Watu 48 waokolewa mafuriko Morogoro

Watu 48 waokolewa mafuriko Morogoro

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando amewasili mapema asubuhi leo Ijumaa Januari 13, 2023 eneo la Kihonda mahali ambako wananchi wameathirika zaidi huku akisaidia kuokoa watu na mali zao.
👍
 
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wapo kwenye maeneo mbalimbali Manispaa ya Morogoro wakiendelea kuokoa watu na mali zao.
1673619468825.png


1673619468825.png

Alijumuika nao
 
13 January 2023
Morogoro, Tanzania

Wananchi wanyooshea kidole mradi wa reli SGR

 
Mara nyingi mto msimbazi hujazwa na maji toka mvua za morogoro, hivyo, daresalamu inaweza isinyeshe mvua kubwa lakini mto ukajaa, tena kwa bahati mbaya haya hutokea usiku wakati watu wamelala, tuwe makini sana sisi wakongwe wa jiji tunafahamu hili sana.

==== ====

Mvua kubwa iliyonyesha usiku kuanzia majira ya saa nane hadi alfajiri, imesababisha mafuriko na kuleta hofu kwa madereva kuendesha magari katika maji hayo yanayokatisha juu ya barabara ya Morogoro - Dodoma.

Chanzo: ITV
Haiwezekani mvua ya Moro kujaza mto Msimbazi
 
Aisee kuna mafuriko ya hatari yanaendelea muda huu Morogoro mjini tangu saa 10 usiku hadi sa hivi bado yanaendelea.

Mimi nipo Kihonda huku watu kibao hawajalala wanapambana kutoa maji yalioingia ndani na kuokoa vitu vyao.

Mvua likikata tutegemee habari za vifo na watu kubomokewa nyumba tu, mvua inapiga kwa sifa kama haitopiga tena. Aisee ni balaa!

PICHA/VIDEO

View attachment 2479141


View attachment 2479185
View attachment 2479186
View attachment 2479187
View attachment 2479190
View attachment 2479207

----- --- -------

Mvua yasababisha mafuriko, foleni Morogoro
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro kuanzia saa 9 alfajiri, zimesababisha madhara mbalimbali kwa wakazi wa mkoa huo ikiwa ni pamoja na mafuriko na foleni ya magari Barabara kuu ya Morogoro kwenda Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando amewasili mapema asubuhi leo Ijumaa Januari 13, 2023 eneo la Kihonda mahali ambako wananchi wameathirika zaidi huku akisaidia kuokoa watu na mali zao.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wapo kwenye maeneo mbalimbali Manispaa ya Morogoro wakiendelea kuokoa watu na mali zao.

Asante ila tambua mvua haipigi ila inanyesha!,
 
Back
Top Bottom