Waziri Jerry Silaa ana kitu, atafika mbali, abarikiwe

Waziri Jerry Silaa ana kitu, atafika mbali, abarikiwe

Hapana,anachokifanya ni siasa.yaani katika hali ya kawaida atawarudishia hao walalamikaji maeneo yao,then aliyenyanganywa ataenda mahakamani atashinda kesi,then atamtoa tena mlamikaji.silaa hatokuwepo miaka yote.
Hii imetokea kariakoo.
Maneno ya waziri sio sheria.
Alichotakiwa kufanya ni kitengeneza platform nzuri ya utatuzi wa migogoro ya ardhi,na sio kuruka ruka kama kuku.
Huu ni ujinga,ni siasa za kizamani za kimagufuli.
Basi tufunge mhakama,na tuwaambie mawaziri wote wawe majaji
We utakuwa walewale majambazi ya ardhi. Jifunzeni kukubali kazi nzuri
 
We utakuwa walewale majambazi ya ardhi. Jifunzeni kukubali kazi nzuri
Tena huyo Mfanyabiashara tapeli Mmasi achunguzwe na vyombo vya Dola kwenye chanzo cha kifo cha Marehemu mwenye Nyumba,huwenda likawa ndiyo lilimtanguliza Marehemu mbele ili lijipatie Mjengo wa bure! Na utajiri wake uchunguzwe kwa kina! Tunaweza tukawa tunafuga majoka bila kufahamu!!
 
Hakuna mahali popote Jerry Silaa amefanya ionekane kuwa kazi yake ni "mbadala wa mahakama". Matatizo yote aliyoyashughulikia ni ya uonevu wa baadhi ya watu wanaojiona wao wana uwezo dhidi ya wengine wanaowaonea. Ni hawa hawa kila mara wanaoyatumia hayo mahakama kimakosa kuhalalisha uovu wao

Ukimwondoa Magufuli, na sasa Samia kwa njia tofauti anazotumia kulazimisha mahakama zifanye kazi zake kwa kuangalia wanayoyataka wao; hakuna viongozi wengine chini yao wanaoweza kulazimisha makhakama zifuate matakwa yao.

Haya mnayoyasisitiza hapa, ni yale yale ya utegemezi wa kufanyiana 'favor'. Hakimu anaamua kesi ili amfurahishe waziri, anayemtegemea naye arudishe 'favor' ile ile kwa hakimu katika mambo ambayo waziri anayasimamia.
Hapa mnahusisha hata mawaziri wasiopenda njia hizo, kwa sababu zenu mnazozijuwa wenyewe.
Bado Tanzania tupo chini sana Ki-weledi kuona sawa tu wanasiasa wawe waamuzi wa migogoro ya ardhi. Na hao hao wanasiasa ndio wanaoamua nani ashinde uchaguzi nani atoswe! Na mmeridhika na hata kuunga mkono ushenzi huu!
 
Ungejua power za Commissioner usinge andika hivi..nenda ukasome Quasi Judicial Tribunals ni nini ?
Kama kamishna wa ardhi ana haki ya kuamua kesi ya ardhi basi mfumo wetu wa haki haupo sawa.
 
Hadi hapo, waziri ana mamlaka kumtoa Mmassy kwenye nyumba hiyo kufuatana na mmiliki halali tayari anafahamika, na Mmassy ana kesi ya kughushi hati na mkataba wa mauziano.
Sasa hii kesi inatatuliwa na waziri Slaa yeye kama nani, Mahakama?!
 
Sasa hii kesi inatatuliwa na waziri Slaa yeye kama nani, Mahakama?!
Wwe lazima utakua ni mtoto wa Mmasi,maana akili zako ziko kama za Mmasi kubisha kila kitu anacho aambiwa na Mamlaka! Wwe Umeambiwa nenda.kasome hicho kifungu ,kusoma hujasoma lakini bado waleta ubishi! Kichwa kama guluguja!!
 
Bado Tanzania tupo chini sana Ki-weledi kuona sawa tu wanasiasa wawe waamuzi wa migogoro ya ardhi. Na hao hao wanasiasa ndio wanaoamua nani ashinde uchaguzi nani atoswe! Na mmeridhika na hata kuunga mkono ushenzi huu!
Nani kasema ameridhika, kama siyo watu kama nyinyi mnaonyonya uchafu (chawa) toka kwa hao wanasiasa unaowazungumzia hapa.
Angalia mada zote, hata humu JF, huwezi kukosa kujuwa ni kundi gani linaloleta matatizo makubwa kwa waTanzania kwa kukumbatia maharamia haya yaliyopo madarakani.
Haihitaji kazi kubwa, kujua msimamo wa mtu kama wewe upo wapi, kwa sababu michango yako humu ipo wazi.
Sasa unakuja hapa na kujilalamisha, kutupia waTanzania lawama huku ukijua wazi CCM imewaweka mateka. Hawa waTanzania hawana njia za kuwaondoa hawa majambazi, kwa sababu wanatumia vyombo vyetu vitukandamize tunapopaza sauti za kukataa; halafu watu kama wewe mnashangilia!
 
Bado Tanzania tupo chini sana Ki-weledi kuona sawa tu wanasiasa wawe waamuzi wa migogoro ya ardhi. Na hao hao wanasiasa ndio wanaoamua nani ashinde uchaguzi nani atoswe! Na mmeridhika na hata kuunga mkono ushenzi huu!
Mkuu tuna tatizo kubwa sana, la kuweka siasa kwenye kila kitu. Yaani ni propaganda kila sehemu. Kwa hali hii sijui tunaweza kuzalisha vijana ambao wanaweza kukaa mezani na wazungu, halafu pakawepo na win win situation. Kama anaacha kuhangaika na sera pamoja na mipango, anaenda kusuluhisha kesi mitaani, wengine wanaenda kukagua feni kwenye kivuko, dah tutafika kweli?
Sasa hivi kuna mafuriko, kuna ongezeko kubwa la makazi holela, kuna upimaji na uuzaji wa maeneo kiholela, unakuta madalali wanakata viwanja 10mx10m wanaweka barabara za 3m kiasi kwamba magari hayawezi kupita.
Watu wanavamia na kujenga hivyo katika maeneo hatarishi. Waziri yupo tu anawakamata akina mmasi
 
Kwa kweli huyu baba Allah amlinde zaidi nilimkubali kwenye mgogoro wa nyumba kariakoo pale alionyesha hekima ya hali ya juu
 
Sasa hii kesi inatatuliwa na waziri Slaa yeye kama nani, Mahakama?!
Commissioner wa ardhi na waziri husika, wanao uwezo kutatua migogoro ya ardhi kisheria kabisa,

Soma KAZI ya commissioner wa ardhi wa wizara ana majukumu yepi.
 
Kwa kweli huyu baba Allah amlinde zaidi nilimkubali kwenye mgogoro wa nyumba kariakoo pale alionyesha hekima ya hali ya juu
Anafanya jambo zuri,

Kwa Hali ya kawaida, kumpata commissioner wa ardhi wizarani Si jambo Rahisi,

Lakini Slaa amelifanikisha ,kusaidia ofisi iwafuate wadau walipo.

Abarikiwe.
 
Anafanya jambo zuri,

Kwa Hali ya kawaida, kumpata commissioner wa ardhi wizarani Si jambo Rahisi,

Lakini Slaa amelifanikisha ,kusaidia ofisi iwafuate wadau walipo.

Abarikiwe.
Sijawahi kumuelewa kiongozi yoyote kabla ila huyu nimemuelewa na anafanya kazi
 
Sijawahi kumuelewa kiongozi yoyote kabla ila huyu nimemuelewa na anafanya kazi
Wapo wengi,

Hata Majaliwa kabla hajavutwa shati,

Watumishi, mkurugenzi akisikia PM anakuja eneo lake, walikuwa hawalali USINGIZI,

Mwingine alikuwa Lowwassa, mfuatiliaji sana,

Bila kusahau Magu akiwa Miundombinu,

Bashungwa, Aweso, Biteko, nao wanajitahidi.
 
Yaani ni hopeless kabisa.katika viongozi wa hovyo tulio nao huyu jamaa ni namba moja.

Hajiamini kabisa.anatumia jeshi la polisi kutisha watu.

Sijui kwa nini raisi anaendelea na huyu jamaa.

Kamuabisha shehe kariakoo. Hata sheria za wakfu hazifahamu.

Tanganyika law society, tume ya haki za binadamu, mwanasheria mkuu pamoja na mahakama wanatakiwa watoe tamko kukemea huu ujinga
Acha hao watu wapate haki yao, hivi wewe unaweza mshinda msama mahakamani? Kwavile hii nchi sehemu kubwa ni corrupt acha hao wachache wapate haki yao
 
Kwa sasa muda hautoshi kutengeneza katiba mpya, uchaguzi uko mwaka huu na mwakani.

Halafu katiba haiwezi kuwa na kila kitu, Benki ya Dunia walileta mradi wa hati za kidigitali, mbona hatumsikii akiziongelea? Hizi ndio mzizi wa fitna kwa hao maafisa ardhi wanaocheza na mafaili.

Wizara ya ardhi mwaka jana ilipewa bilioni 350 wajenge ofisi za ardhi kila mkoa, mbona hajazindua hata ofisi moja?
Kwahiyo kwakua hakuna ofisi iliyojengwa ndio raia wasipewe haki zao? Ushawahi dhulumiwa nyumba au kiwanja wewe? Inaumiza sana
 
Migogoro mingi ya ardhi chanzo ni wizara yake,

Na nafasi ya Waziri na maamuzi yake kupitia vikao na taarifa Ofisini kwake Ina umuhimu mkubwa.

Wengi hukosa HAKI wizara ya ardhi ndipo huenda mahakamani.

Kwa case ya Mmassy, tayari imetatuliwa Kwa 50%, mama yule atatumia utatuzi wa Waziri kama mojawapo ya ushahidi na kupata ushindi.

Si lazima kupinga Kila kitu.
Halafu bora mmasy katolewa kwenye nyumba akaendelee kudai anayoiita haki yake huko mahakamani akiwa nje ya nyumba.
 
Swali ni kwamba huyo mmasy hiyo hati kaitoa wapi?
Je hiyo hati ni halali?
Ana uhakika gani kwamba huyo mama hadanganyi?je kabla ya kwenda site alisikiliza pande zote mbili? Au ameenda na maelezo ya upande mmoja halafu ya upande wa pili anaysikilizia pale pale?
Amefanya intensive background search ili kujua historia halisi ya huo mgogoro?
Na hao maofisa wa wizara waliompa mmasi hio hati,wamechukuliwa hatua gani?
Kwa sababu anachokifanya silaa ni kuwalinda maafisa ardhi,na kuwaadhibu wananchi kwa kivuli cha kutetea wanyonge.
Halafu anatumia kigezao gani cha kuchagua kesi anazoenda kuzitatua site?
Na je kati yake yeye na mahakama, tumuamini nani? Mbona asilimia kubwa ya kesi anazotatua site wanaoitwa wanyonge ni jinsia. Ya aina moja tu?
Acha ujinga wewe, kwa kesi ya mzee mmasy tayari wizara ilishamuandikia barua mzee mmasy arudishe hati, pili mzee mmasy aende mahakamani akaishitaki wizara.
Mzee mmasy aliwezaje kuuziwa nyumba na marehemu aliyeko makaburini? Tena nyumba uliyokuwa umepanga
 
Hapana,anachokifanya ni siasa.yaani katika hali ya kawaida atawarudishia hao walalamikaji maeneo yao,then aliyenyanganywa ataenda mahakamani atashinda kesi,then atamtoa tena mlamikaji.silaa hatokuwepo miaka yote.
Hii imetokea kariakoo.
Maneno ya waziri sio sheria.
Alichotakiwa kufanya ni kitengeneza platform nzuri ya utatuzi wa migogoro ya ardhi,na sio kuruka ruka kama kuku.
Huu ni ujinga,ni siasa za kizamani za kimagufuli.
Basi tufunge mhakama,na tuwaambie mawaziri wote wawe majaji
Hao watu waende mahakamani wakaishitaki wizara, kudhulumiwa nyumba inauma sana
 
Back
Top Bottom