Watoto wa shule sekondari siku hizi hawapendi kuchomekea! Nani alaumiwe kati ya Wizara, Wazazi au Walimu?

Watoto wa shule sekondari siku hizi hawapendi kuchomekea! Nani alaumiwe kati ya Wizara, Wazazi au Walimu?

Ila kweli aisee..Mimi huku nawaona hawafanani na mwanafunzi..Mimi sijasoma zaman sana lakini angalau tulikuwa tunavaa decently, sketi ndefu, shati unachomekea unavaa na Tai. Kiatu cheusi na socks. We used to look smart!
Lakini siku hizi hata socks hawavai, hasa watoto wa kiume, sijui kimetokea nini.

Ila tusiwalaumu wao tuanze na wazazi maana wakati mtoto anatoka kwao wazazi wanatakiwa wahakikishe yuko sawa na shule pia walimu wanatakiwa waangalie uvaaji wa mwanafunzi wao maana huwezi kuwa mwalimu wa shule ambayo mwanafunzi wamevaa kihuni kihuni na ukawa comfortable. Wazazi na walimu wawe wa kwanza kulaumiwa.
Muda wa wazazi kutoka nyumbani asubuhi unapishana
 
Hili bomu la utovu wa nidham nani analilea?

Unaweza kufikiri wizara ya elimu imebadili utamaduni wa uvaaji!

Siku hizi watoto wa shule za sekondari hususani hizi za kutwa hawapendi kabisa kuchomekea sare za shule, katika 100 utakuta watano tu ndiyo wanaochomekea!

Hata ukitazama hizo suruali wanazovaa nyingi ni njiwa (yaani hazifuniki kiwiko) Mashati yao ya shule mengi ni madogo hayafiki kiunoni (Vitopu) Wengine hawana hata vibebeo (mabegi) wanabeba daftali kitozi mkononi Haya yote yanatia sana mashaka tunaandaa wasomi gani

Je, hii style ya uvaaji tunaandaa watumishi wenye sifa gani huko baadae?

Je, nani anastahili hizo lawama? Wizara, wazazi au walimu?

Au tusubiri watumishi wasio na nidhamu baadae ndipo tuwakanye!?

Kwa hiyo shule zote zinaandaa watumishi?
 
Lakini hata mtaani kunahitaji nidham, hawa hawa ndo wakwe wenu baadae watawaolea watoto wenu
Kuchomekea ndo kipimo cha nidhamu?

Haya mawazo ndo yanachelewesha maendeleo kwa taifa.

Nenda hata mtandaoni tu tafuta picha za wanafunzi wa dunia ya kwanza then angalia kama wanahangaika kuchomekea unakoona wewe ndiyo nidhamu.

Na kutokuchomekea kwao bado ndo innovators wa technolojia mbalimbali unazotumia wewe mchomekea shati.
 
Unatfsirije kukosa nidhamu? Kuchomekea ni nidhamu?
Kukosa nidhamu ni kitendo binafsi cha kutozingatia utaratibu uliowekwa!

Mfano!
Kama ukikuta sehemu wazee ndo wanatakiwa kukaa kwenye kiti, halafu vijana wasimame, wewe ukaamua kukaa na mzee akasimama pembeni ilihali wazee wote wanatakiwa kukaa! Hii inatafsilika kijana HUNA NIDHAMU! unless umepewa kibali cha kukaa na wakubwa kwa sababu maalum
 
Nashangaa sana.kama mdau wa elimu nasikitika.Tena nawaona hawa wa hizi shule za kata.sijajua hivi huwa walimu wa nidham siku hiz hakuna au? Kwanza wanashona vinjiwa na vichupa anavaa vimoka hana soks.yaan elimu na nidhamu ni mate na ulimi.usipokuw na nidham jua tu utaishia kusindikiza wenzio.
Nani kakudanganya nidhamu ndo itakufanya uwe bora kielimu?

Kuna watoto watukutu hawana nidhamu ila performance zao darasani na kwenye mitihani ya national level hawakamatiki.

Nidhamu ya uoga ndo imetufikisha hapa kama taifa.
 
Kwanza mim mwanang lazima avae suruwal yenye pindo kwa chin na lazm achomekee.avae na saa na lazima shat iwe panga la pasi.na lazima atumie deodorant za kwapa.marufuk kunyoa kiduku
Wanafunzi wengine yote hayo hawafanyi ila ndio wanaoongoza mitihani na masomo darasani.

Uncle wangu alishindikana kwenye shule moja hivi kubwa tu nchi hii kila wakati ni kuitwa kwenye vikao na walimu hakuwa na hiyo nidhamu ila performance yake hakuna aliyekuwa akiikaribia maana ndo anaongiza darasa na mtihani wa form four amepata Division one ya 7.
 
Kuchomekea ndo kipimo cha nidhamu?

Haya mawazo ndo yanachelewesha maendeleo kwa taifa.

Nenda hata mtandaoni tu tafuta picha za wanafunzi wa dunia ya kwanza then angalia kama wanahangaika kuchomekea unakoona wewe ndiyo nidhamu.

Na kutokuchomekea kwao bado ndo innovators wa technolojia mbalimbali unazotumia wewe mchomekea shati.
Taasisi yoyote duniani ina Uniformity!

Jeshini hata kama ni mtaalam wa Kara k, lazima uvae kadri ya vazi lilivyoelekezwa!
Shule ni miongoni mwa taasisi! Lazima Uvae kama mwanaTaasisi husika!

Kushindwa kufanya hivyo ni utovu wa nidham!
Sare ziko pote kwenye taasisi hata makanisani kuna sare, hata misikitini kuna sare, hata kwa waganga kuna sare!
Hadi wachawi wana sare! Ambapo hutambuana na ndo nidhamu yao katika taasisi!
 
Swali ni kwamba kuvaa sare ndo nidhamu?

Mbona askari wanafukuzwa kazini kila siku na wanavaa hizo sare unazokazania ndiyo nidhamu?

Hao walimu wenyewe wanafukuzwa kazi kila uchwao kwa kutokuwa na nidhamu sasa maana ya nidhamu ni sare / kuchomekea ama ni matendo ya mtu anavyoishi na jamii husika?
 
Picha linaanza mwalimu katia bonge la modo na kitop (et ndo shati) iliyobana sana. Unategemea mwanafunz atakuaje
 
Swali ni kwamba kuvaa sare ndo nidhamu?

Mbona askari wanafukuzwa kazini kila siku na wanavaa hizo sare unazokazania ndiyo nidhamu?

Hao walimu wenyewe wanafukuzwa kazi kila uchwao kwa kutokuwa na nidhamu sasa maana ya nidhamu ni sare / kuchomekea ama ni matendo ya mtu anavyoishi na jamii husika?
Nimekupa tafsiri ya nidham post namba #176
Kama hujaelewa bhas mkuu
 
Kwa ujumla nidham ya wanafunz wengi imeshuka especially shule za kata, siasa zimetawala sana unakuta mtoto anafanya makosa wakuu wa shule wanogopa kutoa adhabu kwa sababu za kisiasa kuwa wataonekani hawajali, coz suala hilo ataingiloa diwan, M/Kiti wa chama, mtendaji wa kata/mtaa/kijiji, so siasa zimezidi sana,

Lakin pia mzazi haoni umuhimu wa kumfatilia mwanane coz elimu ni bure lakini kungekuepo na ada angefatilia koz anasikia uchungu kwa ada yake, sasa halip ada anafatilia nini, mwisho wa siku nidhamu inaporomoka na ufaulu unashuka
Wizara ikitoa tamko dogo tuu la maadili inatosha mkuu. Ni swala la kuongea hadharani kwenye vyombo vya habari "mwangwi" wake unapiga kigoma hadi mtwara
 
Back
Top Bottom