DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Yaani Kila kitu kinautaratibu, nikifanya langu mm hapa, watakuja waseme waziri kakurupuka. Wote huwa tunafuata utaratibu huu huu, kuwa kwa haraka waziri huwa nasema hili baya au hili liko hivi, na nimesema hapo tayari. Sasa, kinachofuata ni kuwa, ataitwa na kamishna, atahojiwa ilikuwaje kafikaje huko alikofika, atasema, huenda wengine wataunganishwa maana uelewa utakuwa sasa mpana. Inaweza gusa huko shuleni alikokuwa lakini pia watoto watahitaji huduma na wazazi pia watahitaji huduma, yaani mfumo mzima uliguswa utahusika kwenye hatua mbalimbali Kila mmoja kwa nafasi yake kama ni kupata unasihi au kuwajibika. Na hapo baada ya huo uchambuzi ndiyo wizara itasema ikaja ikaenda ikawa hivi na Sasa kilichofanyika hiki. Halafu Sasa maoni yatatolewa je nn kimesahaulika au kimeachwa wapi Ili hatua zaidi ziendelee juu eneo hilo. Nadhani huu ni utaratibu mzuri kabisa, au vipi ndugu zangu?

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Upo sahihi Dokta.

Bila utaratibu hakuna usahihi au tija nzuri
 
Anawauliza watoto wanaochukiwa na baba zao. Je amewaandaa kisaikolojia? Mbona yaonekankama ni udhalilishaji kwa watoto na wazazi wao. Angalia clip hapa

Hii haikubaliki, huyu amejisahau. Na shule iliyobariki imejisahau.

Ili binadamu yoyote awajibike, lazima kuwepo na hofu au maumivu. Bila hofu au maumivu mwanadamu hawajibiki.

Kwa matiki hiyo; mzazi kumweleza mtoto kuwa usiposhinda mitihani yako ya form four, jua mimi si baba yako, ni kumtia hofu ili awajibike.

Mhe. Dr Gwajima - WAZIRI saidia hapo
 
Naona Sana, najitahidi Sana kushirikiana na jamii kuchukua hatua, hata niwe wapi siachi kuchungulia nini kinaendelea na kusaidia jambo pale ninapoona niongeze nguvu, ila pamoja na kuja hadi humu, wenzako wengine wanaona ni upuzi tu kwa kuwa mara ingine naweza kutofautiana nao [emoji28]. Anyway ndiyo uongozi na binadamu ni sisi sisi, Iko siku ya kale yatapita na tazama yatakuwa mapya, tutapumzika na yote, tuendelee kushirikiana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Ndiyo hivyo Dr, penye wengi pana mengi. Lakini tunaiona nia yako njema ! Keep it up Dr!
 
Ahsante Sana, pamoja na kuwa Niko safari mbali Sana na masaa yanatofautiana, Mungu alinipa Rehema za kuona. Kwa kweli hili jambo halina afya kabisaaa.

Pamoja na uchovu na usiku wote huo: nilihakikisha katika hatua za awali Nampata mhusika na kumwambia hili jambo ni baya, halifai na ni kinyume na sheria ya mtoto na huduma za ustawi. Aache mara moja. Aidha, nimeelekeza ofisi yangu washughulikie kwa stahiki zote zinazohusika na asitokee mwingine kufanya mambo haya hayafai.

Ahsante Sana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
🙏🙏🙏
 
Nakubaliana na wewe. Lakini kuna wakati Roho wa Mungu ananiambia niseme nao tu tena kwa hekima na upole Ili labda watapona dhidi ya mzigo wa chuki ambao nadhani wengi wametwishwa kwa kusudi la mwovu au wamejitwisha tu wao wenyewe mzigo ambao hata hawana safari nao. Hivyo, labda itawaponya.

Ila nawasoma kuwa wengine wako kimkakati kabisa na kadri ninavyowatambua nami kweli sasa nitawapotezea Ili waendelee na lao nami na langu. Halafu Baraka za Mungu zitatimia kwa Kila mmoja kwa kadri ya Rehema zake atujuaye wote. [emoji1666] Ubarikiwe. Ahsante Sana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Ckuwahi fikiri kama muheshimiwa waziri ungeweza kureply hizi text na kusikiliza maoni mbalimbali ya wadau wa jamii forum.

Hakika hii n kaz nzuri iliyotukuka. Ila Lai yangu kwa wanajamii forum wenzangu baada ya kuona tatzo limetokea tusiwe watu wa mbele kulaani na kutukana bali kupitia Hilo tatzo hakika iwe n changamoto na fursa ya kutoa mawazo yetu na kushauri nn kifanyike na wapi tunakosea ilimradi kesho hyo kitu isijirudie.

Na hii ndo solution ambayo inaweza tufikisha mbali zaidi.[emoji120]
 
Ain’t trying to play gender card, atleast not here sweet!

ala la muda, hao wasichana hapo ni wakubwa, probably wanaelewa vizuri kilichotokea kwenye maisha yao na wazazi wao.
Unaambiwa mtoto huyu hakuonja malezi ya baba na mama wakiwa wanaishi katika nyumba moja. Nakuomba uelewe kitu kimoja, mwanaume kumkataa mwanamke ni dhambi kubwa katika maisha ya mwanamke kiasi kisasi hicho hakitakaa kiishe hadi kiama. Na bahati mbaya muwe na mtoto, mwanamke atakuchapa kupitia mtoto.

Ila Mwanamke akimkataa mwanaume hapo maisha yanasonga. Na watoto ambao mama ndio waliwakataa Baba za watoto, hutasikia malalamiko ya watoto kwa baba zao.

Ushauri wa bure; kwa vijana kama unaona mambo hayaendi na ukaamua kushika hamsini zako; jitahidi mama akukatae yeye. Kila wakati kuwa mnafiki na kujifanya bado unampenda na kumtaka. Wanawake wanapenda UBOSI ujue.
 
Mheshimiwa Waziri, nashauri watu kama hawa muwe mnawapa semina, ili wafanye kwa usahihi.

Pili, mheshimiwa Waziri natamani ungetembelea kituo cha watototo flani...nisikitaje jina au utume wataalam wako.

Kuna mtu amewajaza kituoni, anapewa misaada ya waziwazi na wazungu na raia pia lakini jioni yake anapeleka kuuza vyakula kwa maduka makubwa na watoti wana hali mbaya sana.

Nitawasilishaje hili kwako?

Mtaani kwetu kila mtu analaani hili, tumemuonya mhusika tumechoka.
Kibaya zaidi ni Diwani wa ccm
Mkuu, usingetaja wadhifa wake wa udiwani, kufanya hivyo kutamfanya achukue tahadhari ili kuficha ukweli.

Lakini umefanya vyema kuonesha kukerwa na uovu unaotendeka. Mh. Waziri kaweka mawasiliano yake humu. Mpigie simu au umtumie sms. Huyu mama yuko serious sana na kazi yake. Naamini ukimpa maelezo yanayojitosheleza, atachukua hatua haraka sana. Huwa haachi zege lilale.
 
Hii haikubaliki, huyu amejisahau. Na shule iliyobariki imejisahau.

Ili binadamu yoyote awajibike, lazima kuwepo na hofu au maumivu. Bila hofu au maumivu mwanadamu hawajibiki.

Kwa matiki hiyo; mzazi kumweleza mtoto kuwa usiposhinda mitihani yako ya form four, jua mimi si baba yako, ni kumtia hofu ili awajibike.

Mhe. Dr Gwajima - WAZIRI saidia hapo
Kabisa, kumwambia mtoto usilete zero ndani kwangu ni kutokuwajibika? Kwahiyo anataka tukawafanyie quez mashuleni?
 
Mkuu, usingetaja wadhifa wake wa udiwani, kufanya hivyo kutamfanya achukue tahadhari ili kuficha ukweli.

Lakini umefanya vyema kuonesha kukerwa na uovu unaotendeka. Mh. Waziri kaweka mawasiliano yake humu. Mpigie simu au umtumie sms. Huyu mama yuko serious sana na kazi yake. Naamini ukimpa maelezo yanayojitosheleza, atachukua hatua haraka sana. Huwa haachi zege lilale.
UShauri umefanyiwa kazi
 
Ahsante Sana, hata wewe ninakubariki tu. Mungu akipenda, atakusaidia kuona.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Dr, tafadhali usiupoteze muda wako kuwajibu watu wanaotaka kukutoa kwenye reli. Kama ni muhimu kuwajibu watu wa aina hiyo, utuachie sisi, tutawajibu kwa kadiri tutakavyoona inafaa. Vinginevyo, ni kuwapuuzia tu.

Wewe shughuli na yale ya msingi🙏
 
Nakubaliana na wewe. Lakini kuna wakati Roho wa Mungu ananiambia niseme nao tu tena kwa hekima na upole Ili labda watapona dhidi ya mzigo wa chuki ambao nadhani wengi wametwishwa kwa kusudi la mwovu au wamejitwisha tu wao wenyewe mzigo ambao hata hawana safari nao. Hivyo, labda itawaponya.

Ila nawasoma kuwa wengine wako kimkakati kabisa na kadri ninavyowatambua nami kweli sasa nitawapotezea Ili waendelee na lao nami na langu. Halafu Baraka za Mungu zitatimia kwa Kila mmoja kwa kadri ya Rehema zake atujuaye wote. [emoji1666] Ubarikiwe. Ahsante Sana.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
🙏🙏🙏
 
Huyo akishaona majina ya kigalatia mfano kina Ester,Dorika or Dorice,Maria n.k mapepo yanampanda....
Jana kwenye uzi mwingine nikaona anamparamia Dk. Gwajima analeta ubishani wa kijinga licha ya kupatiwa majibu sahihi. Nikataka nimwambie waziri kuwa huyo bibi kuna sababu nyingine inayofanya alete ubishani na sio hoja iliyo mezani, ila nikasita. Bahati nzuri mods wamepita naye, bibi yupo segerea ya JF anasoma kama guest muda huu.
Yaani anakuwa mjinga mjinga licha ya kuwa kwa umri anaweza kuwa amewapita 90% ya wanaJF.
 
Dr, tafadhali usiupoteze muda wako kuwajibu watu wanaotaka kukutoa kwenye reli. Kama ni muhimu kuwajibu watu wa aina hiyo, utuachie sisi, tutawajibu kwa kadiri tutakavyoona inafaa. Vinginevyo, ni kuwapuuzia tu.

Wewe shughuli na yale ya msingi🙏
Sidhani kama una msaidia dr, ungekuwa unamsaidia ungeshafanye press release juu ya hili, mwache dr ajipambanie, dr tutakuunga kwenye group la friends of samia tunaona kazi za mawaziri wa madini viwanda afya wewe hatukusikii
 
Ustafute umaarufu kwa mambo ambayo wewe ni mbumbumbu. Bakia kwenye fasishi zako tu zisizo na kichwa wala miguu.

Hivi ni watoto wangapi wanajuwa ni nani analipa ada ya shule? Mimi binafsi niko na mke wangu miaka zaidi ya 30. Suala la ada za shule huwa mke wangu ananipa summary ya mahitaji ya watoto na ninamkabidhi. Na yeye ndiyo ana deal na kuwalipia.

Sasa Lillian Mwasha akikutana na mwanangu akamuuliza swali kama hilo si atajuwa kuwa na mimi nimemtlekeza mwanangu!!

Hebu Robert Heriel Mtibeli soma majibu ya waziri kwenye comments mbalimbali ukiwa na akili yenye utulivu, utaelewa kosa la Lillian Mwasha
Heriel ana andika vizuri sana fasihi...lakini acha ujuaji kwenye asiyoyajua!
 
Kudos Mheshimiwa, suala la wazazi kutelekeza watoto ni suala moja, Alilolifanya Lilian ni suala lingine kabisa ambalo ndilo lengo la hii thread.

Umeelewa kwa usahihi mheshimiwa, na umechukua hatua sahihi.

By the way, kuna miongozo ya kufanya kazi na watoto (working with children), ili kutokusababisha Vulnerability na harm. Hili litiliwe mkazo, sio kila mtu anapaswa kupewa access na watoto tena wa sensitive issues kama hizi.
Bila shaka wewe ni Muamala Jamii!
 
Kumbe kaliwa kichwa ...safi sana..hivi haoni aibu ,hata kaa Waziri hayupo sahihi( sio Kwa muktadha huu) Mpe hata heshima yake !
Hivi ni Mawaziri wangapi wamepita hiyo sekta ,walikuwa passive ...huyu anafanya vizuri! Tumpe Moyo ! Ninaongea haya Kwa uzoefu mkubwa!

Back
Top Bottom