Wazee wa Betting mmeona mwenzenu Hanscana ameliwa Milioni 7.5?

Kuhusu bank kukopesha Kampuni za betting , bwana mdogo usifikiri kila biashara unaweza kukopa bank. Bank hairuhusu tu hata kutoa pesa kutoka kampuni ya kubetia , utadepsit lakini kutoa hawata kuruhusu , kila nchi ina sera zake za kifedha.
Betting kwako unaichukuliaje kwani?

Bajeti ya mwaka wa fedha ya 2024/2025 ilikupita?

Incase haukusoma basi iko hivi

Shilingi bilioni 17.42 zimeingia serikalini mwaka wa fedha 2024/25 kutoka sekta ya michezo ya kubahatisha.

Shilingi bilioni 29.89 zinatarajiwa kukusanywa mwaka wa fedha 2025/26.

Leseni 14,124 zinapangwa kutolewa (mpya 845 na kuhuishwa 13,279).

Kwa hiyo kusema hakuna benki itazikopesha kampuni za betting Huu ni upotoshaji.

Sekta inayolipa kodi ya mabilioni na kupewa leseni na serikali ni sekta halali ya biashara. Benki zinakopesha biashara halali zenye mtiririko wa mapato.
 

Hapa ndio unaposhindwa kuelewa.

Kwa lugha rahisi: Kampuni inasema “mtu mmoja tunaweza kumlipa mpaka 500M.”

Hiyo ni kwa mtu mmoja, si kwa jumla ya watu wote.

Kwa hiyo hata kama watu 1000 wakashinda 10M kila mmoja, hakuna anayezuiwa kwa sababu kila mmoja yupo ndani ya limit ya mtu mmoja.

Sijui hapo umeelewa?
 
We jamaa ni mgumu sana kuelewa tuliza akili soma kwa makini.
Nimesama hivi, haitotea siku ukafilisi kampuni ya kubeti kwasababu ya ushindi wako.
Kwanza sijasema mtu mmoja anaweza kufilisi kampuni. Kwa hiyo kujenga hoja kusema "haitatokea siku ukafilisi kampuni ya kubetia" inaonyesha wazi kunielewi.

Pili sio kila linaloitwa kampuni basi linakuwa na mtaji mkubwa ku handle population kubwa ya watu.

Tatu, Hata kama kampuni hazitangazi “tumefilisika,” kuna ushahidi wa malalamiko ya kuchelewesha malipo, kufuta mikeka, au kusitisha huduma ghafla.

Mfano: Malalamiko ya M-Bet yaliyosambaa mitandaoni – watu walishinda lakini wakazuiwa kulipwa kwa kisingizio cha “mfumo.” Hii ni dalili ya kampuni kushindwa kulipa kwa wakati inayosababishwa na kampuni kuyumba kiuchumi

Mtaji mdogo kwenye kampuni hutegemea zaidi loss za watu kuendesha kampuni.

Mfano Wasafi wana tuhuma nyingi za kufuta mikeka ya watu walio win pesa nyingi.
 
Kijana mfumo kusumbua ni kawaida, hivi unajua kuna limit ya miamala ya kiasi inachoweza kulipwa kwa siku unafahamu hilo?
 
Sasa kama wapo ndani ya limit watazuiwa vipi? Nimekwambia risk ya kampuni kupata hasara inazuiwa kwa mtu mmoja mmoja kwasababu haiwezekani kila mtu kushinda lakinI inawezekana mtu mmoja kushinda kiasi kikubwa
 
Hata kwenye stake tu kijana hunifikii. Umashawahi kuwa VIP player mpaka unapewa manager wakukusaidia mambo yako kwenye kampuni za kubeti? Au unabeti jero jero
View attachment 3530141
Nilikua nasoma huu mjadala wenu, hapa ulipokuja kuweka hizi screenshots ndio nikajua umedhamiria kuongopa.

Hizi sio bet halisi(real money), hizo ni demo account(virtual money). Nakupa mtihani rahisi, weka onyesha notifications ya deposits ya hizo pesa au withdraws.
 
Hao wenzenu matapeli wanakula na kampuni za betting hapo anapiga PR ili wapumbavu kama nyinyi muendelee kumtajirisha muhindi
Kampuni hiyo aliyobetia ni SPORTYBET, SPORTYBET hawana huo utaratibu. Huo utaratibu wanazo kampuni za kirusi
 
Hao wote wanatumia kampuni za kirusi sababu ni wakala wao. Wanapata commission kulingana na watu wanaojiunga na wanaovheza kwa kuweka promo code.

Hilo ndio tatizo kubwa la kampuni za kirusi. Hawawezi kufanya hicho wanachofanya kwenye kampuni Kama sportybet
 
Chatgpt inaongozwa na prompt

Ukiweka prompt zenye kuiongoza kuleta matokeo ya uongo basi utaletewa uongo na haiwezi kubeba lawama kama policy yake inavyosema.

Kwa mfano hapo iliposema hata ukishinda huwezi kulipwa. Huu ni uongo.

Mteja hawezi kuwa na kazi ya kusoma policy za kampuni ili ajue limitation yake ni ipi ili asizidishe na kujikuta bet imesuinda na halipwi.

Ila kampuni litachofanya ni ku set mfumo wa kutoruhusu mkeka kuingia kwenye system iwapo utakuwa na payout iliyopitiliza maximum ya kampuni kulipa mtu mmoja.

Hiyo ikiwa na maana kwamba, kama kampuni limitation kwa mkeka mmoja ni milioni 500 maana yake mifumo ya kampuni haitaruhusu single user kuweka mkeka mmoja wenye zaidi ya milioni 500.

So Chatgpt wako umemuelekeza kutoa majibu potofu kuwa system ya kampuni inaruhusu mkeka kupita halafu baada ya kushinda eti kampuni likagoma kukulipa hela yako. Huo ni uongo.
 
Hilo halihusiani na soccer inayochezwa hadharani. Hata hao wenye hizo kampuni na teknolojia hawajui Leo Barcelona atashinda ngapi. Wanachoweza labda ni kununua mechi kitu ambacho hakiwezekani kwenye ligi kubwa na timu kubwa.

Hakuna sayansi Wala uchambuzi wowote ambao utakuambia leo Barcelona anashinda ngapi.
 
  1. Kama kampuni ndogo ikishindwa kulipa
    • Inaweza kuchelewesha malipo,
    • Kufunga akaunti,
    • Au kufilisika (rare, lakini hutokea kwa kampuni zisizo na leseni imara)
Hapa jamaa yako pamoja na kwamba ulimuongoza akupe majibu yale yanayoendana na fikra zako lakini amekuja kukukataa kwenye hiki kipengele ulichodai kampuni haliwezi kufikisika
 
Acha upotoshaji. Ukiona mkeka wako umefutwa ujue kuna fraud umefanya , na hii hushughulikiwa kwenye risk management. Unaweza kuokota fixed game ukaiweka kwenye mkeka wako unadhani utalipwa? Ticket inafutwa na unaweza kufutiwa account . Halafu wasafi bet suo kampuni ndogo nimiongoni mwa kampuni 10 zenye mtaji mkubwa afrika mashariki. Kampuni hii inamilikiwa na matajirI wa Belarus ambao wanamiliki pia Oddbet kenya ambapo walifanya partnership na diamond kuingia kwenye market ya Tanzania
 
Tutajie kampuni iliyofilisika kwa ushindi wa wateja mkuu
Hapa jamaa yako pamoja na kwamba ulimuongoza akupe majibu yale yanayoendana na fikra zako lakini amekuja kukukataa kwenye hiki kipengele ulichodai kampuni haliwezi kufikisika
 
Hata kwenye stake tu kijana hunifikii. Umashawahi kuwa VIP player mpaka unapewa manager wakukusaidia mambo yako kwenye kampuni za kubeti? Au unabeti jero jero
View attachment 3530141
Hata kwenye lost pia naweza nisikufikie.

Lakini kama ulikuwa point yako ni kuonyesha umaridadi wako wa ku stake high bado hii haikupi credit moja kwa moja.

Kuna mikeka mingi iko viral inazagaa mitandaoni watu wana share stake zao.

So hii haithibitishi kuwa huyo ni wewe inathibitisha tu kuwa kuna screenshot umeweka.

Hususan pale nikipima judgment zako za kuona mechi 50 kama kipimo cha odds nyingi hiyo inanipa mashaka kuwa hizi slip haziwezi kua zako.
 
Wewe unaweka uongo. Zipo kampuni watu hushinda lakini hufutiwa bets zao, n pia zingine hugoma watu kutoa pesa, Wala sio sababu ya fixed games. Kampuni za kirusi zinaongoza kuwa na hii tabia ya kuzuia watu kutoa pesa. Wasafi pia wana hii tabia
 
Tutajie kampuni iliyofilisika kwa ushindi wa wateja mkuu
Nadhani hapa nikirudishe kwenye Chatgpt yako

Kuna sehemu imeunga mkonk hoja yangu kuhusu kampuni kufilisika.

Au ulikopi bila kusoma Mkuu?
 
Asikuongopee hizo alizoshare ni demo account. Hakuna real money hapo. Mwambie aonyeshe notification kwenye hiyo app

Kampuni za kirusi ndio huwa na hii tabia. Huwezi kukugta huo ujinga sportybet
 
Nadhani hapa nikirudishe kwenye Chatgpt yako

Kuna sehemu imeunga mkonk hoja yangu kuhusu kampuni kufilisika.

Au ulikopi bila kusoma Mkuu?
Nimekupa mtazamo wa chatgpt , kampuni itafiliska kwa mambo mengine lakini sio kwasababu wateja wameshinda kwasababu kiwango cha ushindi kina limit , hamuwezi kushinda zaidi ya mtaji wa kampuni. Na kampuni zinatofautiana kwenye limit , nyingi hauwezi kushinda zaid ya milion 500 , nikakupa mfano kampuni 1 tajiri duniani kwenye betting unaweza kushinda hadi trilion 1000 ila timu hazitakiwi kuwa zaidi ya 50 na siku ukishinda utalipwa pesa yako na utaona Kampuni ikiendelea na watafurahia ushindi wako kwasababu utawatangaza zaidi. Na kuna uwezekano ukawarudishia sehemu ya hiyo pesa kwa kupoteza kama ukiendelea kubeti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…