Watoto hawana faida, hasa kwa masikini. Kuzaa watoto ni mateso ya kujitakia tu

Na maskini wana nguvu za kiume na uzazi mzuri hatari. Watoto sita, mtu unawezaje kuwalea kwa shughuli za shamba na biashara ndogo ndogo? Matokeo yake watoto wanasoma kwa kuunga unga hadi mtu anamaliza shule, kapitia mikono mingi kwa mjomba, shangazi, baba mkubwa etc.
 
sahihi lakini tunabidi tuheshimu mawazo ya mtu shida wanaume wengi hawa Hudumii watoto wao
 
sahihi lakini tunabidi tuheshimu mawazo ya mtu
Ni kwel ,kama vile, ambavyo alipaswa si tu kuheshimu mawazo yetu wengine bali ya baba kwanza aliyemzaa

kutohudumia watoto ni shida ambayo ina sababu nyingi sana na mara chache sana umasikin huwa sababu. Shida za kindoa, masuala ya uaminifu kwa wenzi n.k ndio maana kuna matajiri kibao wametelekeza watoto wao licha ya kuwa na uwezo wa kuwatunza. Na pia kuna masikin kibao wanaotunza watoto wao kwa hali na mali mpaka wanafanikiwa.
humo ma vyuoni asilimia kubwa ya wanafunzi ni watoto wa masikini

Shida inakuja sasa, umesomeshwa mpaka chuo kikuu ila bado UNATKA URITHI NA MALI ,huu ndio ufala sasa kama wa mleta mada na wajinga wenzie wanaounga mkono
 
Hongera Mkuu kwa kuwa na mawazo ya namna hii!
Kuna dhana mbili lazma uzifahamu vyema kwanza! kuna familia za Kiafrika na Magharibi! Mitindo miwili tofauti ya maisha.

Umezungumzia dhana kwamba Obama ana watoto 2, Bush ana mtoto 1 na Clinton ana mtoto 1. Ila hao ni wachache, Donald John Trump ana watoto watano akiwemo Barron Trump mbona hujamzungumzia au kwa kuwa sio mtu wa muhimu katika kuunga mkono hoja yako? Genghis Khan alikuwa na watoto wangapi? Wanahistoria na wanasayansi wamejaribu kuangalia vinasaba tu wameona ni kazi ngumu kwani ni zaidi ya watoto mia moja na kitu.
Bi Eleanor pamoja na Rais Franklin D. Roosevelt walizaa watoto sita akiwemo rubani Elliott Roosevelt.

Kaya ambazo zina uwezo wa kuzaa wazae tu maana kila mtoto anakuja na sahani yake! Watoto sio mizigo hata siku moja; ila wazazi tunawaona ni mizigo kwa kuwazaa bila mipango.
 
Mshukuru Mungu alikuleta duniani kupitia wazazi wako ili leo uje ukufuru hivi.

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
 
Wewe ukiwa hasara kwa wazazi wako,usi generalize wote.
Halafu watoto siyo mtaji,ni faraja tu.

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
 
Wewe ukiwa hasara kwa wazazi wako,usi generalize wote.
Halafu watoto siyo mtaji,ni faraja tu.

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
Sawa watoto ni faraja ila uwe umejipata mkuu kwenye ilo wala hakuna ubishi

Ikiwa hujajipata mlo wako wa siku tu unaupigia mbio mpk inakua mtihani iyo faraja ya watoto utaipata saa ngapi mkuu?

AU nyinyi ndo wale wazazi maojua kubebesha wake zenu mimba ila mtoto akishazaliwa ankua kama hahusiki na ww vile hamuna mda na watoto wako, nyinyi ni mbio tu na kutafuta maisha hujui mtoto ameamkaje ama ameshindaje, amekulaje yaani hupati ata muda wa kuka na mtot wako mkapiga stori,
kama hufanyi ayo kuna haja gan ya kuwa na mtoto mkuu?
iyo faraja unayoizungumzaa wewe unaipatia wapi kwa hao watoto ukiwa hupati ata mda wa kukaa na watoto wako ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…