Watu 12 wakamatwa kwa kula hadharani mchana Zanzibar
Wewe unajitambua kweli ,uhusiano wa kula mchana na serikali ni wapi na wapi,
Wamekamata watu wanaokula mchana kwakuwa ni mwezi wa rama,
Sasa hakunaje uhusiano na uislamu!
kwani serikali ya Zanzibar inaongozwa na khalifa wa kiislamu?
 
Wakati unakaza fuvu kukashfu imani ya mtu mwingine anza kwanza kuweka hapa takataka za imani yako ilituone ni namna gani unahaki yakuona chamwenzio sio bora nachakwako ndio bora.

Hapo nasemea hizi taka taka zinazoenda kuikashifu dini ya waislamu kwatukio hilo la zanzibar.
 
Inakuwaje watu wasioshiriki mfungo wafungwe kama sio udini ? Kwani Zanzibaar ni dola ya kiislam kama Saudi? matukio haya yanazidi kutuletea hofu kwamba its har for islam to co exist with non muslims kama zilivyo nchi nyingi za kiarabu, kwamba sehemu ikijaa waislam basi haki za wasio waislam zinaminywa (Ni nchi chache kama senegal zimeweza), Haya mambo yanayoendelea Zanzibar inabidi yafutwe kabisa, ni mambo yatayoleta mazoea kukandamiza wasio waislam zaidi na zaidi kadri muda unavyoenda

HABARI YA WATU 12 WALIOKAMATWA KISA KULA .....

Kufuatia taarifa mbalimbali zilizosambaa mitandaoni zikidai kuna baadhi ya Watu Visiwani Zanzibar wana tabia za kula chakula hadharani wakati wa mchana mwezi huu wa Ramdhani, Jeshi la Polisi limefuatilia taarifa hizo na kubaini uwepo Watu hao.

Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa mjini magharibi (Zanzibar) amesema walifanya msako na kuwakamata Watu hao 12 katika maeneo tofauti ya mjini ambapo sasa wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Madema wakisubiri taratibu za kupelekwa Mahakamani.

hapo awali kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ilifanya mahojiano maalum na Mrajisi wa Baraza la Sanaa Zanzibar ambalo pia husimamia Milka, Silka na Tamaduni za Zanzibar na ambapo alizungumzia kanuni zinazopiga maarufuku mbalimbali za mwezi mtukufu ikiwemo kusimamisha shughuli za mziki, kufungua Baa, ulaji holela wa hadharani na uvaaji usio na staha.
 
Zanzibar inaendeshwa kwa sheria za dini ukienda kule fuata sheria za kiislamu..

Ni kama uko Iran, haina maana kupiga kelele.
 
Sometimes mambo mengine ni kujitakia tu. Sasa kama kule wameamua hivyo kuna shida gani kula chakula chako ndani. Utakuta mtu anatoka bara anaenda kule kufungua tamasha la muziki mwezi huu ili tu aoneshe kuwa amenyanyaswa.

When you're in rome respect romans.
 
Ukiangalia matajiri wao wakubwa wana asili ya uarabuni. Kuanzia Tanga mpaka Mtwara. Hata ukienda Tabora tatizo watanzania hatujiulizi wala hatuoni.
 
Kwa muktadha huo ipo hati hati ya hao watuhumiwa waliokula vyao mchana kweupe wakiwa wamevinunua kwa hela zao na bila kumshikia mtu bunduki ale nao kukatwa vichwa!!!

Ukikaa ukawaza kwa akili pana utagundua haya yote yanatokana na jamii fulani kukosa elimu ya kawaida kabisa ya kuchangamana na watu.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia watu kumi na mbili kwa tuhuma za kukutwa wakila mchana hadharani kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao wanaifanya kuwa idadi ya watu waliokamatwa kwa tuhuma za kutenda makosa mbalimbali kufikia sitini na mbili

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini magharibi Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Abubakar Khamis Ally amesema kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonesha baadhi ya watu katika eneo la viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar wakila hadharani wakati wa mchana wa Ramadhani, Jeshi hilo lilifanya msako na kuwakamata watu wapatao kumi na mbili wakiwa na vielelezo ambapo amesema wanaendelea na taratibu nyengine ili kuwafikisha Mahakamani.

Aidha ameyataja makosa mengine ni pamoja na unyang’anyi, Madawa ya kulevya na makosa mengine ambapo watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi na wengine tayari wameshahukumiwa Mahakamani.
Sasa kama mtu imani yake inamruhusu kula anakamatwa kwa kosa gani?
Je, jeshi la polisi Zanzibar ni tofauti na polisi wa bara?
Je, serikali ya awamu hii Ina dini?
 
Back
Top Bottom