Watoto wa siku hizi wanadekezwa sana

Watu hawapangii wengine namna ya kulea ila hawataki kusumbuliwa na matokeo ya malezi ya mtu mwingine, mfano umepata wageni wenye watoto halafu mara watoto waanze kupanda juu ya friji, tv , meza nk, au waanze kimbizana mpaka rooms nk.
 
Kumbe wwe huwajui kina Junior,wao wanapoona wageni ndiyo huwa Sasa Wanaanza vituko vyao, Mara watake kuaangalia tv, yaani mradi fujo tu hapo Sebuleni!!
Kama ni ngeni si unawaambia wazazi wake mfanye uliloendea. Au ndiyo mgeni wa Kitanzania kuhamia kwa shemeji?
 
Kuamka na kukimbilia kwenye tv kunatengeneza kizazi cha vijana wavivu mno mno.
 
Motto akiwa na tabia njema ni wa baba akiwa na tabia Mbaya ni wa mama
 
Kuna mtoto alienda na mama yake ugenini,dogo akagoma kula wali na maharage akasema mimi nimezoea kwetu nakula wali na mayai..
Kama alivyosema mleta uzi,yaani dogo wa darasa la 6 anadeka wakati nikiwa na umri kama huo,nilikuwa nafua nguo mwenyewe,natwanga pumba kisha nachanganya na damu ya ng'ombe nampikia ugali mbwa wa pumba na damu ya ng'ombe(watu wa machinjioni kila silu walikuwa wanatuuzia damu ya ng'ombe),asubuhi sana lazima niamke kumfungia mbwa bandani na kumfungulia saa 4 usiku,nilikuwa naenda shamba kupanda au kwenye palizi,kila jumamosi nampeleka mbwa kumuogesha kwenye ofisi za idara ya mifugo.
Wageni wakija nyumbani,nawasalimia kisha natoka nje naenda kucheza mpira.
Leo unakuta dogo hata kufagia nje hataki,kuna jamaa mmoja ana mdogo wake ana miaka 17 nilishangaa eti dogo hajui kupika ugali yeye anachojua ni kuchemsha chai tu
 
Yani mimi sipendi ujinga ujinga aisee..mimi nilinyooshwa nikiwa mdogo sikuelelewa kimayai kabisa na nilikua mtoto wa mwisho..na wanangu wanafuata humo humo...ni aibu sana wtt kwenda ugenini kuvuruga vitu vya watu...lilia vitu visivyowahusu...kimbia kimbia hovyo...mimi wanangu wako very discplined yani wakienda mahali unaweza dhani hawapo..mpka warudi kwao...tumshirikishe Mungu kwny malezi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…