Zamani watu waliweza kutembeleana kwasababu hatukuwa na matumizi mengi yanayohitaji hela.
Hakuna umeme (baadhi ya maeneo), simu wengine walikuwa hawana, vifurushi bei rahisi, vyakula vilikuwa vingi kwasababu hakukuwa na mabadiliko ya hali ya hewa, tunatumia antena (analogia), nauli bei nafuu, upatikanaji wa kazi ni rahisi n.k.
Sasa hivi matumizi yamekuwa mengi na upatikanaji wa pesa siyo rahisi.
Matumizi ya kila siku ambayo unatakiwa utumie, Bando ya internet, king'amuzi, bando la dk na sms, umeme na maji. Vyote hivyo vinahitaji hela.
Nikutafuta shilingi muda wote