Wazazi Mnaosomesha Watoto Shule za Private jifunzeni kufanya tathmini ya Pesa mnayowekeza katika Elimu hiyo na matokeo yake (Hawatazeekea Nyumbani)?

Maelezo meng ila umeandika pumba na utumbo

Kila mtu anafamilia yake na kila mtu anawatoto wake na kila mtu anauwezo wake kipesa so acha uswahili komaa na familia yako familia za wengne waachie wenye familia zao

Hii kampeni ya kupinga EM imekua kubwa sana na sioni ata cha maana mnachopinga au kuhoji
 
Hao wahindi na waarabu hawasomeshi watoto wao? Kwa taarifa yako hao matajiri unaowajua wanasomesha watoto wao kwenye shule bora za gharama. Mo Dewji kasoma IST na chuo Georgetown University. Unadhani kuitoa biashara ya milioni hadi ifike bilioni itawezekana kwa hiyo elimu duni unayotaka kuwapa wanao?
 
Nunua kiwanja hata Kisarawe au chanika huko, huyo mtoto hadi amalize chuo kiwanja hicho hicho ulichonunua hata milioni 2 utauza hata 20M
Una akili duni mno bro. Hujui kuna kitu kinaitwa inflation? Mpe mtoto elimu bora huenda akawa na mawazo makubwa zaidi kuliko hayo ya kwako ya kijima.
 

Elimu lazima iendane na uchumi wa mtu husika kama mzazi wa mtoto

Mo Dewji alisoma shule ya gharama na pia alirithi biashara kubwa. ( alipewa elimu inayoondena na
biashara za familia yao ili aweze kuziendesha),

hakupelekwa IST na Georgetown kwa ajili ya kuzunguka na bahasha kugombea ajira za watu.

Mimi nadhani mtu ambae anasomesha mtu shule kwa gharama hafu hajaweka mazingira
yatakayo endena na hiyo elimu ya mwanae huyo anazingua.
unakuta Kuna Mtu anauza zake tu Viazi mbatata Sokoni pamoja na bidhaa zingine ndogondogo
ila yuko katika Vikundi vya Vicoba kama Saba hivi anawasomesha Watoto wake Shule za
Gharama wakati Yeye bado amepanga na hana hata Uwanja na Kwao shida hazibanduki.
 
Kujifunza nn? Labda lugha ya kigeni kwa ufasaha, napo pana walakini.
Tusidanganyane.
 
Una akili duni mno bro. Hujui kuna kitu kinaitwa inflation? Mpe mtoto elimu bora huenda akawa na mawazo makubwa zaidi kuliko hayo ya kwako ya kijima.
Elimu Bora labda uwe na bajeti ya kumpeleka Feza au IST na sio hizi EM za kukaririshana ili kufaulu, pia Ushasema "huweza" , hivyo viwanja guaranteed; mwaga hizo pesa kwenye ardhi huku ukimpambania mwanao Saint Kayumba na tuition (tuition unaweza kuchukua Walimu hawahawa wa private) na ndani ya miaka 20 unakuwa na ubavu hata wa kumkabidhi mwanao cheki ya milioni 50 siku anaoa au kuolewa
Tatizo hapa naona ndugu zangu wala ishu sio elimu Bora bali uvivu na kutojiamini kwa mzazi kutake charge elimu ya mtoto wako
Aidha uchome 20 M afu mwisho wa siku azunguke na makaratasi kama kahaba kwenye ofisi za watu (tena akiwa anapishana na wenzake waliosoma Saint Kayumba ndani ya msululu huo huo ) au mpe double chance ya mafanikio kwa kuwekeza kwa kiasi kwenye elimu yake (narejea kwenye neno lako "huweza") wakati kiasi kingine kikiwa kimewekezwa guaranteed kabisa katika ardhi au uwekezeji mwingine wenye guarantee kubwa ya marejesho
 
Kama ada ya laki 8 inakushinda labda umwage mavi kupata hizo ardhi. Acha ku-justify umaskini wako ndugu. Elimu haina mbadala na kamwe haitakuwa na mbadala.
 
Ba
Badilisha headline ya uzi wako isomeke "JINSI YA KUFUGA POPOMA NA KUEPUKA KUPOTEZA PESA KWA KULIPA ADA YA KIJANA WAKO MZURI"
 
Yaani watu wana Vipaumbele vibovu sana, maofisini humu Kuna watu wanahangaika ada za mamilioni wakati hata hawajajenga
 
Kama ada ya laki 8 inakushinda labda umwage mavi kupata hizo ardhi. Acha ku-justify umaskini wako ndugu. Elimu haina mbadala na kamwe haitakuwa na mbadala.
Tatizo mna dharau sana, yaani waliosoma na kufanikiwa kupitia kayumba mnadhani sijui ni ushirikina
 
Tatizo mna dharau sana, yaani waliosoma na kufanikiwa kupitia kayumba mnadhani sijui ni ushirikina
Mimi nimesoma Kayumba mwanzo mwisho ila mzazi wangu hajawahi kuwa na akili za kipumbavu za kutaka nisisonge mbele kielimu ili nirithi vitu vyake. Kupitia elimu niliyopata hata mzazi anajivunia ninapomshauri kwenye shughuli zake. Na wala hajawahi kudai nimsaidie pesa ingawa huwa najiongeza na kumtumia. Ndugu maisha hayahitaji shortcut... vinginevyo utaendeleza tu generational poverty.
 
Generational poverty mnaidumisha kwa kushindwa kukombolewa kifikra na hili jinamizi litawatafuna vizazi na vizazi
Kumpa mwanao investment kubwa ambayo guarantee ya return (kuajirika) ni chini ya 50% ni sawasawa Simba icheze na lipuli afu uchore mkeka kwamba Lipuli atashinda 5 - 0
Yaani hiyo mwanao bila hata kulipa ada kubwa hivyo unaweza ukashangaa ukamtafutia kadi ya maktaba ya mkoa akiwa kayumba huko huko tena akafanya vizuri zaidi ya hata wale wa kayumba
 
Hii kampeni ya kupinga EM imekua kubwa sana na sioni ata cha maana mnachopinga au kuhoji
Hatupingi ila tuna tafakari, yaani wazazi wanashinda njaa maofisini ili mtoto asome "ei, bi, si, di" badala ya "a, be, che, de"
Yaani lugha akuletee mkoloni afu eti ufuge acid tumboni kwa kushinda njaa ili mtoto aweze kuizungumza vizuri even though ukikuwa unaweza kuhakikisha mtoto anaiongea vizuri bila hata kushinda njaa
 
Kama una uwezo wa kumsomesha mtoto EM msomeshe, Hizi excuses za kutaka kupunguza gharama kwa lengo la investments hazina tija.

Kwenye mizunguko yetu ya maisha kwa siku, wiki, mwezi, mwaka tumekuwa tukipoteza pesa nyingi kwenye Anasa, Saluni hasa wanawake, Sadaka nono kwa watumishi feki, Kununua gari tusizomudu kugharimikia, Michango ya harusi, n.k

Kabla ya kufikiria kuingilia Utulivu wa Elimu kwa mtoto, Anza kubadiri lifestyle yako utakuta unasave kiasi kikubwa yawezekana kuzidi hicho cha EM, mnachopigia kelele kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…