Hivyo vitu ambavyo umeviorodhesha karibu vingi kama siyo vyote vinapatikana Zanzibar nzima. Nafikiri wengi wao kwa asilimia kubwa hufuata misingi ya dini yao ya kiislamu.
Ila naamini wengi wao huifuata hii dini kama utamaduni na siyo kiimani.Masharti ya hii dini kwa kizazi cha leo bila imani thabiti na kujitoa inahitaji moyo sana kuyafuata. Ndiyo maana unafiki umejikita mizizi sana. Mfano wa masharti hayo ni kama vile:
1) Usinywe pombe: (Umezungukwa na baa pande zote)
2)Usicheze kamari: (Umezungukwa na kampuni za kamari pande zote.)
3)Usifanye umalaya : (Umezungukwa na madanguro yanayonekana na yasiyoonekana pande zote)
4)Usitoze riba: (Huku unahitaji faida maradufu)
................................n.k bila nguvu ya Mungu utachemsha tu na kuwa mnafiki mkubwa.
Kingine ni suala la chuki dhidi ya watu kutoka bara, hii huambukizwa tangu utotoni sijui ni nini kilitokea lakini jamaa wanawachukia watu kutoka bara kuliko maelezo.
Hii nayo ni ujinga wa kurithishana, naamini kiasili kisiwa hakina mwenyewe kiasilia kwani hata hawa wanaolishwa hizi sumu ukiwafuatilia kiundani asili za mababu zao unakuja kugundua kuwa walihamia huku visiwani muda mrefu!!!!!!!!!!!!
Wengi wao hasa wanaokaa shamba, hawajafanikiwa kutembea nje ya visiwa hivi, ni kama mtu unakaa sehemu moja muda mrefu ukiamini kuwa ni sehemu bora kuliko sehemu nyingine, ukitoka utagundua kuwa dhana yako ilikuwa potofu!!!!!!!!!
Nb 1: Naamini Mungu hana dini (Mtazamo wangu).
Nb 2: Dini zote zimeundwa na kutengenezwa na mwanadamu (Mtazamo wangu)
Nb 3: Huwezi (mtazamo wangu ) kutenganisha dini na utamaduni wa jamii husika. Mfano:
1) Utamaduni wa kimagharibi na Ukristo.
2) Utamaduni wa Kihindi na Uhindu.
3)Utamaduni wa Kiyahudi na Uyahudi.
4)Utamaduni wa Kiarabu na Uislamu.
5)Utamaduni wa kichina na Confucianism, Taoism, and Buddhism.
6)Utamaduni wa Kijapan na Shinto na Buddhism.
7)Utamaduni wa kirusi na orthodox.
Nb 4: Tunatofautina kiimani na kiitikadi lakini tukiheshimiana hutaweza kuziona hizo tofauti.
Nb 5: Binadamu wote tunategemeana.
Ni mtazamo tu!!!!!!!!!!!!!!!!!