Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
"The way forward" ni mapekendekezo ya Rasimu mpya ya katiba yalowasilishwa na jaji Warioba yatakiwa kufanyiwa kazi.Daaah inatosha sasa! 😱😥
Ebu tutafute the way forward!
Tuache ukimya tuiokoe Tanzania
Kisha watanzania kuamua wataka raisi wa aina gani mtu ambae kweli atafanya yale ambayo hayati Magufuli aliyafanya lakini bila kuonea watu (kama kweli alifanya hivyo) , kuhakikisha watu waovu hawamchonganishi na wananchi (maana hawa watu waovu na wahuni ni wengi) na atafuata misingi ya katiba mpya ambayo itakuwa imepigiwa kura ya maoni na wananchi na kupitishwa rasmi kuwa katiba mpya ya Tanzania.
Katiba mpya ndo itakuwa msingi wa demokrasia yetu, itawezesha chaguzi huru, viongozi kuwajibika na kuwajibishwa na pia raia na viongozi wote katika sehemu yoyoite kuheshimu misingi ya katiba hiyo.
Misingi ya katiba italinda raia na kuhakikisha haki yao ya msingi kama huduma za barabara, maji safi na uhuru wa kujifanyi shughuli halali zinoingiza kipato halali bila kubinywa na tozo za ajabuajabu zote zinatolewa. Misingi ya katiba itahakikisha TRA wanafanya kazi inavyopaswa na hawawaonei wafanyabiashara wadogo bali wanafuata misingi ya ukusanyaji kodi.
Zambia, Malawi, ni mifano tosha ya chaguzi bora ambazo zimeleta viongozi wenye nia angalau ya kuboresha maisha ya wananchi wa kipato cha kawaida. Tunisia ni moja ya nchi za kiafrika ambayo juzujuzi wamepiga kura ya maoni na wananchi wameiridhia.
Bila hivyo wananchi wataendelea kulalama kila siku lakini hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya msingi na badala yake wapigaji wataendeleza mambo yao ya kuwaachia wafanyabishara wajikusanyie faida kubwa bila kulipa kodi, waingizaji madawa ya kulevya kuendelea na kazi zao, wageni kushikilia mtaji wa soko na kuzuia soko la ndani kukua kwa kusingizia wao ni NGOs.
Ndo maana walikuwa wakilalamika kwamba hayati JPM aliwazuia walokiita access kwa local market ambayo kiukweli JPM alielewa kuwa wao ndio walikuwa walifanya kitu kiloitwa "capital flight".
Kwenye uchumi hii "capital flight" ni uondoaji wa fedha kwenye mzunguko na kwenye mabenki kwa makusudi unofanywa na wafanyabiashara na makampuni baada ya serikali kuanza kubana mianya mbalimbali ya ukwepaji kodi na kusababisha fedha kukosekana baada ya serikali mpya kuingia madarakani na kuweka sheria mbalimbali na kubadili sera mbalimbali za kiuchumi.
Kwa kuwa wananchi wengi walikuwa hawaelewi kinoendelea kiukweli raisi aliepita JPM alipata shida ingawa aliweza kuifanya nchi ijiendeshe hadi kufikia uchumi wa kati ambao ulitanganzwa na haohao wawezeshaji IMF na Benki ya Dunia. nchiu ikapita kwenye janga la ugonjwa wa uviko-19 bila shida sana, mazao yakazalishwa kwa wananchi kuhimizwa kulima na wale wadogowadogo (wamachinga wakahasishwa kufanya biashara kwa kusajiliwa ili iwe rahisi kuwatoza kodi
Leo hii JPM hayupo mambo yote yaso na maana ambayo yalipotea kwa miaka mitano yamerudi kuwa ni yaleyale ingawa yafanywa kichinichini yaani "low profile".
Watanzania wapaswa kuukataa mwenendo huu na kulazimisha utekelezwaji wa kuishughulikia rasimu ya katiba mopya kama ilivyopendekezwa na mheshimiwa jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba.