Watu hawataki kutembeleana siku hizi, kila mmoja yuko bize kusaka shilingi

Watu hawataki kutembeleana siku hizi, kila mmoja yuko bize kusaka shilingi

Hata hivyo wengi hawataki yale maisha ya umbea nakufuatiliana sana we unazani mke wako atakubali kuwa anatembelewa na dada zako nyumbani kwako si unajua sisi waswahili tena maneno mengi

Watu wengi wameamua kuwa na majamaa na sio marafiki hiyo hali ndio imechangia sana kutokutembeleana
 
Tatizo lilianzia kwako Mkuu, kosa lako ni hili hapa:-

Unampigia simu mtu unamuambia upo maeneo aliyopo, unaomba kuonana naye halafu unapanga kuonana naye kwake yaani unajikaribisha kwa mtu

Hata mimi ningekukataa tu Mkuu, ulitakiwa, baada tu yakumuambia upo maeneo aliyopo, ungeomba kuonana mahali mpate kuongea mambo mawili matatu.

Sasa yeye ndio angepima na kukukaribisha kwake ama kukuuliza ulipo afanye michakato muweze kuonana.

Atakuwa amekuona unataka kujua mambo/maisha yake akaona akukatae tu Mkuu, usilaumu wala, ni maisha yalivyo tu.
 
Muongo Muongo tu alisema yupo busy na hapo nilipokuepo na eneo alilokuwepo ni kama 200M tu. Kichwani nikajua tu huyu hataki shobo za kijinga, nikamwambia fresh nipo leo na kesho akasema atanicheki ndio ikatoka hiyo mpaka leo.
Watu wanabadilika
 
shida kuna watu wakikutembelea kazi yao ni udadisi wa kijinga.
binafsi hata fundi akija kwangu nikaona anaangazaangaza macho na kuliza mambo yasiyohusiana na kilicho mleta namwambia chukua vifaa vyako hakuna kazi tena
 
Naona alikuwa busy kweli. Next time moe.muda wa kutosha na uende wakati hana kazi.

Binafsi sijaona tatizo lolote hapo, hakuwa na nafasi hiyo siku.
Mimi naona vinginge: huyo mzee mkoa aliohamia mambo hayakumuendea vizuri, kutahamaki keshafulia na huenda aliuza kila kitu ili kujikomboa, lakini akapoteza kila kitu. Sasa amepanga banda la uani hana kitanda wala kiti. Kwa mazingira hayo lazima akimbie marafiki wa zamani
 
Binafsi nadhani ni maamuzi ya jinsi unavyotaka kuishi na cycle yako.

Tengeneza cycle ambayo mnaweza kuamua mkutane lini, wapi ili mfurahie kidogo.

Nimeijaribu hii, inatusaidia sana kwa kweli, na kuna wakati mwambie kaka/dada yako aje na familia weekend muwe pamoja. Sijui tumemuwaje hakyanani!!
 
Ndio haya mabadiliko yapo, lakini ni nini mwisho wake?
Zamani watu waliweza kutembeleana kwasababu hatukuwa na matumizi mengi yanayohitaji hela.

Hakuna umeme (baadhi ya maeneo), simu wengine walikuwa hawana, vifurushi bei rahisi, vyakula vilikuwa vingi kwasababu hakukuwa na mabadiliko ya hali ya hewa, tunatumia antena (analogia), nauli bei nafuu, upatikanaji wa kazi ni rahisi n.k.

Sasa hivi matumizi yamekuwa mengi na upatikanaji wa pesa siyo rahisi.

Matumizi ya kila siku ambayo unatakiwa utumie, Bando ya internet, king'amuzi, bando la dk na sms, umeme na maji. Vyote hivyo vinahitaji hela.

Nikutafuta shilingi muda wote
 
Kwa mazingira hayo, wengi hatufurahii maisha kwa sababu muda mwingi tuko bize kwenye kutafuta shilingi, mwingine jumatatu mpaka jumapili muda wote ni bize; katika hali hii tukisema maisha ni utumwa tutakuwa tumekosea?​
 
Hata hivyo wengi hawataki yale maisha ya umbea nakufuatiliana sana we unazani mke wako atakubali kuwa anatembelewa na dada zako nyumbani kwako si unajua sisi waswahili tena maneno mengi

Watu wengi wameamua kuwa na majamaa na sio marafiki hiyo hali ndio imechangia sana kutokutembeleana
Au elimu ya mkoloni ndio inatubadilisha kutoka kwenye tamaduni za zamani?
 
Back
Top Bottom