Inasemwa kuwa mzee alikusanya fedha nyingi zilizotokana na njia zote tuzijuazo na hazina ilituna sana.
Hizi ni fedha zote za ndani (kodi na ushuru), za wafadhili wa nje, ADB, WB na vyanzo vingine ambavyo bado viliendelea kuleta fedha za maendeleo
Yadaiwa kuwa baada ya mzee baba kuaga dunia hii tambarabovu, watu waliingia hazina na kila sehemu nyeti kuhakikisha wanachukua fedha zote.
Hadi leo mtindo huo ( wa kuiba fedha hazina) na sehemu zingine umeachwa uendelee na hakuna anaejali kwani kila mtu yupo "high-high" kukusanya kilicho chake.
Hivyo yanotokea leo hakuna haja ya kujifanya twashangaa sana.
Wanasiasa si watatuzi na wakombozi wa shida zozote zile kwa wananchi bali ni binadamu kama wewe na mimi hivyo nao wana matamanio ya kuwa watu katika watu, matamanio ya kuwa matajiri na wenye fedha na pia matamanio ya kuishi maisha mazuri.
Wanasiasa kwa asili si viongozi wazuri isipokuwa kama upeo wao ni wajuu sasa ndipo wataishia kuwa viongozi maarufu lakini bila kutatua shida za wanaowaongoza, na hufanya machache sana makubwa. Hayati Mwalimu Nyerere pamoja na makubwa mchache aloyafanya ametuwezesha watanzania wote kuzungumza kiswahili kama lugha yetu ya taifa.
Ndo maana siasa ni fani ambayo mtu yoyote aweza kuingia awe profesa, mwalimu, mchungaji na kadhalika lakini hawaji kuwa viongozi ili kutatua shida za wananchi wanowachagua, bali waja kujitatulia matatizo yao kwanza, ndio maana ya kuambiwa wahakikishe "kila mtu ala kwa urefu wa kamba yake".
Kwa kuwa hawa tunowaita viongozi wana ajenda zao za siri ni rahisi kuona wanashindwa kukusanya kozi ipasanyo kwa kushirikiana na wafanyabiashara, kuwabinya wananchi wa chini kwa kuwabambikizia tozo za kila aina, kushindwa kusimamia uchumi wa nchi ipasanyo, kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, kushindwa kutagtua tatizo la ajira kwa kubuni njia za kuwawezesha wananchi kujiendesha kimaisha kwa biashara zinowafaidia wao, na kushindwa kubuni mikakati ya kuwanyanyua wananchi kiuchumi.
Serikali yoyote inoshindwa kukusanya kodi ipasanyo nikimaanisha kodi ya maendeleo na kodi ya viwanja, ukiachilia mbali mapato ya halmashauri na tozo zinojulikana kama uingizaji magari nchini, hiyo si serikali bali ni genge la wapigaji.
Si kila ajiitae mwanasiasa ni kiongozi na si kila anekuwa kiongozi ni lazima awe mwanasiasa.