Kuna mtoto alienda na mama yake ugenini,dogo akagoma kula wali na maharage akasema mimi nimezoea kwetu nakula wali na mayai..
Kama alivyosema mleta uzi,yaani dogo wa darasa la 6 anadeka wakati nikiwa na umri kama huo,nilikuwa nafua nguo mwenyewe,natwanga pumba kisha nachanganya na damu ya ng'ombe nampikia ugali mbwa wa pumba na damu ya ng'ombe(watu wa machinjioni kila silu walikuwa wanatuuzia damu ya ng'ombe),asubuhi sana lazima niamke kumfungia mbwa bandani na kumfungulia saa 4 usiku,nilikuwa naenda shamba kupanda au kwenye palizi,kila jumamosi nampeleka mbwa kumuogesha kwenye ofisi za idara ya mifugo.
Wageni wakija nyumbani,nawasalimia kisha natoka nje naenda kucheza mpira.
Leo unakuta dogo hata kufagia nje hataki,kuna jamaa mmoja ana mdogo wake ana miaka 17 nilishangaa eti dogo hajui kupika ugali yeye anachojua ni kuchemsha chai tu