DOKEZO Waziri aagiza mabasi 60, Kampuni ya Esther

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Unataka evidence gani? Huyu ameeleza anachokifahamu na ameomba chombo husika kufuatilia.
Elete ushahidi wewe mahakama?
 
Mwigulu kama anaiba mjue tu kawekwa hapo kwa maslahi ya wakubwa.

Ukimuona chura juu ya mti ujue kawekwa
 
Kwa hiyo umenuna mtu kujinunulia magari?Hebu acha akili za kimasikini mkuu!Au haupendi tukalione ziwa Singidani?😂😂😂
Hajanuna ili tunauliza pesa kapata wapi ndio swali la msingi,huko nyuma huyu Mr tozo hakuwa na ukwasi namna hii sasa inabidi tuingiwe na wasiwasi kuwa hizi bila shaka ni tozo zetu,jamaa sio mfanyabiashara na hata kwenye sheria za maadili sidhani kama aliandika ana mali hizo wakati akiwa amepata uwaziri, pia usisahahu jamaa na kilabu ya mpira huko nyuma alikuwa hana jeuri hata ya kuandika mabango akaishia kuandika kwenye mawe!
 
Sasa hao Tiss kazi yao ni ipi maana ufisadi kila mwaka wa fedha CAG anapokagua ni majanga matupu.

Yaani hawana uwezo wa kuzuia rushwa na ufisadi hadi CAG abaini madudu?

Kuna watu mtaani ni matajiri wa kutupwa na ni watumishi wa umma ambao hawana biashara rasmi zinazotambulika lakini wanakula maisha kama nchi haina waangalizi wa rasilimali za umma.
 
Taarifa ya CAG huwa haisemi moja kwa moja kwamba mtu au TaaSisi X ni mafisadi kwa sababu sio kazi Yao..

Wao wanapima.value for money na matumizi ya pesa kwa mujibu wa sheria za umma..

Ndio maana Huwa ni hoja za mkaguzi wanapewa mda kuzijibu,wakileta vielelezo zinafutwa wakishindwa kuna kurudisha pesa au kwenda mahakamani..
 
Haya na wewe lete ushahidi wa mikataba ya mikopo ya mtuhumiwa.
 
Hapo kwenye kwenda mahakamani maana yake wameshindwa kuonesha uwazi wa matumizi husika. Kwa maana hiyo CAG anakuwa sahihi.

Je, muda huo hadi CAG anabaini madudu yote hayo Tiss wanakuwa wapi?

Kila mara tunaona ubadhirifu wa fedha za umma baada ya ukaguzi wa CAG hadi kufikia Rais kuchukizwa na kuwatimua kazi waliotajwa kwenye ripoti ya ukaguzi.

Rais hadi anafikia kumtumbua mtu maana yake ni kweli ubadhirifu umefanyika. Sasa kazi yao ni ipi haswa?
 
Mfano mzuri bandarini kuna ufisadi wa kutisha kila mwaka na wahusika hubainika baada ya ripoti ya ukaguzi wa CAG.

Pale bandari kuna Tiss, Polisi na wana usalama wengine wengi lakini bado hawabaini ubadhirifu hadi CAG afanye ukaguzi ndo unaona madudu yanavyofumuliwa.
 
Sio kazi ya Tiss kusimamia miradi na taarifa ya CAG ni complex ukitaka Tiss wafanye hiyo Kazi sijui kama Wana manpower za kutosha kuwepo kila sehemu kufanya uchunguzi sio tuu wa pesa bali wa quality ya miradi,hii ni ngumu Bora hata ungeuliza Takukuru maana wao ndio Wana jukumu la moja kwa moja..
 
Tiss sio Malaika au majini bali ni watu kama wewe na Wana mahitaji ya pesa pia.
 
Sijapinga maendeleo yaliyofanyika bali kujali maendeleo ya upande mmoja pekee,
Baba ako ana ela anajenga majumba kila mahali, magari kila aina shule anakusomesha ya kata, hajali mavazi yenu familia kila akiombwa ela anadai anajenga kwanza, miaka 6 bila kuongezewa mshahara wakati vitu vinapanda bei kila uchwao?
Ndio maana mliona watu wanalia vyuma vimekaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…