Kampuni ya betting haipend haiwezi kusababisha hata mara moja wewe ulost kwasababu hata wenyewe hawajui matokeo yatatokaje. Lakini anajua hata iweje lazima faida iende upande wake . Leo ukipata milion moja kuna uwezekano ukaja kuirudisha yote au kurudisha hata mara 5 ya hiyo pesa. Mhindi anataka ushinde ili akupige vizuri , mtu aliyewahi kushinda pesa kubwa ni rahisi kuja kupigwa kuliko ambaye hajawahi kushinda. Na hata ukishinda wewe kuna maelfu watapoteza. Mimi nimewahi kushinda milion 4 ila nilikuja kupoteza over 15M + ile milion nne yao , imagine yeye kazi yake kununua platform na kuweka mtaji , wewe unaweka pesa na bado uchague timu ambazo zitashinda na tena ukikosea hata moja kwenye timu 20 bado anakugonga. Kwa ufupi betting ina faida kwa mmiliki sisi wengine tunajifurahisha huku tunaumia