Watu wazima wanaojitapa kuzaliwa Dar ni mojawapo ya watu wa ovyo sana

We nakwede97 mbona povu hivi? Kama vipi hama huko Kwimba uje Dar upunguze hasira..!! Maana si kwa povu hili aisee..!!! Yaani umeongea kama vile wote wa huko Namabengo au Runzewe mna apatimentiiii..!!! 😀 😀 😀 😀 😀
 
Kuzaliwa dar ni elimu tosha na kwamba umeanza kupata ustaarabu zamani sana kwahiyo punguza makasiriko
Hata kule marekani ukikulia new york wewe ni mjanja kuliko wa majimbo mengine
 
Cha ajabu, mtu anatamba, eti mwingine anaumia..!! Waliozaliwa Rungemba au Lupapira ndo wanaumia sana
 
Hatuna Sasa nyie mda wote dar mtadhan mmejenga magorofa kumbe wadandia daladala 🙄 Bora na sisi wa huku hatuna mbwembwe
 
Hatuna Sasa nyie mda wote dar mtadhan mmejenga magorofa kumbe wadandia daladala 🙄 Bora na sisi wa huku hatuna mbwembwe
Kwahiyo akitamba aliyezaliwa Dar huku amejenga gorofa ni sawa??? Sasa fikiria mtu huna gorofa na umezaliwa Iselamagazi..!!
 
Ukiwa Katavi Dar ni mkoani pia,Mikoani nje ni nje ya mkoa uliopo
 
Dar ndio kila kitu hata ukiandika kwenye CV kuwa umezaliwa Dar ni added advantage compared to mtu aliezaliwa Ushirombo. Sio kila mtu anapata chance adhimu ya kuzaliwa Dar only kwa wachache na wenye bahati.
Cha kushangaza vijana kutoka mikoani ndio wanakuwa maraisi wa nchi hii. Kariakoo imetawaliwa na vijana wa mikoani nyie wazaramo kazi kucheza Ngoma na umbea
 
Kuzaliwa Mburahati, Mbagala, Tandale kwa mfuga mbwa, Buza, Gongo la Mboto n.k iwe ni jambo la kujivuna kuliko kuzaliwa Ilemela, Njiro au Iringa mjini??
Hawa jamaa ni wana fikra dunj sana.

Unakuta mtu kazaliwa Tandale kwa Tumbo huko, katika makuzi yake alikuwa analala chumba kimoja na dada zake, choo cha foleni wanashare na wapangaji wenzao kama 10, hasubui akiamka anakunywa chai na Visheti, shule yenyewe kasoma Kayumba mwanzo mwisho...

.... Halafu eti mtu huyo anakuja kujiona yeye ni bora na mjanja kuliko mimi ambaye nimezaliwa na kukulia Isamilo Mwanza, shule nimesoma Lake,likizo nilikuwa napelekwa na wazazi wangu serengeti national parks na katika makuzi yangu sijawahi kupanda daladala.

Yaani hawa jamaa kuzaliwa tu dar-slum kunawapa superiorty complex ya kipumbavu, na wakati wengi wao ni wajinga sana.
 
Hahahhahahha....

Umezaliwa wapi kwani? Nenda RITA wanakutengenezea kitambulisho unaweza kusema umezaliwa Amana...
Heri aende akabadilishe place of birth aseme amezaliwa hata Katavi, Inyonga kuliko kuonekana na yeye amekuzwa na chips na supu ya utumbo wa kuku huko buza.

kwanza kuna maboss ukiwaambia wewe ni mzaliwa wa dar hawawezi kushirikiana na wewe kwenye jambo lolote lile serious, maana inaaminika kwamba nyie wazaliwa wa dar ni makanya boya na vichwa vyenu havina la maana zaidi ya stori za akina Diamond na Zuchu pamoja na Simba/Yanga.
 
Wakenya waliozaliwa Nairobi huwa hawana huo muda mchafu na tambo za hovyo za Kiswahili.
Wakenya wanajivuniaga kumiliki pesa tu na kushika nguvu ya madaraka.

Zile tambo za sijui eti "mimi mtoto wa mjini" huo ujinga wameaachia wabongo hususani matoto ya dar ambao wengi hawana hela wamebaki kuwa machawa tu kwa matajiri waliotoka mikoani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…