Wazazi Mnaosomesha Watoto Shule za Private jifunzeni kufanya tathmini ya Pesa mnayowekeza katika Elimu hiyo na matokeo yake (Hawatazeekea Nyumbani)?

Wazazi Mnaosomesha Watoto Shule za Private jifunzeni kufanya tathmini ya Pesa mnayowekeza katika Elimu hiyo na matokeo yake (Hawatazeekea Nyumbani)?

Nyerere alisema elimu hamfanyi mtu asiwe masikini bali elimu humfanya mtu kujua namna ya kupambana na huo umasikini.
Kwahiyo hao wanaopeleka watoto Saint Kayumba wanawapeleka kufanya nini? Kama kuelimika ni English Medium basi Kuna wazazi wanauza vishata na sambusa ili watoto wasome kumbe wanaingizwa chaka (sikujua hili!)
 
Katika kila jamii, elimu hupewa nafasi ya kipekee kama nyenzo ya kufanikisha maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Wazazi huwekeza kwa gharama kubwa kuhakikisha watoto wao wanapata elimu bora, wakiamini kuwa elimu ni ufunguo wa maisha bora. Lakini swali la msingi linabaki: Je, uwekezaji huu unatoa faida inayolingana na gharama zinazotumika?

Katika makala hii, nitachambua gharama za kumsomesha mtoto hadi chuo kikuu, nikiilinganisha na hali halisi ya soko la ajira nchini Tanzania. Pia, nitatoa tafakari mbadala kuhusu thamani ya ardhi kama uwekezaji, pamoja na mbinu ambazo mzazi anaweza kutumia kupunguza gharama za elimu bila kuathiri ubora wa maarifa anayoyapata mtoto wake.

GHARAMA ZA KUMSOMESHA MTOTO: TAKWIMU ZINASEMAJE?

Wazazi wengi hujitoa kwa hali na mali kugharamia elimu ya watoto wao. Kwa mujibu wa makadirio yafuatayo, mzazi anayemsomesha mtoto mmoja kutoka darasa la kwanza hadi chuo kikuu anahitaji angalau:

1. Elimu ya Msingi (Darasa la 1 - 7):

Tsh 800,000 kwa mwaka x 7 miaka = Tsh 5,600,000

2. Elimu ya Sekondari (Kidato cha 1 - 4):

Tsh 1,200,000 kwa mwaka x 4 miaka = Tsh 4,800,000

3. Elimu ya Juu ya Sekondari (Kidato cha 5 - 6):

Tsh 1,200,000 kwa mwaka x 2 miaka = Tsh 2,400,000

4. Chuo Kikuu (Mwaka wa 1 - 3):

Tsh 2,500,000 kwa mwaka x 3 miaka = Tsh 7,500,000

Jumla ya gharama kwa mtoto mmoja inakuwa Tsh 20,300,000, na kwa watoto watatu inafikia Tsh 60,900,000.

Lakini je, mzazi anayefanya uwekezaji huu ana uhakika wa kupata faida kupitia ajira ya mtoto wake baada ya kuhitimu?

HALI YA SOKO LA AJIRA: UHALISIA ULIOPO

Kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), mwaka wa masomo wa 2023/2024 uliona ongezeko la udahili wa wanafunzi wa shahada ya kwanza kufikia 186,289 (Mwananchi).

Hata hivyo, soko la ajira haliwezi kuwahudumia wote. Takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonyesha kuwa kila mwaka nafasi za kazi mpya serikalini na sekta binafsi hazizidi 50,000. Kwa hesabu rahisi:

Wahitimu wa vyuo kwa mwaka:
186,289

Nafasi za ajira zilizopo: 50,000

Wahitimu wasiopata ajira mara moja: ~136,289

Uwezekano wa kupata ajira mara moja: ~27%

Kwa maneno mengine, asilimia 73 ya wahitimu wa vyuo vikuu hawapati ajira mara moja.

Hili linaibua swali muhimu: Je, mzazi aliyelipa ada kwa miaka 16-20 anaweza kupata mrejesho wa uwekezaji wake ndani ya muda mfupi?

UWEKEZAJI MBADALA: THAMANI YA ARDHI JIJINI DAR ES SALAAM

Hebu tuchukulie mfano wa mzazi aliyekuwa akitumia wastani wa Tsh 3,000,000 kwa mwaka kwa mtoto mmoja katika elimu tangu miaka ya 1990s. Kama angewekeza pesa hii kwenye kununua viwanja jijini Dar es Salaam, leo hii thamani yake ingekuwa ya mamilioni.

Kwa mfano, mnamo 1995, viwanja katika maeneo kama Tegeta vilikuwa vinauzwa kwa kati ya Tsh 500,000 – 2,000,000. Leo hii, kiwanja cha ukubwa wa 1,200m² katika Mbweni kinauzwa kwa Tsh 85,000,000 (Jiji.co.tz).

Kwa maneno mengine, mzazi aliyenunua kiwanja miaka ya 1990s kwa Tsh 2,000,000 leo anaweza kuwa na mali yenye thamani ya zaidi ya Tsh 200,000,000.

Hii inaonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mzazi kupata faida kubwa zaidi kwa kuwekeza katika ardhi badala ya kutegemea ajira za watoto wao kama njia ya kupata mrejesho wa gharama za elimu.

NJIA YA KUOKOA GHARAMA ZA ELIMU PASIPO KUPOTEZA UBORA

Je, kuna namna mzazi anaweza kumpa mtoto elimu bora kwa gharama nafuu?

Jibu ni ndiyo!

Njia mojawapo ni kumpeleka mtoto shule za serikali na kisha kuongeza maarifa kwa njia ya tuition.

Mfumo huu umefanikiwa katika nchi kama Kanada, ambako homeschooling na masomo ya ziada (tutoring) vimeongezeka kwa 36% kila mwaka, huku gharama ya elimu kwa mtoto mmoja ikiwa chini kwa 90% ukilinganisha na shule binafsi (Moe.go.tz).

Kwa hesabu rahisi, mzazi anaweza kutumia Tsh 120,000 kwa mwaka kwa tuition bora badala ya Tsh 1,200,000 kwa shule binafsi, hivyo kuokoa hadi Tsh 1,080,000 kwa mwaka kwa mtoto mmoja.

HITIMISHO: NI WAKATI WA KUHOJI UWEKEZAJI WETU KATIKA ELIMU

Hakuna anayepinga thamani ya elimu, lakini ni muhimu wazazi kuhoji kama njia wanazotumia kugharamia elimu zina manufaa makubwa kwa watoto na familia kwa ujumla.

Kwa kutumia shule za serikali pamoja na masomo ya ziada, mzazi anaweza kuokoa hadi 90% ya gharama za shule binafsi na kutumia fedha hizo kwa uwekezaji wa muda mrefu kama ardhi, biashara au hisa.

Uamuzi wa leo utaathiri maisha ya kesho. Je, ni busara kuwekeza zaidi ya Tsh 60,900,000 kwa watoto watatu bila uhakika wa faida, au ni heri kutumia kiasi hicho kwa uwekezaji wenye uhakika wa marejesho?

Tathmin ya gharama utakayolipa soba au gharama ya mtoto kupewa mimba, kuolewa pre matured na kuachika ni kubwa Mara elfu!

Shule inasaidia mambo mengi!
 
EM zina ziada:
- Mazingira mazuri ya kujifunzia
-walimu wanaowajibika
-Nidhamu ni kipaumbele Kwa shule karibu zote
-Wanafundisha elimu ya dini Kwa uhakika
-usafi wa vyoo uko vizuri
-lugha za ziada kama Kifaransa zinafundushwa
-Usalama wa mtoto angalau unazingatiwa

Sasa huwezi kupata hivi vyote bila kulipia
 
Akili yako inawaza kuajiriwa tu tena serikalini!

Umewahi kumuona mwarabu au mhindi ofisi za umma Tz? Unafikiri hawasomi? Wanasoma Kayumba?

1.2M kwa mwaka ni sawa na 100K kwa mwezi ambayo ni sawa na 25K kwa week.

Hiyo 25K/week ni sawa na local beer
10/week.

Mbona hamtuletei hizi analysis za fedha kwenye pombe na uzinzi au huko uwekezaji unalipa?
 
EM zina ziada:
- Mazingira mazuri ya kujifunzia
-walimu wanaowajibika
-Nidhamu ni kipaumbele Kwa shule karibu zote
-Wanafundisha elimu ya dini Kwa uhakika
-usafi wa vyoo uko vizuri
-lugha za ziada kama Kifaransa zinafundushwa
-Usalama wa mtoto angalau unazingatiwa

Sasa huwezi kupata hivi vyote bila kulipia
Kwani hao watoto ma genius waliosoma Manzese Primary na sasa ni Madaktari bingwa, engineers si walisoma shule zenye mazingira magumu lakini wamefika mbali bila hayo mazingira mazuri
 
Akili yako inawaza kuajiriwa tu tena serikalini!

Umewahi kumuona mwarabu au mhindi ofisi za umma Tz? Unafikiri hawasomi? Wanasoma Kayumba?

1.2M kwa mwaka ni sawa na 100K kwa mwezi ambayo ni sawa na 25K kwa week.

Hiyo 25K/week ni sawa na local beer
10/week.

Mbona hamtuletei hizi analysis za fedha kwenye pombe na uzinzi au huko uwekezaji unalipa?
Mleta mada anazungumzia watanzania wa kawaida wenye kipato cha kawaida wanao poteza pesa kwenye EM
 
Ingekuwa ni hivyo kina Mo Dewji na Mbowe wasingekuwa na haja ya kwenda kusoma vyuo vikuu vya nje ili hali ukwasi wanao wa kutosha.
Hao sio wenzako mkuu, Mo dewji tangu lini asomeshe mtoto afu ategemee mwanae awe kijakazi kwenye kampuni Fulani mjini hapa? Hao watu wanasomesha watoto ili waje kuendeleza Biashara za familia; unamwaga milioni 20 kwenye elimu ya mwanao wakati hata kiwanja cha kumrithisha huna , ili iwaje?
Cha ajabu anamaliza chuo na anakua na qualifications sawa na saint kayumba ambaye naye kafika chuo hivyo hivyo (kwenye vyeti hawajali kama mwanao kasoma Saint Theresia secondary bali wanajali GPA, hata mtoto wa Maimuna muuza vitumbua aliyesoma Msengelo sekondari hana tofauti na mwanao kwenye macho ya muajiri)
 
Mbona hamtuletei hizi analysis za fedha kwenye pombe na uzinzi au huko uwekezaji unalipa?
Vipaumbele mkuu, jifunze kutofautisha uwekezaji na starehe; starehe sio lazima iwe na mantiki ila uwekezaji wa elimu lazima uwe na mantiki
Hela inayochomwa kwenye uzinzi na pombe nitaipangiliaje katika maendeleo?
 
Waliosomesha kanumba ndo wana viwanja vingi compared na hawa waliosomesha private? Uhalisia hao hao wanaosomesha hizo shule za gharama pia ndo wana maeneo prime, kazi nzuri na biashara kubwa kubwa
Ndugu yangu, kwa akili za Sasa za mtanzania anayesomesha saint kayumba hana hela hata za kufanya uwekezaji wa aina hiyo
Nachoongelea hapa ni hawa ndugu zangu ambao wanajikamua ipasavyo mtoto asome EM mpaka mara nyingine wanapiga pasi ndefu maofisini ilimradi ada zilipwe...... Siongelei hao wenye pumzi za kusomesha watoto EM na kufanya uwekezaji at the same time
 
Hizo ni failure zako binafsi kama mzazi na sio mfumo wa elimu , yaani jukumu la mwanao asipate mimba au asitumie unga unaliachia shule? Kweli?

Una umri gani? Mimi nimesoma, na nisingesoma probably ningeoa nikiwa na miaka 20 hiyo, ila Sababu ya shule nimeoa nikiwa na miaka 31, very matured, ni shule pekee ndo imenihifadhi mpaka na miaka 31, ningeacha mapema ningeanza kuface challenges mapema sana na pengine nisingeziweza Kama ambavyo nimezianza na 30
 
Una umri gani? Mimi nimesoma, na nisingesoma probably ningeoa nikiwa na miaka 20 hiyo, ila Sababu ya shule nimeoa nikiwa na miaka 31, very matured, ni shule pekee ndo imenihifadhi mpaka na miaka 31, ningeacha mapema ningeanza kuface challenges mapema sana na pengine nisingeziweza Kama ambavyo nimezianza na 30
Umri wangu unafanana na wako, kwahiyo ungesoma saint kayumba ungekua umeoa ukiwa na miaka 20? Sijaelewa
 
Back
Top Bottom