DUNIA KIGANJANI
Waliotunga huu msemo hawakuwa wajinga, kuna watu ama jamii ambayo inaunda mifumo ya kuziunganisha jamii zote dunian bila kujali tamaduni, dini na rangi sehemu moja(mtandao), ambapo utaweza kupata kila kitu within the short time.
Itafika mahala hatutokuwa na umuhimu wa kufanya kazi,kukutana kijamii, kwenda mahospitali ama kuzunguka kufanya shopping, bali kutakuwepo na AI instruments zitakazo fanya kazi kwa mbadala wa mwanadamu, kuanzia kazi za kijamii mpaka kiuchumi , huku binadamu akiwa kama msimamizi tu wa shughuli hizo kupitia kifaa cha mawasiliano baina yake na hizo artificial tools.
Tulipo fika hapa si kwa bahati mbaya bali kuna watu/jamii wanao weka effort kubwa kuunda mifumo ambayo huleta impacts kwa jamii hata baada ya miaka mingi mbeleni.
Tunavyoongelea haya sasa hivi kuna matajiri kama akina Elon musk wao wanaumiza akili kuunda bidhaa ambazo zitapunguza matumizi ya nguvu kazi ya mwanadamu, pia hawa hawa wanaunda hata akili bandia na wanadamu feki(robots) ambao wanaweza kufanya shughuli za kijamii mbadala wa mwanadamu.
Si hao tu kuna hata mikutano ya nchi na mashirika hufanyika ili kuunda mifumo ya Pesa isiyoshikika(pesa ya kidigital) na vitambulisho vya utaifa na kadi za kibenki kupitia kifaa kidogo ambacho kitajumuisha kuifadhi mifumo mingi ambayo leo hii mifumo hii imegawanyika na ina milolongo mingi.
Kiufupi jamii wanayoijenga ni ile ya ubinafsi, upekeako, kujipenda wewe mwenyewe, kujiamini wewe mwenyewe, utegemezi ktk mashine+ Computer+akili bandia ambayo binadamu kaitengeneza kwa akili zake lakn maajabu anaitegemea imtatulie matatizo zaidi ya akili yake.
Nimeandika haya yote kuonesha kwamba huu utaratibu wa kuacha kufanya yale mazoea na tamaduni za kijamii inakwenda kufa kama sio imeanza kufa, maana kuna mifumo ambayo watu walidesign iwe hivi miaka ya nyuma kwa manufaa yao.
Manufaa yao ni yapi kwa mujibu wao? [emoji116]
[emoji117]kuunda jamii mpya yenye ustaarabu, ubinafsi na tabia ambazo wanaita wao utandawazi.
[emoji117]kuunda jamii mpya ya watu walio Under control ya watawala wa kinchi na mamlaka zingine za kiserikali+kidini, kwasasa binadamu bado hajawa wa kutawalika kiurahisi sababu ya ule uhuru wa maamuzi/ uhuru wa kuamua jambo, ama uhuru wa kupinga jambo, basi kinaandaliwa kizazi cha kisukule ama kiroboti chenye akili iliyopumbazwa ambayo itaamini lolote litakalosemwa na mamlaka ya serikali ama Tawala ya dunia, yaani kiufupi kizazi icho kitaamin taarifa yoyote itolewayo na Media ama inayozungumzwa sana na media ama published information kuliko hata kutumia common sense kufikilia jambo.
Kizazi ambacho kitafanya lolote kinaloambiwa, yaan miaka ijayo usishangae kuona ile Free will ikafa, mtu hata akiambiwa fanya ngono na mnyama ili uongeze kinga za mwili, nae atafanya hivyo sababu ni Media imesema ama ni government order, hakuna muda wa kuhoji wala kujiuliza ni kutii tu, hata ukiambiwa meza dawa fulan watu watatii maana ni habari inayozungumzwa na wengi, hivyo watu wataamini ktk populality+trending news kwa kuamini kwamba jambo linalovuma sana ama nilalosemwa sana basi hilo ni kweli.
Huko ndiko tuendako, haya hayatokei kwa bahat mbaya wandugu haya yanapangwa kabisa ndiomaana wanaharibu mifumo mizima ya kijamii kama ushirika wa kijamii wa kushare habari na hisia za kijamii ili kuzuia ile hali ya watu kuelezana tofauti zao, bali wao wanataka kama kitu unakiamin baki nacho pekeyako na ukiamini hata kama ni uongo/kweli baki nacho, maana ukikifikisha ktk jamii kitapata muda wa kujadirika na kuzungumzwa pia kikatolewa mapungufu, hivyo jamii inakuwa na Common sense ama uwezo kuyakabili mambo na kupata solution.
Kizazi hiki kimeharibiwa kwa kuletewa mifumo ya elimu inayo mkomoa mtoto tangu anazaliwa mpaka anakuwa mtu mzima, yaan unapozaliwa unalishwa habari nyingi useless zinazokukeep busy bila faida yoyote, ukiondoa elimu mzigo bado kuna mambo ya burudani haswa mpira na muziki, haya ndio yanamuweka kabisa mwanadamu kifungon ama ktk utumwa wa kufuatilia mambo ya kijinga anayoamin ni burudan kumbe yanamuweka bize asifikirie mambo ya msingi.
Huko ktk hizi burudan feki kuna Pesa nyingi zinakuwa Funded/kudhamini hii michezo ili ienee dunia nzima ama ifanyike kila muda na kila mwaka pasipo manufaa yoyote ktk jamii.
Jiulize zile trillions zilizotumika kufanya michezo ya mpira wa kombe la dunia zimeleta matokeo gan kwa jamii? Watu wamepata nini nje ya burudan ovu ya muda mfupi waliyoifanya huko viwanjani?
Zile pesa kwanini wasingetumia ktk mambo ya msingi kama kukuza uchumi wa wananchi na nchi masikin badala yake zinatumika kufanya maonesho ya kipumbavu ambayo hayana faida kwa jamii?
Hapo utagundua kuwa kuna jamii nyuma ya pazia zina dhamini haya mambo kwa kumfanya mwanadamu haswa muafrika kuwa kiumbe mpumbavu, mjinga, mshenzi na mtumwa wa mifumo yao(MSUKULE/ROBOTI).
Tupo hapa, miaka 5-10 ijayo mtayapata haya matokeo maana ndiko tuendako na tushaanza hatua nyingi sana
Kizazi kijacho kitakuwa cha kishenzi na kipuuzi sana, lkn haiondoi uwepo wa wachache wenye akili ktk hilo kundi la wapumbavu wengi.
WE ARE UNDER THE GREATEST DEVIL'S CONTROLLING SYSTEMS.