KERO Wauza viwanja na speaker mnazoweka barabarani mnasababisha kero au Noise pollution

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Na wale wanaotuamsha saa 10 usiku tuwaweke kundi lipi?
 
Kaka umeongea kwa msisitizo sana, sema nadhani utapeli umeanza tangu enzi za zamani maana hakuna jipya chini ya jua. Chamsingi ni mtu kuwa makini na kujifunza kutokana na makosa ya wengine.
Nachukia sana utapeli na niko makini sana Kuna wakati mwingine mtu simjui akinisimamisha barabarani nampuuza kama sijamuona ili kutokumpa nafasi ya kujieleza na utapeli wake

Kweli wizi haujaanza leo na utakuwepo sana tu, muhimu ni kuwa makini
 
Nachukia sana utapeli na niko makini sana Kuna wakati mwingine mtu simjui akinisimamisha barabarani nampuuza kama sijamuona ili kutokumpa nafasi ya kujieleza na utapeli wake

Kweli wizi haujaanza leo na utakuwepo sana tu, muhimu ni kuwa makini
Vyema sana
 
Nchi ngumu mno hii, basi tu. Hapo mbezi mwisho ni maturubai tu, hakuna utaarabu, yaani kuna mda hadi jam ya waenda kwa miguu. Ukishuka stendi ya malamba kuna jam kabisa kwenye ngazi...hizo kelele sasa!
 
Ukitapeliwa kiwanja, we mtafute tapeli umalizane naye ili asirudie tena. Tapeli hatapeli mtu mmoja
 
Ukitapeliwa kiwanja, we mtafute tapeli umalizane naye ili asirudie tena. Tapeli hatapeli mtu mmoja
Mara chache naona watu baada ya kutapeliwa wakimtafuta tapeli kumalizana naye. Sijui matapeli wanapotelea wapi
 
Hata sio wengi ndugu yangu. Kuna wajinga wachache tu wanaharibu hali ya hewa. Ki ukweli mimi nakereka sana
Nadhani hao wajinga ni wazee wa kuchangamkia fursa ya ni matapeli wazoefu wameona fursa wamepita nayo. Ila wana waharibia wale wenye uadilifu.
 
VIWANJA VIWANJA VIWANJA
KAMPUNI YA KILUVYA KIBAHA VIWANJA COMPANY LTD, INAKUTANGAZIA OFA YA VIWANJA VINAVYOPATIKANA KIBAHA NA KILUVYA

VIWANJA VYETU NI KUANZIA SH MILIONI MBILI NA KUENDELEA.....
PATA KIWANJA CHA UKUBWA WA 20/20 KWA MILIONI MBILI...

OFISI ZETU ZIPO MBEZI MWISHO MKABALA NA ..........
hawa jamaa mpaka nimewakalili sasa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hahahaa Mkuu umetisha sana.
 
Noise Pollution is everywhere in TZ hasa mijini, hujakutana na hawa wauza Tangawizi, Iliki na Mdalasini mitaa ya NMB Sokokuu Arusha

Hujakutana na wapiga Passport pale Moshi mjini na Arusha mitaa ya Stadium

Kuna wauza urembo mitaa ya Magombeni, soko la Mbagala na Kimara mpaka stand kuu ya Magufuli

Kuna hawa wauza madawa kwenye mabasi, dawa ambazo hata TFDA haizitambui na wauzaji sio Madaktari

Yaani ni kero tupu na serikali haikemei wala kutoa suluhisho la Hii Pollution labda hawajui ni tatizo
 
Lazma ukariri maana kila kona wapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…