Ndio maana biashara nyingi za waswahili hufa mwenyewe mwenye nazo akizeeka au kufaNani kasema shule ndo urithi? Binafsi binti yangu atasoma huko na miradi ataikuta ashindwe yeye!!! Kumpa mtoto elimu bora sio urithi ni wajibu wetu kama wazazi kumpatia hayo..... kama hela huna peleka kayumba” wewe unaamini hao wanaosomesha kayumba ndo watawapa urithi watoto wao? Ashindwe kumpa elimu bora atoe urithi!!! Anatoa wapi? Wengi wanaopiga hizi kelele kama zako kibunda hawana
Sababu ya midimamo.ya kijinga kama huu wako
Wafanyabiashara matajiri wakubwa wahidi na waarabu watoto wa akina Dewji na Mzee Bakheresa watoto wao wamewasimesha shule na vyuo bora vya binafsi vya kimataifa kwa mabilioni na kuwakabidhi biashara waendeshe wa.waswahili wanawaza kusonesha kayumba
Wazee wa watu akina Dewji na Mzee Bakheresa huwaoni tena wakiamka asubuhi kwenda kazini wameachia kila kitu watoto wao wasomi na wanapeleka mbali zaidi kuliko wazazi wao
Mswahili unakuta kikongwe kutwa kinahaha kuendesha biashara wakati ana watoto wakubwa kibao.
Mfanyabiashara mswahili anamnyima mtoto elimu nzuri halafu eti ooh mimi lengo langu nabana hela nimwachie biashara
Ataendeshaje wakati elimu ndogo kwenye ulimwengu wa sasa wa ushindani mkubwa wa kibiashara kimataifa? Kampuni itamfia mikononi mwake