Watu wengi wa Kanda ya Ziwa sio wastaarabu wakati wa kula, wanatia kinyaa!

Kanda ya ziwa yote ni shida
 
Wadigo nao kule Tanga wanakula kwenye Sinia moja especially wali au pilau hata watu wanne, wote wanakula kwa mikono baada ya kunawa halafu wanakaa chini kwenye jamvi.
Pamoja na kukaa na kusomea tanga tabia hiyo imenishinda kabisa.
Hawana uchafu kama ktk kula. Pwani yote watu hula pamoja ki asili lakini hakuna uchafu huu wa Kanda ya ziwa
 
Si ungeenda moja kwa moja kwamba ni wasukuma? Ukisema kanda ya ziwa ujue unahusisha Wajita, Wakurya, Wahangaza, Wahaya, Wakerewe, Wazanaki, Wasukuma....
Wote ni walewale ila hiyo sio kanda ya ziwa tu ni kote wanaokula kwa mkono
 
Hio Tabia ilinikera sana mwingine unakuta anashika ugali wote Kama mtu ananyonga sterling ya gari kukata Kona ugali wote unapakwa michuzi hadi kinyaa.
Mtu anaacha kula upande wake anafinya upande wako.
Hahaaaaa, nimecheka kama mazuri. Ni kweli kabisa jamaa wapo hivyo. Kuna mmoja nilisoma naye SUA. Hahaaa, yupo hivyo hivyo. Anakula huku anaongea na mavyakula yapo mdomoni. Anatafuta mzeeee, sauti za kutafuna nyamnyamnyam zinasikika kama guruwe bwana.
 
😂😂😂
 
Wadigo nao kule Tanga wanakula kwenye Sinia moja especially wali au pilau hata watu wanne, wote wanakula kwa mikono baada ya kunawa halafu wanakaa chini kwenye jamvi.
Pamoja na kukaa na kusomea tanga tabia hiyo imenishinda kabisa.
Mbona hiyo ni kawaida na wengi tumekuwa tukiwa hivyo. Huo ulikuwa mtindo mzuri wa maisha na ulikuwa unaleta umoja na amani na kutoa ubinafsi katika ngazi ya kaya na jamii kwa ujumla.

Huu ubinafsi na uchoyo wa sasa umeanza toka.ngazi ya familia tokana na aina ya ulaji wenu wa kisasa wa kujipakulia. Wengi wanajijazia wao bila kuangalia wengine tofauti na ule wa pamoja.

Pamoja na yote, ukanda wa pwani wana tabia manners nzuri tofauti na wasukuma.
 
Wengine watasema watu wote wanaolipa mahari si wastaarabu.

Na kukupa hoja nzuri tu kuonesha hata wewe mlipa mahari unaendeleza biashara ya watu na bado upo katika kundi la watu waliokosa ustaarabu.

Levels.
Upo nje ya mada Msukuma. Anasemea table Manner. Ni kweli wasukuma hamna table manners mnakula hovyo hovyo. Sijui bwana Maduhu Nyanda huko Marekani mnaishije na usukuma wako au nawe unakula hovyo hovyo maana unaweza kumtoa Msukuma usukumani ila huwezi kuutoa usukuma ndani yake.
 
Wasukuma hawapo wa aina moja.

David Kidaha Makwaia, Francis Nyalali, Paul Bomani, Andrew Shija, John Momose Cheyo, John Rubambe, Bob Makani, Marcel Komanya, Musobi Mageni, Balozi Nhigula just to name a few, hao wote ni Wasukuma, nimekula nyumbani kwao, the best meals with the best table manners. All types of cuisines.

Nyie mnakwenda kwa watu masikini huko halafu mnachafua Wasukuma wote kwa stereotype za watu masikini, ambao wote mnakula ugali wenye wanga mtupu usio na virutubisho, mkizungukwa na nzi wasiohesabika huko Tanzania.

Acheni stereotypes.

Wasukuma are more than seven million strong, na pia kuna kila aina ya Wakonongo wanaolowea Usukumani kina Magufuli hawa wanajiita Wasukuma, you can't possibly stereotype us and still be accurate.

Njoo kwetu Mwanza, Shinyanga, Mbezi Beach, Oysterbay, New York, New Jersey, DC Massassuchetts, London and all over the world nikuoneshe Wasukuma wanavyokula.

Acha ku steteotype watu kwa kutumia kigezo cha subset ya wenye umasikini na kukosa elimu.

Tukianza kwenda hivyo, ninaweza kusema wabongo mlio Tanzania bado mnakula mavi, ndiyo maana bado mnasumbuliwa na kipindupindu mpaka leo.
 
Muhaya atakuchanganyia maharage, dagaa, nyama, tembele, mlenda, tambi kwenye sahan moja hawa watu kula nao yataka moyo
Kwenye ulaji umewasingizia nadhani ndilo kabila linalozingatia table manners hasa ukanda huo, kama mnakula katika sinia moja ile kizamani ni hairuhusiwi kuongea ukiwa unakula, ukishiba unasogea nyuma, kuna ule mkao wa kuinama ukiinuka ni umeshiba, kila mmoja na bakuli lake hamna la kuchovya bakuli moja, ukikiuka hayo hapo juu kwenzi itakayokupata lazima usimulie hadi wajukuu
 
Mada ilianza vizuri ila ghafla imehamia kwenye ukabila.

Tukianza kutazamana kwa makabila la huyu zuri la huyu baya itakuaje?
 
Wasukuma wana katabia ka kunawa sehemu moja hata kama mpo 10+ haka katabia kananikera na kuniudhi sana, aliyenawa ni yule wa kwanza tu wanaofatia ni kunawa uchafu wa mwingine na mwingine mpk wa mwisho nae ananawa humo humo kisha wanaenda kula aiseeeee putuuuu,
 
Ujio wa hizi vijiti vya meno unakuta jitu zima linachokonoa meno in public au muuza chakula ana sevu huku kijiti cha meno kipo mdomoni Mimi hata hamu ya kula inakata kabisa.
Kiujumla usafi na table manners kwa chakula cha umma ni changamoto sana sehemu kubwa ya Tanzania kama unazingatia hayo mambo, ila raia wengi inaonekana hawajali wala kuzingatia sana hizo ishu.
Mifano ni mingi
1.Kuna sehemu mtu anakata nyama ya supu iliyoiva na mkono wa chooni huku mikono hiyo hiyo anapokelea nayo pesa.
2.Sehemu nyingi tu wana utaratibu wa kurudishia kwenye bakuli la maji machafu yaliyonawia jagi wanalotumia kunawashia watu halafu wanalitumbukiza tena kuchotea maji masafi ya kunawaishia watu.
3.Kuna sehemu watu hutumia maji machafu yaliyonawia baada ya kumaliza kula.
4.Kuna watu wanasukutua na kuoshea midomo yao na makohozi sehemu za kunawa ili watu wale.
5.Kuna watu hawewezi kununua mahindi ya kuchoma bila kuyashishika ndipo wachague
 
Tabia za watu masikini katika jamii tofauti zinatofautiana pia. Jamii za watu masikini za vijijini ukanda wa pwani wanaweza kuwa na ustaarabu mkubwa zaidi katika matumizi ya vyoo kuliko sehemu nyingi.
 
Tabia za watu masikini katika jamii tofauti zinatofautiana pia. Jamii za watu masikini za vijijini ukanda wa pwani wanaweza kuwa na ustaarabu mkubwa zaidi katika matumizi ya vyoo kuliko sehemu nyingi.
Nimeenda Nangurukulu nikakuta watu wanakunya pwani baharini.

Nimepita Muhoro mji unanuka mavi.

What are you talking about?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…