Watu 'Powerful' 12 ni akina nani hadi waachiwe kuharibu Bonde la Ihefu?

Watu 'Powerful' 12 ni akina nani hadi waachiwe kuharibu Bonde la Ihefu?

HIZI FAMILIA 12 ZILIZOJENGA UKUTA KUZUIA MAJI YASITEREMKE MTO RUAHA KINA NANI HAO


KWANINI MAKAMU ASINGEAMURU SIKU ILEILE YALETWE MAGREDA YAVUNJE HUO UKUTA??NANI YUKO NYUMA YAO??

KUNA UKUTA FLANI UMEBOMOLEWA MAJUZI TENA KABLA YA KIONGOZI AJAONDOKA NAO WALIKUTWA WAMEZUIA MAJI...

HAWA NANI WASIVUNJIWE MPAKA SASA HUO UKUTA??

USIHAME TANZANIA...
N
 
Utakuta Hawa Wanafamilia 12, wameanza hii shughuli baada ya JPM kufariki.


Tumtume nani Sasa?? Mipango?? Ataweza kweli ??
Mipango hawezi, kwenye mkutano na wananchi alipewa majina, hata moja hajalitaja. Usalama wa taifa wanajua hujuma hiyo, na mkuu wao anajua wahusika lakini ana ongea tu!
 
21 November 2022
MFEREJI ULIOJENGWA UKUTA MKUBWA KUZUIA MAJI KUINGIA MTO RUAHA MKUU WAANZA KUBOMOLEWA
-



Ni utekelezaji wa maagizo 10 ya Makamu wa Rais kuhakikisha mabanio yote haramu ya maji yanabomolewa - Inakadiriwa umegharimu zaidi ya Milioni 400.

- Kazi zaidi inahitajika kufanyika kubomoa kingo nyingine Siku chache baada ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango kuzielekeza Mamlaka zinazosimamia mto Ruaha Mkuu kuhakikisha vizuizi vyote vinaondolewa Ili kuuruhusu mto huo kutiririsha maji kama kawada.

Moja kati ya kizuizi kikuu Cha mto Ruaha kupata maji kimeanza kuondolewa Hapa ni Kata ya Imalio Usongwe katika mfereji wa nguvu kazi Mwanavala unaopeleka maji katika mashamba ya mnazi katika eneo la Warumba yanayotakiwa kuingia katika Mto Ruaha Mkuu na kuelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Bwawa la Mtera, Kidatu, Bwawa la Nyerere na hatimaye Bahari ya Hindi.

Zoezi la kubomoa mabanio haya yasiyorasmi yanayotumika kuchepusha kinyume na sheria kutoka katika Mto Mfereji huu unakadiriwa kuwa umejengwa kwa zaidi ya Milion 400 miaka kadhaa nyuma.

Jitihada za kuuokoa mto Ruaha Mkuu kuufanya uwe unatiririsha maji mwaka mzima Zinaendelea na Mto Ruaha kuacha kukauka mwaka mzima INAWEZEKANA.

Ukiokoa mtiririko wa Maji mto Ruaha Mkuu maana yake umeoko na kuilinda Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Maana yake pia umalihakikishia Taifa Upatikanaji wa umeme katika Bwawa la Mtera, Kidatu na Nyerere linaloelekea kukamilika.
Source : JAMVI online TV
Watu wa kwanza kuchapwa viboko ni mamlaka za usimamizi wa mto Ruaha. Vizuizi vyote vinajengwa wapo na wana kula mishahara.
 
Nimemsikiliza ndugu yangu Balile! Kwa aliyosema ni mambo mazito yanayofanya kama Taifa tujiulize mamlaka zetu hasa za usalama wanamuogopa nani kwenye ulinzi wa rasilimali zetu?

Balile binafsi nimekupa heshima ya pekee kwa hili.
Mamlaka za usalama zimebaki na kazi ya kuhakikisha CCM inashinda na kumlinda rais.
 
Hao watu powerful wapo tanesco
Hao watu powerful wapo TRA
hao watu powerful wapo BOT
hao watu powerful wapo Bandari

Yaani kila sehemu wapo hatuwezi kuendelea kwa style hiyo.
 
Watu wa kwanza kuchapwa viboko ni mamlaka za usimamizi wa mto Ruaha. Vizuizi vyote vinajengwa wapo na wana kula mishahara.
Mkuu usiwalaumu hawana nguvu yoyote ya kuwaondoa wao ni wadogo sana kwao unataka wafukuzwe kazi wakati hawana pakwenda hujasikia huyo mtoa taarifa amesema waliojaribu kusema wote wamepotezwa na wengine kuuliwa.
 
Ni taarifa inayoonesha kwamba hatutaendelea. Tuna kundi la watu wa hovyo, lakini wanaitwa ni powerful!
Kwa maoni yako endelea;

Unapoona mpaka Mtendaji wa Kijiji au Mtaa anashiriki wizi wa kura ama kuharibu Uchaguzi in favor for CCM ujue ana maslahi binafsi ndani ya serikali ya CCM. Ndo maana wengi wanaoteuliwa wanakuwa branded kuws WAMEULA
 
Na wao wanasema Magufuli alikuwa shetani
Ndio nasema hayo majina yote yana sababu zake, Magufuli kaitwa dikteta kaitwa shetani kutokana na aina ya uongozi wake na Kikwete kaitwa dhaifu kutokana na aina ya uongozi wake ulivyokuwa.
 
Ndio nasema hayo majina yote yana sababu zake, Magufuli kaitwa dikteta kaitwa shetani kutokana na aina ya uongozi wake na Kikwete kaitwa dhaifu kutokana na aina ya uongozi wake ulivyokuwa.
Kumbe? Sasa akiitwa shetani usikasirike
 
Back
Top Bottom