Watu hawataki kutembeleana siku hizi, kila mmoja yuko bize kusaka shilingi

Ubize wa maisha utatufanya watoto wetu waoane wenyewe kwa wenyewe utakuta mtoto wa bamkubwa anaanzisha mahusiano na mtoto wa bamdgo hii yote kutokutembeleana so kadhara yapo pia
 
Ubize wa maisha utatufanya watoto wetu waoane wenyewe kwa wenyewe utakuta mtoto wa bamkubwa anaanzisha mahusiano na mtoto wa bamdgo hii yote kutokutembeleana so kadhara yapo pia
Na hii kuwa bize sana kwenye kutafuta hela, inapelekea kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili
 
Dunia imeharibika
 
teknolojia imerahisisha maisha.
kama tumeshaongea kwa njia ya simu unataka tuonane ili iwe je? tupige selfie au?

kama shida ni pesa kuna mobile transactions za kutosha.
kama ni parcel kuna currier companies kila kona - kwa njia zote: nchi kavu, maji, anga. unachagua tu.

sasa hivi mtu unaonana na familia yako tu - mkeo/mumeo na watoto wenu.
 
Huu utamaduni tumeutoa wapi?
people don't have the best interest in you. unafiki ni mwingi sana. naongea kwa experience.
watu wanakutafuta ili wapate chochote kutoka kwako.
mtu unamkopesha pesa ikifika muda wa kumdai ugomvi. sasa yanini kujuana?

kama shida ni bia nnachukua kibunda changu naenda baa nakaa kaunta nanyonya vyombo vyangu nikimaliza nalipa bili yangu nakula kona kivyanguvyangu. maisha mazuri kabisa yasiyokuwa na stress.
 
Ratiba tu zimebadilika,hizi sio enzi za kutoka shamba saa7 mchana na kurudi kukaa kivulini kuvuta kiko, mtu utamkuta nyumbani saa ngapi? Ni kawaida tu hata wewe kuna muda huwezi onana na mtu
 
Hapo kwenye Technology Hapo
Umemaliza kazi Uncle.
 
We mara ya mwisho kumtembelea mshikaji wako nilikuwa lini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…