Watu wenye pesa/mafanikio wako very humble

Huyo jamaa yako ana ubishoo wa kizamani kinoma toka 97.Hata huku Iringa unapotea potea .
 
Habarini za wakati huu wakuu..

Nimegundua kwamba watu wengi (siyo wote) wenye pesa/mafanikio ya kweli wako very humble. Hadi naanzisha huu uzi, yapo matukio mengi yamethibitisha conclusion hii.

Jana jioni nilienda Morena Hotel Dodoma kujipumzisha. Nikiwa pale nikakutana na rafiki yangu niliyepotezana naye muda mrefu. Akaomba ani-join kwenye meza yangu. Alikuwa anakunywa maji makubwa. Tukawa tunastorisha, akaniambia kwa sasa yeye ni Mhandisi binafsi, aliacha kazi Serikalini akaamua ajiajiri.

Tukiwa tunaendelea na story, nikapigiwa simu na business partner wangu, akaja kutu-join. Kwanza partner alipofika tu alikuwa kaning'iniza funguo za gari kwenye lux, alipofika mezani akazitoa kiunoni akazianika mezani, sambamba na iphone zake mbili. Nikamtambulisha story zikaendelea.

Story zikiendelea, partner akapigiwa simu na client ambaye tunamdai, badala ya kwenda kuzungumzia pembeni au kwa sauti ya chini akawa anapayuka kwa kutaja hadi kiasi cha pesa tunachomdai akidhani kwamba kama ni kiasi kingi kwetu basi ni kingi kwa kila mtu. Sikushangaa kwasababu nimeshamzoea, yeye ni mtu flani hivi (wakubwa mmenielewa).

Baada ya muda kidogo Mhandisi akaagiza Hennessy VSOP Cognac ya 700ml. Akatuambia na sisi tuagize. Mimi nimeacha pombe, nikaagiza grand malt na coke. Nikamuona partner ana wasiwasi, uso wake umesawajika, ni kama alikuwa anajiuliza kuhusu bill. Akaagiza Heineken, akaletewa 6! Bill ikaja, Mhandisi akalipa, alikataa kabisa kushea au sisi kulipa. Taratibuuu, partner akachukua funguo za gari na simu mezani akaweka mfukoni [emoji28]..

Mhandisi akanywa Hennessy kidogo tu, ingine akabeba, akaomba tuhame pale, partner naye akabeba Heineken zake.

Ile tunafika parking, Mhandisi anasukuma Toyota Land Cruiser V8 VXR nadhani ni ya 2021 ile, partner ana Toyota Vanguard yake, akawa mpole sana. Msiulize mimi naendesha nini [emoji3]...

Mhandisi akaomba tumfate nyuma. Break ya kwanza Bambalaga. Aisee partner alilewa mpaka anauliza pale tuko wapi!

Tukaagana usiku wa saa saba, tukabadilishana contacts. Leo saa tatu asubuhi Mhandisi kanipigia, kuna mradi "X" amepata tender hapa Dodoma. Anataka tuwe Wanasheria wake, yaani tufanye 'retainership agreement', na anatulipa kwa mwaka mzima, leo hiihii amesha-deposit malipo yetu yote ya mwaka in millions. Partner amebaki mdomo wazi!

Mhandisi ni mpole sana. Anachagua maneno ya kuzungumza. Hana mbwembwe yeye ni vitendo tu.

Hii siyo scenario ya kwanza, ziko nyingi sana.

Kwahiyo ukiona mtu anajisifia sana, anaonesha possessions zake hadharani ili kila mtu ajue, ujue hamna kitu hapo. Anafanya hivi ili kujilinda. Kuna kitu najifunza hata whatsap status za matajiri ni tofauti sana na za masikini. Matajiri wengine huwa hawapost kabisa au wanapost mara mojamoja, na wakipost hawawezi kupost fitina au majungu.

Hata humu JF, wadau ambao wako vizuri sana huwezi kuwaona ni wajuaji. Hata namna wanavyo-comment au ku-post, ni tofauti sana na masikini na waigizaji wa maisha.

Maisha ni safari ndefu, naendelea kujifunza..
Yes again Yes. Kuna umasikini we akili ama maarifa ama emotional intelligence na Kuna umasikini we pesa na Mali.
Pia navyojua Mali ama mafanikio hayaendani na kujiinua kuonekana wewe Ni zaidi ya aliyekupa ama anayehakikisha wewe unapumua.
Yani Ni ngumu mno ukawa na pesa ya maana like mo, bill gate na ukawa na kiburi Ni ngumu. Huwa haviendani inabidi uwe humble ndio kanuni ya kuzidi kupata Mali. Yaani cheki matajiri wote hata Elon musk unapiga naye stori Kama kamshkaji fulani na ongea zao sio za kuji boast.

Mie nishafika sehemu nikaona kuwa yaani mafanikio na kuji proud havikai sehemu moja hata siku yaani narudia hakuna mwenye uwezo mkubwa mno akawa mwenye kiburi Ni wachache mno yaani rare case.
Hata appearance zao huwa Ni normal.
Since they don't feel Inadequacy, don't need any mattering,or validation from outside since they've already validated or fulfilled in their soul inside and not outside.
Real life is soul or spiritual searching ndio unapata mafanikio.
Mana imeandikwa nitafuteni mie na mie ama.mali Ni ziada tu
 
Habarini za wakati huu wakuu..

Nimegundua kwamba watu wengi (siyo wote) wenye pesa/mafanikio ya kweli wako very humble. Hadi naanzisha huu uzi, yapo matukio mengi yamethibitisha conclusion hii.

Jana jioni nilienda Morena Hotel Dodoma kujipumzisha. Nikiwa pale nikakutana na rafiki yangu niliyepotezana naye muda mrefu. Akaomba ani-join kwenye meza yangu. Alikuwa anakunywa maji makubwa. Tukawa tunastorisha, akaniambia kwa sasa yeye ni Mhandisi binafsi, aliacha kazi Serikalini akaamua ajiajiri.

Tukiwa tunaendelea na story, nikapigiwa simu na business partner wangu, akaja kutu-join. Kwanza partner alipofika tu alikuwa kaning'iniza funguo za gari kwenye lux, alipofika mezani akazitoa kiunoni akazianika mezani, sambamba na iphone zake mbili. Nikamtambulisha story zikaendelea.

Story zikiendelea, partner akapigiwa simu na client ambaye tunamdai, badala ya kwenda kuzungumzia pembeni au kwa sauti ya chini akawa anapayuka kwa kutaja hadi kiasi cha pesa tunachomdai akidhani kwamba kama ni kiasi kingi kwetu basi ni kingi kwa kila mtu. Sikushangaa kwasababu nimeshamzoea, yeye ni mtu flani hivi (wakubwa mmenielewa).

Baada ya muda kidogo Mhandisi akaagiza Hennessy VSOP Cognac ya 700ml. Akatuambia na sisi tuagize. Mimi nimeacha pombe, nikaagiza grand malt na coke. Nikamuona partner ana wasiwasi, uso wake umesawajika, ni kama alikuwa anajiuliza kuhusu bill. Akaagiza Heineken, akaletewa 6! Bill ikaja, Mhandisi akalipa, alikataa kabisa kushea au sisi kulipa. Taratibuuu, partner akachukua funguo za gari na simu mezani akaweka mfukoni [emoji28]..

Mhandisi akanywa Hennessy kidogo tu, ingine akabeba, akaomba tuhame pale, partner naye akabeba Heineken zake.

Ile tunafika parking, Mhandisi anasukuma Toyota Land Cruiser V8 VXR nadhani ni ya 2021 ile, partner ana Toyota Vanguard yake, akawa mpole sana. Msiulize mimi naendesha nini [emoji3]...

Mhandisi akaomba tumfate nyuma. Break ya kwanza Bambalaga. Aisee partner alilewa mpaka anauliza pale tuko wapi!

Tukaagana usiku wa saa saba, tukabadilishana contacts. Leo saa tatu asubuhi Mhandisi kanipigia, kuna mradi "X" amepata tender hapa Dodoma. Anataka tuwe Wanasheria wake, yaani tufanye 'retainership agreement', na anatulipa kwa mwaka mzima, leo hiihii amesha-deposit malipo yetu yote ya mwaka in millions. Partner amebaki mdomo wazi!

Mhandisi ni mpole sana. Anachagua maneno ya kuzungumza. Hana mbwembwe yeye ni vitendo tu.

Hii siyo scenario ya kwanza, ziko nyingi sana.

Kwahiyo ukiona mtu anajisifia sana, anaonesha possessions zake hadharani ili kila mtu ajue, ujue hamna kitu hapo. Anafanya hivi ili kujilinda. Kuna kitu najifunza hata whatsap status za matajiri ni tofauti sana na za masikini. Matajiri wengine huwa hawapost kabisa au wanapost mara mojamoja, na wakipost hawawezi kupost fitina au majungu.

Hata humu JF, wadau ambao wako vizuri sana huwezi kuwaona ni wajuaji. Hata namna wanavyo-comment au ku-post, ni tofauti sana na masikini na waigizaji wa maisha.

Maisha ni safari ndefu, naendelea kujifunza..
Hakika
 
Kwa ujumla watu masikini Wana kelele Sana.....
Hata baa za watu masikini zina makelele Sana ...

Kelele inaenda Sana na umasikini
Kelele inaenda Sana na kutosikia details...na watu wasiopenda details Wengi ndo masikini
Debe tupu huvuma zaidi. Bee don't bother to explain to flies how Honey is sweet than shiit.
Akipata tak00 hulia mbwata, n k
 
Mwenye hela huwa mpole na mwembamba wa wastani na muonekano wa afya njema.
Masikini huwa na maneno mengi sifa kwake hazishi, akikusaidia miaka 10 baadae atakumbusha msaada wake kwako. Pia afya zao huwa hafifu kula ovyo ovyo(kitambi kubwa)
Ukiwa tajiri wa hela kuwa tajiri wa afya pia.
Hii kweli kabisa mwaka jana nilikutana na mzee mmoja aliniambia ana 57 yrs nikabaki nashangaa jinsi alivyo mwenye afya, mwili wa wastani nachokumbuka alisema yeye huwa hatumii kilevi chochote na hali vyakula vya wanga ndio mafanikio ya afya yake.
Ni mstaarabu sijawai ona yeye mpaka familia yake, ni mmiliki wa makampuni makubwa hapa nchini.
Kilichonivutia kwake zaidi ni afya.
 
hivi mnataka funguo tueke wapi labda. tuwe tunaacha kwa walinzi ama?
coz funguo mara nyingi inakuja na holder na hizi za kisasa ni liplastic tu lenye ukubwa wake, then tunaambatanisha na funguo zetu muhimu in case umetoka na usafiri wako usisahau funguo hizo muhimu ulipotoka.
sasa funguo zote hizo mnataka tueke mfukoni acheni ushamba bwana kuning'iniza funguo ni jambo la kawaida.
hizo hoja zingine ntaafiki.
 
Back
Top Bottom