Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

Wazazi wa Ki Africa wakatili kweli yote hayo jamani japo sikupitia vyote hapo lakin walikuwa wanatuonea,hivi unaambiwa hakuna kula kwa watu unaenda hata na mama sehemu kwa rafiki zake halaf kinatengwa chakula kizuri unatoa macho halaf mama anakukonyeza yaan anakupa ishara hakuna kulà na kuwahi kusema kuwa ameshiba huyu wakati si kweli ,maana ukiwa mdogo kula mara kwa mara ni sawa tu,kiukweli wazazi ni makatili sana
 
Nakumbuka niliwah chapwa kisa nimemgaya rafiki yangu nikawa sitembei nae na simpi ushirikiano shule ya msingi hapo,sasa siku moja akazomewa na mimi nikawa kwenye lile group la kumzomea nikawa namzoea kinafiki ,si akaenda kunisemea nyumbani kwetu kuwa siku siendi nae shule,nilichapwa siku hiyo jamani eti huyu ni ndugu yako unamuacha ili iweje ,Neema popote ulipo sikupenda kabisa kwenda kwetu kunisemea na nikala kipondo,na kipindi hicho nikipigwa au kuchapwa tu naumwa nachemka homa
 
Wazazi wa Ki Africa wakatili kweli yote hayo jamani japo sikupitia vyote hapo lakin walikuwa wanatuonea,hivi unaambiwa hakuna kula kwa watu unaenda hata na mama sehemu kwa rafiki zake halaf kinatengwa chakula kizuri unatoa macho halaf mama anakukonyeza yaan anakupa ishara hakuna kulà na kuwahi kusema kuwa ameshiba huyu wakati si kweli ,maana ukiwa mdogo kula mara kwa mara ni sawa tu,kiukweli wazazi ni makatili sana
[emoji38]...ila mkuu Mama sabrina,yalikuwa ni mojawapo ya maadiliii
 
duh![emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] old is gold! asilimia 60 nimepitia hayo..thanks mtoa mada kwa kunikumbusha long!!!
 
Ukiwahi kushiba Kabla ya mkubwa wako utachapwa pia.... Tuliopitia Haya malezi tunaishi na kila aina ya bnadam katka mazngra yoyote
 
Umeacha Juma na Rosa,Manenge na Mandawa,Kinango na Nzige nk!You can't compare with this generation!
 
Ukiwahi kushiba Kabla ya mkubwa wako utachapwa pia.... Tuliopitia Haya malezi tunaishi na kila aina ya bnadam katka mazngra yoyote
Kizazi cha sasa kinawasiojulikana!Wakihojiwa wakikosa majibu na wakabaini unakitia mchanga kitumbua chao utarajie kufanyiwa kinachojulikana na wasiojulikana.
 
Ukitumwa ukamaliza nusu saa utachapwa,

Ukienda kuzurula kwa jirani utapigwa tu,

Ukipanda juu ya miti narudia kusema utapigwa tu,

Usipokunywa dawa utapigwa tu..

Ikisadikika umetukana utapigwa tu hata mtu ukihisiwa,

Etc etc

Haaaaaaaa! umenikumbusha mbali bibi yangu anakutuma kuchota maji anatema mate chini anakuambia urudi kabla haya mate hayajakauka ole wako uchelewe utaipata mbaya.
 
Haaaaaaaa! umenikumbusha mbali bibi yangu anakutuma kuchota maji anatema mate chini anakuambia urudi kabla haya mate hayajakauka ole wako uchelewe utaipata mbaya.
Hii nayo bro ang alipenda sana kuitumia,au ananiambia kimbia kama Umeme
 
Back
Top Bottom