Watu 12 wakamatwa kwa kula hadharani mchana Zanzibar
Hapana mkuu kule raia wengi wanakubaliana na kinachoendelea tunaopiga kelele ni watu wachache wa huku bara, tukisema kule kuna taratibu zao mnapiga makelele acha dawa iingie tu
Shida tu vyombo vya serikali kujihusisha navyo, ingebaki tu kama taratibu, kanuni, mila na desturi za eneo husika ambazo zinatatuliwa Kwa maelekezo ambayo sio Sheria mfano "mtu anapoingia anaambiwa si busara kula hadharani na hata akionekana anakula anaambiwa". Ni kama tu watalii wanapoingia Kuna maeneo wanatakiwa wavae nguo za kujistiri na the same huku bara watu wakienda kijijini wanapiga nguo flani hivi

Yaani imebidi niingie chimbo kuona kama kidini inakatazwa kula hadharani na inaonekana ni rukhsa tu hadharani japokuwa Kuna nchi zina Sheria za kutokula hadharani.

All in all ukiingia / ukiishi eneo ambalo lina taratibu zake ambazo jamii imeamua kufuata basi huna budi kuji-twist uende na matakwa ya wengi
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Kwahiyo haifwati Katiba ya muungano?
Katiba inafatwa kutokana na utashi wa Rais aliyeko madarakani. Hata mahakama huamua kutokana na mtazamo wa rais anayekuwa madarakani, na sio Sheria zinavyosema.
 
Huu ni upumbavu ni sawa sawa na usikie watu mahali fulani wamekamatwa kwa kula nyama siku ya ijumaa wakati ni Ijumaa Kuu

Dini isiyoweza kuvumilia ni ya kipumbavu sana, sasa mtu kula kunakuuma nini au ni dhambi gani????
 
Matukio ya watu kukamatwa huko Zanzibar kwa kula hadharani mchana wa mwezi wa Ramadhani upo kwa miaka mingi haujaanza awamu hii.
Huo ni uhuni na haukubaliki..
Kama wewe ukikamatwa kwa kutozingatia ibada za dini isiyokuhusu utaelewa?!

Kuna siku Freemason nao watasema wamefunga kula na hivyo lazima kila mwananchi afunge kama wao.

Kama mtu kafunga kwa kumaanisha mambo ya wengine kula hayawezi kumsumbua.

Kama ndivyo, itakuwaje mfungo ukikukuta bara, utaweza kuzuia watu kula?
 
Kwa hiyo huko hakuna dini nyingine? Kama zipo kwa nini wafuate utaratibu wa Mila za kiarabu?Hata akiwepo mmoja tu lazima muheshimu maamuzi yake. Wa KUFUNGA afunge wa kula ale fainali tukutane siku ya hukumu
Jitahidi kuelewa.
Zanzibar asilimia 90 ni waislamu, sheria zinazotumika zinaelemea dini ya kiislamu.

Ukiwa Zanzibar, kama una busara, utajitahidi kuendana na huo utamaduni wao wa kiarabu, kujaribu kulemaza shingo haisaidii.

Nimetoa mfano, ni sawa na mtu kwenda Iran, halafu ukajidai eti hutaki kufuata taratibu zao, utakuwa ni mjinga.
 
Hivi sisi majitu meusi tuna akili punje nini ? Mbona tunakumbatia hata taratibu za kishenzi kwa mgongo wa imani za kikoloni na utumwa
Jambo la kuhoji ni je Serikali ya Mapinduzi ni Secular? Kama jibu ni Secular ni kwanini inajiingiza ku enforce Sheria za Dini?

Tunahitaji Mjadala mpana sana kwenye hili jambo.

Kwasababu Serikali ya Jamhuri ya Muungano ni Secular.
 
Shida tu vyombo vya serikali kujihusisha navyo, ingebaki tu kama taratibu, kanuni, mila na desturi za eneo husika ambazo zinatatuliwa Kwa maelekezo ambayo sio Sheria mfano "mtu anapoingia anaambiwa si busara kula hadharani na hata akionekana anakula anaambiwa". Ni kama tu watalii wanapoingia Kuna maeneo wanatakiwa wavae nguo za kujistiri na the same huku bara watu wakienda kijijini wanapiga nguo flani hivi

Yaani imebidi niingie chimbo kuona kama Kuna kidini inakatazwa kula hadharani na inaonekana ni rukhsa tu hadharani japokuwa Kuna nchi zina Sheria za kutokula hadharani.

All in all ukiingia / ukiishi eneo ambalo lina taratibu zake ambazo jamii imeamua kufuata basi huna busi kuji-twist uende na matakwa ya wengi
Umeeleza vema ndugu, sina la ziada la kuongeza
 
Back
Top Bottom