Watu wanaongelea pesa za kichawi bila uthibitisho, Kama ni kweli zinapoingia kwenye account anaetuma ni nani ?

Watu wanaongelea pesa za kichawi bila uthibitisho, Kama ni kweli zinapoingia kwenye account anaetuma ni nani ?

watu kibao

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
466
Reaction score
1,663
Naweza kuamini pesa inaweza kupatikana kwa njia nyeusi na hatarishi kama ujambbazi lakini si nguvu za giza.

Yani utoke tu huko kwa mganga uzikute zimedondoka chumbani kama furushi la magimbi, hizi bi hadithi za sungura na fisi.

Kama ni muamala benki zinarekodi kila kitu, jina huwa ni la nani ?

Nachojuwa waganga ni wajanja, walishajua vitu vinavyofanya watu wengi wawe masikini ni starehe, uvivu, matumizi makubwa, n.k. nao wanacheza humo humo watakupa masharti ya kujibana, kupunguza starehe, kuchapa kazi mpaka kieleweke, kuweka aibu pembeni, n.k. mambo ya kafara huwa ni kumsisitiza mtu awe serious,.

Oneni wachina wamegusa kidogo tu nchi kelele zimejaa hapo Kariakoo, wao wanachotumia ni hizo principle za biashara,
 
Back
Top Bottom