Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

ila haya maisha yana mjengea mtoto woga sana .. sa nyingine unachapwa hata hujui umekosea wapi ?
utajua tu baadae ukitulia bibie kuna kauli inasema mkubwa hakosei hata akikupiga hauna kosa utatafuta tu kosa utalipata
 
hicho kizazi chenu unachokisifia ndio kimelifikisha taifa hapa lilipo...
na fimbo zote mlizochapwa lakini mikataba mnayosign hadi aibu kwa vizazi 100 vijavyo..
nyie wazee ningekua na uwezo ningebadiri katiba mshtakiwe woote kwa ujinga mliofanya na sifa za kijinga mnazotafuta sasa hivi
 
Ndio maana mmejaa nidhamu ya uoga... ndio mzee ndio mzee tuu. Profesa mzima anamnyenyekea mwanasihasa kama Mungu.
 
Inaonesha una upendo sana,, yaani nyumbani kwako hutaki ukaukiwe na wageni! Hii hata watoto wangu walikuwa nayo sana ingawa mimi nilikuwa siwachapi wakifanya hivyo! Endelea hivyo hivyo mama usibadilike. Sijui nije nikutembelee nami unililie?
Nimekuwa mkubwa mkuu. Now sililiagi watu.ule ulikuwa utoto tu
 
zaman mwalim.au baba wa mwenzenu akiwa anapita wakat mnacheza mpira mnasimamisha mnamuamkia na kama ana mzigo mnampokea mnaukimbiza hadi home kwake akivuka uwanja tu kabumbu linaendelea siku hizi ukipita katikati ya uwanja unaweza ukapigwa mtama au mpira wa kichwa na matusi juu
Kweli tupu. Waliwahi kumpiga wife na mpira akiwa na 'tumbo lake'. Wife ilibidi akae chini. Dk 5 wachezaji wote walishayeyuka!
 
Hahaha ukikatazwa kitu ukafanya lazima uchapwe tu 😀
 
zaman mwalim.au baba wa mwenzenu akiwa anapita wakat mnacheza mpira mnasimamisha mnamuamkia na kama ana mzigo mnampokea mnaukimbiza hadi home kwake akivuka uwanja tu kabumbu linaendelea siku hizi ukipita katikati ya uwanja unaweza ukapigwa mtama au mpira wa kichwa na matusi juu
Umenikumbusha mbali sana... tulichapwa bakora uwanja mzima kisa hatukumsalimia mzee mmoja wa kitaa akiwa anapita, hakuna aliyekimbia na adhabu ya kukata nyasi za ng'ombe mpaka jion...ilikuwa Frelimo iringa dah
 
342885db86057d985b262b0099b0bdfd.jpg
vijana wa kileo hao so huu ni ujanja au
una ongelea watoto au vijana
 
Ndio maana kizazi chetu kimejaa mazombi unakuta jitu Profesa lakini linaendeshwa sababu ya kuendekeza tumbo;Kizazi cha wasiochapwa wana uthubutu wa kuhoji ingawa wengi dishi limeyumba
Kizazi hiki kina uthubutu sana na ndiyo maana kinafanikiwa.
 
Hii ni mkoa wa Mara hasa hasa marneo ya Majita, Tarime , na Bunda yaani mkoa wa mara kwa ujumla nasikia ndiyo hakuna formula ya maisha nini ufanye na nini usifanye!
Si kweli, hii ilikuwa iko kila mahali siyo kwa mkoa mmoja. Leo hii mgeni yuko sitting room mtoto anaenda mpokonya simu na kuruka ruka kwenye makochi
Umenikumbusha mbali sana... tulichapwa bakora uwanja mzima kisa hatukumsalimia mzee mmoja wa kitaa akiwa anapita, hakuna aliyekimbia na adhabu ya kukata nyasi za ng'ombe mpaka jion...ilikuwa Frelimo iringa dah
Ilisaidia sana kuweka adabu na utii kwenye jamii. Ilikuwa rahisi kumpisha hata mkubwa wako sit kny gari lakini siku hizi yote hayo ni ndoto.
 
Kwa kweli hii ya mkubwa kujamba wakati mimi nipo na wakubwa zaidi ya wawili ilikuwa inanipa shida kweli..
najua mzee ally kajamba naalafu naulizwa ...nani kajamba
nikiuchuna nachapwa
nikisema mzee ally nachapwa pia
nikisema mm nachapwa pi

solution nikisikia mkubwa kajamba mm nalia tu...sinyamazi mpaka harufu pale itakapoisha

😀😀😀😀 mbavu zangu jamani!!!!
 
Nguvu nyingi akili kidogo matokeo yake kuiitikia zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Back
Top Bottom