Waziri anayemiliki jumba la kifahari ufukweni Dubai atajwa

Waziri anayemiliki jumba la kifahari ufukweni Dubai atajwa

Leo katika Gazeti la Raia Mwema kuna taarifa za Waziri anaemiliki Jumba Ufukweli mwa Dubai tena akiwa amelinunua CASH kwa mabilioni ya shilingi.

Cha ajabu mpaka sasa vyombo vyetu husika havijafanya uchunguzi wowote kwa kumhoji ili ijulikane fedha hizi alikwiba wapi na hatua stahiliki. Hii inaonyesha wizi ni kama umehalalishwa ktk kipindi hiki.

View attachment 2881294
Gazeti limemtaja Leo wewe kelele mchana huu ,unadhani uchunguzi ni kama kukaanga chips

USSR

Sent from my Infinix X6511G using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo siku mkija kuambiwa aliyetajwa kumiliki Jumba huko Dubai ni Ndugu Wazir Mohamed Junaid Al Mazrui mfanyabishara wa Magari na vifaa vya ujenzi ambaye pia anamiliki vituo vya mafuta nchi Zambia na Msumbiji mtse,a kumbe wakimaanisha jina na sio cheo.
 
Naona kuna Subliminal message hapo kuwa Kigwa lakini Kigwa si alishafanyiwa Matumbuzi.
 
watanzania walivyo wambee kila sehemu mtajeee akitaja unataka akupangishe weweeee

pambaneni na halizenu mwenzeny kawekeza nyie mnapishana guest za bk 7 sinza shenzitype
 
Huenda urefu wa kamba yake unamruhusu kujipimia hekalu hapo Dubai, na labda ikawa hivyo ni vijisenti tu........nchi inatafunwa sana ndugu zanguni ni kama haina mwenyewe, suluhisho ni nini ili tuweze kusaidia nchi na wananchi?​
 
Haya magazeti na Kigwa wote lao moja, Kigwa anafanya hivyo kwa lengo la kutafuta teuzi, wakati hayo magazeti yanafanya hivyo ili yapate wateja.

Kama jina la waziri mnalo, nyumba anayomiliki ni yake, na ushahidi mnao, kipi kinachowatisha kumtaja huyo waziri?

Wajanja wanatuchezea kiakili ili kuyafikia malengo yao, huku wanajiita whistleblowers!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Rais wetu mpendwa aliruhusu kula kwa urefu wa kamba yako acha wenye nafasi waoneshe urefu wa kamba zao.
 
Hakuna Ushamba uliopitiliza kama kununua nyumba nje ili tu kutakatisha pesa ….mwisho wa siku na Tamaaa tu hutaweza kuifaidi kwani hata huo uwaziri ukiisha utabaki hapa na hutaweza kumudu hizo gharama ..na zaidi kuitunza hiyo nyumba ni gharama na sana ukipeleka watoto wako wataifanya kichaka cha kuvutia madawa ya kulevya , tuwe na Kiasi wandugu.

Una ziada Fanya kitu nyumbani kitasaidia kaka na dada zako watanzania
 
Leo katika Gazeti la Raia Mwema kuna taarifa za Waziri anaemiliki Jumba Ufukweli mwa Dubai tena akiwa amelinunua CASH kwa mabilioni ya shilingi.

Cha ajabu mpaka sasa vyombo vyetu husika havijafanya uchunguzi wowote kwa kumhoji ili ijulikane fedha hizi alikwiba wapi na hatua stahiliki. Hii inaonyesha wizi ni kama umehalalishwa ktk kipindi hiki.

View attachment 2881294
Majawabu anayo Mh. Hamisi Kigwa..
 
Back
Top Bottom