Waziri Gwajima afafanua dawa ya asili ya Corona (NIMRCAF), waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

Waziri Gwajima afafanua dawa ya asili ya Corona (NIMRCAF), waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

Usiwe na mawazo mgando na mtumwa wa historia vitu vipya vinagunduluwa kila siku hiki swali lako la kibwege na linaonyesha una uwezo mdogo mno wa kiakili ulio below sea level.Kwa hiyo ugunduzi mpya hauruhusiwi kuwepo duniani? Tanzania kuna baadhi ya watu wajinga ukiweo wewe ni wajinga hasa hadi wanakera
Kachumbari nao ni ugunduzi?😂😂😂.

Kabla ya corona kuja watu walikua wanakula hiyo kachumbali kila kukicha, basi wasingeugua maana tayari walikua na kinga kwenye miili yao.

Jibu swali, kachumbari ni tiba ya magonjwa?
 
Sometime mtu Bora ukae kimya kuliko kuonesha ujinga hadharani..
Saa toka lini malimao tangawizi ni ushirikina??? Kuongoza nchi yenye wajinga wengi ni kazi Sana..
Pole Mr President kwa kuwa na watu ka Hawa.
Kwa akili yako "kubwa", watu wameanza kula malimao leo baada ya corona?

Kwani kabla ya korona watu walikua hawali malimao? Ilikuaje watu wakapata corona huku tayari wana kinga ya malimao kwenye miili yao?

Watu na akili zetu tunakuna kuambiwa malimao, tangawizi, sijui kachumbari inatibu corona, mnataka tukubali?

Tulieni dawa iwaingia cumamae zenu.
 
Maswali mengine au tuseme ubishi mwingine unashagaza sana - hivi unafikiri kwa nini watoto, vijana na baadhi ya watu wazima hawasumbuliwi na KOVID? Labda tuanzie hapo - ukipata jibu rudi hapa utu - update.
Hata huelewi unachoandika hapa, halafu unategemea uelewe nilichouliza mimi?
 
Wewe ni daktari? Maana umeshupalia utafiti as if ukipewa hizo tafiti utaelewa kilichoko kwenye tafiti.
Ndio.
Wewe unadhani nami ni kilaza kama wewe na huyo YEHODA mnaozungumzia mambo msiyoyajua kabisa kana kwamba mnajua lolote?
Weka hapa maandishi ya huo utafiti halafu ndipo uhoji kama sijui kuudadavua.
ukipewa hizo tafiti utaelewa kilichoko kwenye tafiti.
Weka maandishi ya hizo tafiti kabla ya kuhitimisha kama ninao uwezo wa kuzidadavua na kuzielewa au la.
 
Nauza vitumbua vya moto kutoka China na mikoani natuma
Karibuni
 
Nchi imegeuka kua ya kishirikina, inchi ya wapiga ramli.

Toka lini kachumbari/chachandu ikawa tiba ya magonjwa?

Tufute wizara ya afya maana haina uhumimu, tutumie waganga wa kienyeji na wapiga ramli.
Madhara ya kufanya mambo kwa kutaka kumfurahisa mtu mmoja yaani anaweza kuwanywesha hata mkojo wa punda ili mradi wajione wapo kwenye msimamo mmoja na bwana wao.
 
Waziri wa Afya Dk Gwajima azindua dawa ya Asili ya Corona waweza itengeneza mwenyewe nyumbani

MCHANGANIKO WA DAWA LISHE NA MITI DAWA KWA AJILI YA TIBA YA KORONA

Namna ya kuandaa DAWA LISHE

Mahitaji:
1 Tangawizi ya urefu wa
kidolegumba chako vipande 5
2 Kitunguu swaumu punje 10
3 Pilipili kichaa 4
4 Kitunguu maji chekundu kikubwa1
5 Limao 2
6 Maji ya moto Lita 1

Uandaaji:
1. Osha dawa lishe zote,
2. katakata vipande vidogo vidogo,
3. Ondoa mbegu za limao,
4. Saga mchanganyiko wote kwenye Brenda. (kama huna Brenda au twanga kabla ya kuweka maji moto)
5.Chuja na chujio
6.Hifadhi katika chombo safi kama chupa safi

Kunywa mililita 20 sawa na vijiko vikubwa vya chakula viwili (2) kila baada ya masaa 8.

Kwa ambao tayari ni wagonjwa kunywa hadi utakapo pona

Kwa ambao sio wagonjwa unaweza kutumia kiasi hicho
mara moja au mbili kwa siku kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.

=====

WAGANGA WAKUU IMARISHENI MIFUMO YA UDHIBITI NA KINGA YA MAGONJWA: Dkt. GWAJIMA

*Wizara haina mpango wa kupokea chanjo ya COVID-19

Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma

Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya,Wafawidhi na Maafisa Afya Mazingira nchini wametakiwa kuendelea kuimarisha mifumo yote ya udhibiti na kinga ya magonjwa kwa kushirikiana na wananchi ili kudhibiti magonjwa yote ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati akitoa ufafanuzi juu ya maswali ya wanahabari kuhusu kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ambukiza kwenye ukumbi wa wizara jijini Dodoma.

Dkt. Gwajima amesema viongozi hao wanatakiwa kuwakumbusha wananchi kwenye elimu ambayo Wizara imekuwa ikiitoa ikiwemo kuimarisha usafi, kujifukiza, kufanya mazoezi, kula lishe bora, kunywa maji mengi bila kusahau matumizi ya tiba asili ambazo taifa hili limejaaliwa.

“Serikali itaendelea kuchukua tahadhari zote za ufuatiliaji wa mwenendo wa magonjwa yote kama ambavyo imekuwa ikifanya siku zote na kuendelea kuelimisha wananchi juu ya hatua za kuchukua”. Alisisitiza Dkt. Gwajima.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema Wizara yake haina mpango wa kupokea Chanjo ya COVID-19 inayoripotiwa kuwepo na kutumika kwenye mataifa mengine kwani Serikali kupitia wizara ya afya inazo taratibu zake za kufuata pale inapotokea kupokea bidhaa yeyote ya afya na hufanyika baada ya Serikali kujiridhisha na sio vinginevyo.

Kwa upande wa Tiba Asili Dkt. Gwajima amesema Wizara kwa kushirikiana na Mkemia Mkuu wa Serikali , Baraza la Tiba Asili na wananchi wajuzi wa tiba asili tayari wameshafanya usajili wa bidhaa (dawa) za tiba asili, alizitaja miongoni mwa dawa hizo ni COVIDAL,NIMECAF,PLANET++,BINGWA na COVOTANXA.

Aliongeza bidhaa za mafuta tete ambayo imehakikiwa na Mkemia Mkuu kuwa ni salama na zinatumiwa na watu mbalimbali ni Uzima Herbal Drops, BUPIJI, EUCALYPTUS OIL, LEMONGRASS ESSENTIAL OIL na bidhaa zingine zitaendelea kutajwa na Baraza la Tiba Asili

“Uko ushahidi wa kutosha kabisa kuhusu watu wengi ambao wamepata nafuu na kupona magonjwa mbalimbali ya kuambukiza na yasiyo ambukiza yaliyokuwa yanawasumbua mara baada ya kutumia dawa za tiba asili hata kama walikuwa kwenye matibabu mengine ya dawa za hospitali”.Alisema Dkt. Gwajima.

Hata hivyo Waziri huyo alilielekeza Baraza la Tiba Asili/Mbadala kutoa orodha ya dawa zote ambazo zimepita kwenye utaratibu wa kufanya uchunguzi wa kimaabara ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kuonekana kuwa matokeo ya awali ya uchunguzi ni salama kwa matumizi na kuwa dawa hizo zimekuwa zikitumiwa na watu wengi kwa muda mrefu na kuwaponya ama kupata nafuu.

Dkt. Gwajima amewataka wataalamu wote na wajuzi wa tiba asili wasisite kujitokeza na kufuata taratibu za kuwasilisha dawa na bidhaa zao kwa mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali ili zifanyiwe uchunguzi wa kimaabara kabla ya kukabidhi taarifa ya matokeo ya uchunguzi Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Waziri amesisitiza kwenye kujikinga na hivyo Serikali imeboresha kwenye viwanja vya ndege,mipaka pamoja na sehemu za kupimia magonjwa mbalimbali ili yasiingie nchini kwa watu wanavyoingia na kutoka.

“Tiba asili sio jambo la leo,tumezaliwa tumeona akina mama zetu wanatumia baadhi ya majani kwa kutibu mafua au homa na kujifukiza na baada ya hapo wanatoka salama na kuendelea na kazi,hivyo tiba asili haijatokana na ugonjwa wa Corona bali ni kutoka enzi na enzi”.

Dkt. Mollel amesema hatua za usafi zinatakiwa kuongezwa nguvu na kuwataka wataalamu wa afya kuacha kufikiria mgonjwa anavyoenda kwenye kituo cha afya anaumwa kifua ana Corona bali kuhakikisha wanampima vipimo vingine ili wasije kuuwa watu na mambo mengine ambayo hayana uhusiano na Corona.
View attachment 1691879View attachment 1691881View attachment 1691882View attachment 1691883
Akionesha mfano wa kujifukiza kwa Waandishi wa Habari
View attachment 1691886View attachment 1691887View attachment 1691888
View attachment 1691889
Sawa. Corona ipo
 
Naomba kufahamu utaratibu wa kuzipata hizi NIMRCAF kwa Bei ya jumla. Nimepiga simu huko siku nzima hazipokelewi.

Wanasanyansi wa kitanzania wa National Institute for Medical Research (NIMR) ndio wamefanya huo utafiti. Huwaamini wanasayansi wetu? Ulitaka wawe wakoloni wazungu waliojaa kichwani kwako ndio wafanye uwaamini?
 
Mimi nilianza kutengeneza juisi ya matunda ya asili kabisa.

Nachukua Orange, apple, Banana, limau au ndimu nasaga kwa blender na usiweke sukari.

Hii juisi safi sana natural wanywa kila asubuhi.

Hata watoto wawapatia hii, safi sana.

Punguza pombe, achana na sigara na fanya mazoezi na utoke jasho khasa.

Saa nzuri kukimbia ni asubuhi kati ya saa 11 na saa 7 na jioni ni kati ya saa 12 na saa 7 kukiwa kumepoa.

Ila tusisahau kuepuka misongamano isiyo lazima na ikibidi vaa barakoa.

Nawa mikono kwa kutumia maji ya sabuni na osha mikono kwa vitakasa maji.

Watu hawakumwelewa uzuri raisi wetu JPM wanadai amesema hakuna Korona Tanzania.

Lakini hapohapo wanasahau kasema kwamba kuna watu wamekwenda kuchomwa chanjo na wamerudi Tanzania na wameleta ugonjwa.
Wataje watano walioenda kuchoma hiyo dawa
 
kama madini mnayo mlishindwa nini kutengeneza simu zenu
Swali la kitoto
Kwenu Ardhi mnayo kwa nini huwa unaenda dukani na sokoni kununua vyakula kwa nini usilime kwenu uagize vya shambani kwenu
 
Imeshindikana tu kukubali ukweli wacha tuendelee kujivukiza hamna namna
 
Ndio.
Wewe unadhani nami ni kilaza kama wewe na huyo YEHODA mnaozungumzia mambo msiyoyajua kabisa kana kwamba mnajua lolote?
Weka hapa maandishi ya huo utafiti halafu ndipo uhoji kama sijui kuudadavua.

Weka maandishi ya hizo tafiti kabla ya kuhitimisha kama ninao uwezo wa kuzidadavua na kuzielewa au la.
Wewe ni daktari uliyekariri dawa za wazungu umebobea kwenye dawa za wakoloni wazungu ndio maana kichwa chako kimekaa kizungu zungu hata kutembea unatembea kama mzungu wakati n mndengereko wa kimanzichana
 
Back
Top Bottom