Watu wa Pemba mnaweza vipi kuishi sehemu pagumu kama huku?

Watu wa Pemba mnaweza vipi kuishi sehemu pagumu kama huku?

Wabara na Wahuni kuitwa Wanyamwezi ni sababu ya watu wawili,
Hiyo ya wahuni sijui, lakini wabara kuitwa Wanyamwezi siyo sababu ya Lipumba na Mapalala.

Katika miaka ya arubaini mpaka sitini (enzi ya Muingereza) ikifika wakati wa kuchuma karafuu Pemba kulikuwa na meli inakuja kuchukua vibarua kutoka Bara (enzi hizo Tanganyika). Waliokuwa wanakwenda Pemba kipindi hicho kwa asilimia kubwa walikuwa Wanyamwezi/Wasukuma na Wadigo kutoka Tanga. Aidha vijana wengi na wafanyabiashara kutoka Unguja walikuwa wanahamia Pemba kwa muda. Kwa kweli fedha ilikuwa nje nje katika kipindi cha karafuu. Hata wahindi walikuwepo kwa wingi sana na maduka yao yakiuza kila unachokitaka na hasa mapambo ya wanawake kutoka India.

Uchumaji wa karafuu unahitaji vibarua wengi ili karafuu zichumwe kwa muda mfupi bila kuharibika (zinachumwa katika stage maalumu ya ukuwaji) otherwise zinaharibika na kuwa 'matende' na zinakuwa hazina thamani kibiashara. Kwa hivyo nguvukazi ilikuwa inakuja wanapiga mzigo na baadae wanarudi nyumbani. Lakini kama kawaida kuna baadhi huwa wanabakia kule kule na kuendelea na maisha yao. Hawa waliobaki wengi walikuwa ni Wanyamwezi na ndiyo maana wabara wote tena wakaitwa hivyo.

Enzi hizo karafuu ilikuwa na bei kweli kweli kwa hivyo msimu wa kuchuma karafuu ilikuwa kama sherehe fulani hivi visiwani. Walikuwepo 'wauza urembo (mapambo ya kina mama)' walikuwa wanauza mpaka vijijini. Mfano mfanyabiashara akikutana na mtu akanunua kitu lakini akapungukiwa na fedha basi atamkopesha na yule aliyekopa atamlipa tu hata kama watakutana baada ya mwaka mmoja (walikuwa waaminifu sana).
 
Pemba patamu yahe. Usisahau kufika pale Gombani na Macho manne.
UKifika Macho manne utapata kila utakacho, Wete halikadharika...ingawa macho wengi yatakunyima Uhuru.
Ukichukua ngoma Wete au Macho manne inabidi ukaipigia kusini, yaani mkoa mwingine.

Wabara na Wahuni kuitwa Wanyamwezi ni sababu ya watu wawili, wa Kwanza James Maparara aliyekua mwanzilishi na Mwenyekiti wa CUF, wa pili ni Ibra Lipumba...hawa Wanyamwezi wawili kwao ndiyo brand ya Wabara
Muongo Sana wewe,tangu zamani watu wanaoenda Sana visiwani ni wanyamwezi,hata vibarua mashambani ni wanyamwezi,Sasa wao kila atokae Bara humuita mnyamwezi,kabla ya mapalala na lipumba
 
Nimecheka hapo eti "Samaki Pemba ni bei ghali kuliko Singida"je umeweza kujua sababu ni nin?...
 
Hivyo vitu ambavyo umeviorodhesha karibu vingi kama siyo vyote vinapatikana Zanzibar nzima. Nafikiri wengi wao kwa asilimia kubwa hufuata misingi ya dini yao ya kiislamu.

Ila naamini wengi wao huifuata hii dini kama utamaduni na siyo kiimani.Masharti ya hii dini kwa kizazi cha leo bila imani thabiti na kujitoa inahitaji moyo sana kuyafuata. Ndiyo maana unafiki umejikita mizizi sana. Mfano wa masharti hayo ni kama vile:

1) Usinywe pombe: (Umezungukwa na baa pande zote)

2)Usicheze kamari: (Umezungukwa na kampuni za kamari pande zote.)

3)Usifanye umalaya : (Umezungukwa na madanguro yanayonekana na yasiyoonekana pande zote)

4)Usitoze riba: (Huku unahitaji faida maradufu)


................................n.k bila nguvu ya Mungu utachemsha tu na kuwa mnafiki mkubwa.

Kingine ni suala la chuki dhidi ya watu kutoka bara, hii huambukizwa tangu utotoni sijui ni nini kilitokea lakini jamaa wanawachukia watu kutoka bara kuliko maelezo.

Hii nayo ni ujinga wa kurithishana, naamini kiasili kisiwa hakina mwenyewe kiasilia kwani hata hawa wanaolishwa hizi sumu ukiwafuatilia kiundani asili za mababu zao unakuja kugundua kuwa walihamia huku visiwani muda mrefu!!!!!!!!!!!!

Wengi wao hasa wanaokaa shamba, hawajafanikiwa kutembea nje ya visiwa hivi, ni kama mtu unakaa sehemu moja muda mrefu ukiamini kuwa ni sehemu bora kuliko sehemu nyingine, ukitoka utagundua kuwa dhana yako ilikuwa potofu!!!!!!!!!

Nb 1: Naamini Mungu hana dini (Mtazamo wangu).

Nb 2: Dini zote zimeundwa na kutengenezwa na mwanadamu (Mtazamo wangu)

Nb 3: Huwezi (mtazamo wangu ) kutenganisha dini na utamaduni wa jamii husika. Mfano:


1) Utamaduni wa kimagharibi na Ukristo.

2) Utamaduni wa Kihindi na Uhindu.

3)Utamaduni wa Kiyahudi na Uyahudi.

4)Utamaduni wa Kiarabu na Uislamu.

5)Utamaduni wa kichina na Confucianism, Taoism, and Buddhism.

6)Utamaduni wa Kijapan na Shinto na Buddhism.

7)Utamaduni wa kirusi na orthodox.

Nb 4: Tunatofautina kiimani na kiitikadi lakini tukiheshimiana hutaweza kuziona hizo tofauti.

Nb 5: Binadamu wote tunategemeana.

Ni mtazamo tu!!!!!!!!!!!!!!!!!
Uislam ni Mila/utamaduni unaojitegemea,unaposema wanafuata Kama Mila unadhihirisha uelewa wako mdogo wa Mila na dini,chuki kwa Wabara inakuja kwa kuwa muungano ni WA kulazimisha,wanaamini hivyo,wanaamini muungano umewarudisha nyuma na umeharibu utamaduni wao, unaposema mungu Hana dini unatia shadda kwenye umbumbumbu wako kuhusu mungu
 
Back
Top Bottom