Watu 12 wakamatwa kwa kula hadharani mchana Zanzibar
Hivi sisi majitu meusi tuna akili punje nini ? Mbona tunakumbatia hata taratibu za kishenzi kwa mgongo wa imani za kikoloni na utumwa
Hapana mkuu kule raia wengi wanakubaliana na kinachoendelea tunaopiga kelele ni watu wachache wa huku bara, tukisema kule kuna taratibu zao mnapiga makelele acha dawa iingie tu
 
Jifunze kuvumilia, kila kiumbe kwenye huu ulimwengu kina mwanzo wa upeo na mwisho wa upeo wake, tatizo linaanzia pale viumbe wengine mwanzo na mwisho wa upeo wao unakuwa ni mfupi zaidi.
 
Zanzibar inaendeshwa kwa sheria za dini ukienda kule fuata sheria za kiislamu..

Ni kama uko Iran, haina maana kupiga kelele.
Kwa hiyo huko hakuna dini nyingine? Kama zipo kwa nini wafuate utaratibu wa Mila za kiarabu?Hata akiwepo mmoja tu lazima muheshimu maamuzi yake. Wa KUFUNGA afunge wa kula ale fainali tukutane siku ya hukumu
 
Sometimes mambo mengine ni kujitakia tu. Sasa kama kule wameamua hivyo kuna shida gani kula chakula chako ndani. Utakuta mtu anatoka bara anaenda kule kufungua tamasha la muziki mwezi huu ili tu aoneshe kuwa amenyanyaswa.

When you're in rome respect romans.
Wakiwa bara kuna namna huwa wanabanwa? Au vile bara hawana time na mtu?
 
Wewe unajitambua kweli ,uhusiano wa kula mchana na serikali ni wapi na wapi,
Wamekamata watu wanaokula mchana kwakuwa ni mwezi wa rama,
Sasa hakunaje uhusiano na uislamu!
Wewe unayejitambua,
Nitajie hadithi au aya inayomtaka muhammad awaadhibu wanaokula mchana wa ramadhan.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia watu kumi na mbili kwa tuhuma za kukutwa wakila mchana hadharani kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao wanaifanya kuwa idadi ya watu waliokamatwa kwa tuhuma za kutenda makosa mbalimbali kufikia sitini na mbili

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini magharibi Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Abubakar Khamis Ally amesema kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonesha baadhi ya watu katika eneo la viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar wakila hadharani wakati wa mchana wa Ramadhani, Jeshi hilo lilifanya msako na kuwakamata watu wapatao kumi na mbili wakiwa na vielelezo ambapo amesema wanaendelea na taratibu nyengine ili kuwafikisha Mahakamani.

Aidha ameyataja makosa mengine ni pamoja na unyang’anyi, Madawa ya kulevya na makosa mengine ambapo watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi na wengine tayari wameshahukumiwa Mahakamani.
Wanalazimishwa kumtumikia shetani na mambo yake yote na kazi zake zote.... hivi Zanzibar sio Tanzania? Mbona yakija huku hayabughudhiwi? yanaishi yatakavyo? Hii ndo taibia ya Waarabu/ Waislamu, Israel wawafute kabisa kwenye ramani.
 

Attachments

  • Zanzibar.mp4
    3.4 MB
Back
Top Bottom