Watoto wa shule sekondari siku hizi hawapendi kuchomekea! Nani alaumiwe kati ya Wizara, Wazazi au Walimu?

Muda wa wazazi kutoka nyumbani asubuhi unapishana
 

Kwa hiyo shule zote zinaandaa watumishi?
 
Lakini hata mtaani kunahitaji nidham, hawa hawa ndo wakwe wenu baadae watawaolea watoto wenu
Kuchomekea ndo kipimo cha nidhamu?

Haya mawazo ndo yanachelewesha maendeleo kwa taifa.

Nenda hata mtandaoni tu tafuta picha za wanafunzi wa dunia ya kwanza then angalia kama wanahangaika kuchomekea unakoona wewe ndiyo nidhamu.

Na kutokuchomekea kwao bado ndo innovators wa technolojia mbalimbali unazotumia wewe mchomekea shati.
 
Unatfsirije kukosa nidhamu? Kuchomekea ni nidhamu?
Kukosa nidhamu ni kitendo binafsi cha kutozingatia utaratibu uliowekwa!

Mfano!
Kama ukikuta sehemu wazee ndo wanatakiwa kukaa kwenye kiti, halafu vijana wasimame, wewe ukaamua kukaa na mzee akasimama pembeni ilihali wazee wote wanatakiwa kukaa! Hii inatafsilika kijana HUNA NIDHAMU! unless umepewa kibali cha kukaa na wakubwa kwa sababu maalum
 
Nani kakudanganya nidhamu ndo itakufanya uwe bora kielimu?

Kuna watoto watukutu hawana nidhamu ila performance zao darasani na kwenye mitihani ya national level hawakamatiki.

Nidhamu ya uoga ndo imetufikisha hapa kama taifa.
 
Kwanza mim mwanang lazima avae suruwal yenye pindo kwa chin na lazm achomekee.avae na saa na lazima shat iwe panga la pasi.na lazima atumie deodorant za kwapa.marufuk kunyoa kiduku
Wanafunzi wengine yote hayo hawafanyi ila ndio wanaoongoza mitihani na masomo darasani.

Uncle wangu alishindikana kwenye shule moja hivi kubwa tu nchi hii kila wakati ni kuitwa kwenye vikao na walimu hakuwa na hiyo nidhamu ila performance yake hakuna aliyekuwa akiikaribia maana ndo anaongiza darasa na mtihani wa form four amepata Division one ya 7.
 
Taasisi yoyote duniani ina Uniformity!

Jeshini hata kama ni mtaalam wa Kara k, lazima uvae kadri ya vazi lilivyoelekezwa!
Shule ni miongoni mwa taasisi! Lazima Uvae kama mwanaTaasisi husika!

Kushindwa kufanya hivyo ni utovu wa nidham!
Sare ziko pote kwenye taasisi hata makanisani kuna sare, hata misikitini kuna sare, hata kwa waganga kuna sare!
Hadi wachawi wana sare! Ambapo hutambuana na ndo nidhamu yao katika taasisi!
 
Swali ni kwamba kuvaa sare ndo nidhamu?

Mbona askari wanafukuzwa kazini kila siku na wanavaa hizo sare unazokazania ndiyo nidhamu?

Hao walimu wenyewe wanafukuzwa kazi kila uchwao kwa kutokuwa na nidhamu sasa maana ya nidhamu ni sare / kuchomekea ama ni matendo ya mtu anavyoishi na jamii husika?
 
Picha linaanza mwalimu katia bonge la modo na kitop (et ndo shati) iliyobana sana. Unategemea mwanafunz atakuaje
 
Nimekupa tafsiri ya nidham post namba #176
Kama hujaelewa bhas mkuu
 
Wizara ikitoa tamko dogo tuu la maadili inatosha mkuu. Ni swala la kuongea hadharani kwenye vyombo vya habari "mwangwi" wake unapiga kigoma hadi mtwara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…