekomaa, halafu wewe unakataa; unataka uende nani? Tupo wote, tutaona kitakachofuata baada ya hapo
That's very good. Hizo actions ndizo pia zitathibitisha Umungu wa Urais wa Tanzania .... Katiba Mpya ni Lazima!
 
Kwani walimu wote ni waajiliwa wa serikali .....!!? Kama mtu haitaki hiyo kazi kwa nini umlazimishe? Na uteuzi unatakiwa umcosult Mteuliwa kabla ya kumtangaza. Huo ndio ustaarabu. Hii ya kuteua watu bila ridhaa yao ni uhuni na inaonyesha ni jinsi gani CCM wanavyofikiri wamemiliki wananchi.
Walimu hawa ni watumishi wa umma
Kitawakuta kitu kwani ni kinyume na mikataba yao
 
Walimu hawa ni watumishi wa umma
Kitawakuta kitu kwani ni kinyume na mikataba yao
Fine hata kama ni watumishi wa umma bado wana haki zao za msingi. Watumishi wa umma siyo wananjeshi .... Wanajeshi unaweza kuwadeploy popote na wakati wowote. Hii Katiba ya Kikomunist ndiyo inasababisha haya yote ya kuwafanya wananchi wawewatumwa kwenye nchi yao. Tatizo ni CCM kuendelea wa chama kimeshika UTAMU na kuvifanya vyama vya Wafanyakazi kama taasisi za serikali ..... Na kwa kufanya hivyo wameweza kubana hazi za wafanyakazi.
 
Salaam Wakuu,

Japheth Maganga aliyetuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera akataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya alioteuliwa na Rais Samia hivi karibuni.

Japhet kasema, baada ya Kushauriana na Familia yake, alimuandikia rais Samia kumshukuru kwa kumteua pia na kumuomba atengue uteuzi wake na achaguliwe mtu Mwingine.

Wateule wengine ambao wamekataa uteuzi ni:

Leah Ulaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita na na Dina Mathamani aliyeteuliwa kwenda Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma

Wote waliokataa Uteuzi wa Rais Samia ni Viongozi wa juu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT).

Leah Ulaya ni rais wa CWT, Dinah Mathamani ni Makamu wa Rais wa CWT huku Japheth Maganga akiwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

======

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ameshiriki kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho jijini Tanga huku akisema kwa sasa hawezi kueleza kwanini hajaripoti katika wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Vilevile, Maganga alihojiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga zaidi ya dakika 50 lakini si yeye wala wanausalama hao walioweka wazi sababu za mahojiano hayo.

Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.

Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.

Mara baada ya kumaliza kuhojiwa na polisi kuanzia saa 4:36 hadi saa 5:24 asubuhi nje ya ukumbi wa mkutano huo unaofanyikia katika Hoteli ya Regal Naivera, Mtaa wa Bombo jijini Tanga Maganga alirejea ukumbini na baadaye kidogo alitoka nje.

Nje ya ukumbi ambapo Mwananchi Digital limeweka kambi, Magamba amesema, “kwa sasa nimeziba mdomo labda usubiri tutakapomaliza kikao ndipo nitazungumza kuhusu nafasi ya U-DC na CWT."

Wakati Maganga akisema hayo, Rais wa CWT hakutoka ndani ya ukumbi wa mkutano huo huku maofisa wa CWT wakisema hajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Kitendo cha viongozi wakuu hao wa CWT kuonekana Tanga wakati wenzao wakiapishwa kimezua mjadala mitandaoni na kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba wameomba wateuliwe wengine kwenye nafasi hizo za U-DC ili kuwawezesha kuendelea na majukumu yao katika chama cha walimu.

Chanzo: DC mteule ahojiwa na polisi dakika 50, Rais CWT…
Rais kuteua watu bila kuwauliza kama watakubali teuzi ni dharau na ujinga.
 
Fine hata kama ni watumishi wa umma bado wana haki zao za msingi. Watumishi wa umma siyo wananjeshi .... Wanajeshi unaweza kuwadeploy popote na wakati wowote. Hii Katiba ya Kikomunist ndiyo inasababisha haya yote ya kuwafanya wananchi wawewatumwa kwenye nchi yao. Tatizo ni CCM kuendelea wa chama kimeshika UTAMU na kuvifanya vyama vya Wafanyakazi kama taasisi za serikali ..... Na kwa kufanya hivyo wameweza kubana hazi za wafanyakazi.
Mtumishi wa umma unaweza kuwa deployed popote kwa majukumu yoyote na mwajiri wako/serikali

Ndo mikataba yao inavyosema
 
Back
Top Bottom