Waziri Jerry Silaa ana kitu, atafika mbali, abarikiwe

Kwenye suala la ardhi Mahakama sio msuluhishi wa kwanza, kesi zinaanzia kwenye mabaraza either ya kata na wilaya mahakamani unaenda kuappeal in case umeshindwa.

Silaa yupo sahihi sababu anaongozana na Commissioner wa ardhi na wasajili wa ardhi...ukisoma powers za Commissioner wa ardhi utaona pia wanayo haki ya kufanya Revokation of Right of Occupancy either customary or granted right of occupancy.

Endapo ulifanya forgery, hata ukifanya conveyance au unauza eneo commissioner ni lazima umpe notice kwahyo nakushauri usome sheria ya ardhi vizuri na pia usome power za Commissioner wa ardhi ambaye na yeye yupo chini ya waziri wa ardhi.Pia utambue Jerry ni msomi wa sheria na mimi ninae kuambia hivi ninaijua sheria ya ardhi Kwa uzuri zaidi hakuna jambo baya ambalo Jerry Silaa anafanya zaidi ni kumfanya Commissioner afanye kazi zake Kwa uweredi zaidi.
 
Tupambanie KATIBA mpya Ili waziri asitokane na wabunge.

Hapo mkabeni shati mbunge wa viti maalum akaimu vizuri nafasi ya mbunge awapo katika utumishi wa nje ya Bunge Kwa nafasi ya Uwaziri.
Tunaanzaje kuipambania katiba mpya na wakat wenye katiba yao hawataki wanajua ulaji utapotea tu
 
Ungejua power za Commissioner usinge andika hivi..nenda ukasome Quasi Judicial Tribunals ni nini ?
M

aha ndio mwamuzi wa mwisho wa mgogoro wowote hata makampuni huenda mahakamani kuishtaki serikali endapo inavunja mikataba pasipo utaratibu. Mgogoro wa ardhi baina ya pande mbili hutatuliwa mahakamani na sio wizarani!
 
Hao wote wanaompopoa Slaa wanamakandokanndo kwenye ardhi zao 🤣🤣🤣🤣🤣 chuma kipo njiani kuwafikia. Mtaongea Kijapani mwaka huu
 
Ungejua power za Commissioner usinge andika hivi..nenda ukasome Quasi Judicial Tribunals ni nini ?
Nilichogundua humu wengi hawatumii akili zao kufikiri, wanaendeshwa na uchama,

Ni bendera fuata upepo, hawezi toa maoni yake Hadi asikilizie wanachama wenzangu wanasema nini Kisha naye anaunga tera.

Anachokifanya Slaa na commissioner wa ardhi kipo kisheria kabisa,

Na ni njia nzuri kuwamulika maafisa ardhi walishiriki UOVU huo Ili watumbuliwe na kushtakiwa.
 
Hata hapo alipoanzia ni sawa.Watu wasio na pa kusemea wanadhulumiwa sana
 
Unajua hata mtaani watu wanauziana ardhi kwa kutumia mjumbe bila kumfahamisha Commissioner wala kwenda kwenye ofisi yake kuangalia kuwa is there any encumbrance? baadae ikitokea mgogoro wanalalamika lakini ni mambo ambayo yapo wazi kwenye sheria ila hawayatekelezi. Ila nawashauri unaponunua ardhi nenda katika ofisi za Ardhi kujiridhisha kwanza.
Hao wote wanaompopoa Slaa wanamakandokanndo kwenye ardhi zao [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] chuma kipo njiani kuwafikia. Mtaongea Kijapani mwaka huu
 
Hao wote wanaompopoa Slaa wanamakandokanndo kwenye ardhi zao 🤣🤣🤣🤣🤣 chuma kipo njiani kuwafikia. Mtaongea Kijapani mwaka huu
Na Kuna matajiri wengine matapeli pia wamulikwe,

Akishagundua eneo la wananchi au shamba halina hati, anakimbilia ardhi anapimiwa na kupewa hati bila kuuziwa eneo Hilo na wamiliki au Wana chi.

Hati za namna hiyo pia ni haramu, zifutwe, HAKI ya wananchi ziheshimiwe.
 
hakuna shukurani kwa kila analofanya binadamu, hebu baadhi ya wakati tujaribu kupongeza lile jema linalofanyika.

Shida ya kuachia mfumo ufanye kazi unakuta hao waendesha mfumo (baadhi ya majaji, baraza la ardhi na hata maafisa wa ardhi wenyewe) ndiyo hao walioko mstari wa mbele kudhulumu.
 
Nilichogundua watu wengi wanamponda waziri kwasababu hawajui utaratibu wa case za ardhi zinavyoamuliwa...ukimiliki ardhi kimakosa haina haja ya kwenda mahakamani lakini Commissioner anayo hiyo nguvu ya kutengua umiliki wako. Nawashauri mkasome S.175 ya Tanzania Land Act Cap 113.

Silaa anamsaidia Commissioner kufanikisha majukumu yake kama Commissioner pia anaisaidia mahakama kufanya Execution order.
 
Hata hapo alipoanzia ni sawa.Watu wasio na pa kusemea wanadhulumiwa sana
Imagine maskini kiwanja ni chake kihalali, akiwa anadunduliza kuanza msingi, anasikia kuwa Kuna mtu amekuja anayo hati na amezungushia uzio tayari, ukienda baada ya wiki, unakuta nyumba imesimama tayari,

Ukimuuliza, anakwambia Nina hati na Kwa kuwa nimeshajenga, niuzie, anakupa Bei ya kukugalaliza akijua huna uwezo wa kuendesha case.

Asee Hawa watu wanaudhi,

Watu aina ya Slaa, waombewe sana.
 
Swali ni kwamba, kazi ya waziri ni nini?
Sasa kamq hiyo ni kazi ya kamiahna wa ardhi, kwa nini hawapi nafasi pamoja na kuwajengea uwezo ili waweze kufanya kazi kikamilifu.
Kwa nini hatoi hiyo elimu kwa wananchi ili wajue namna bora ya kutatua migogoro ya ardhi.
Kama maafisa ardhi wana nguvu, na wao ndio wametengeneza hiyo migogoro, mbona hawachukuliwi hatua? Mbona inaonekana ni watu waina fulani tu ndio anaowalenga?
Mimi namuunga mkono kwenda site kwa lengo la kujenga uelewa, lakini napinga mfumo anaoutumia kitatua hiyo migogoro
 
Sorry shell nimemaanisha vituo vya kuuzia mafuta.
Wakati anaingia alianzia kwenye vituo vya mafuta. Kuna vingine akasema vivunjwe. Na akasimamisha ujenzi wa vituo vipya.
Sasa mimi huku mtaani bado naona vituo vinajengwa. Tena kwenye makazi ya watu.
Ni kweli tunahitaji viongozi watendaji, ila utendaji ambao ni SMART
Katika hali ya kawaida, huwezi ukatatua kesi iliyoshindikana miaka 20 ndani ya dakika. Halafu ukasema unetenda haki
 
Kabisa
 
Mwanzo nilipoanza kujibishana nawe sikujuwa kuwa ulikuwa na ajenda maalum unayoisukuma mbele humu JF. Ni ajenda ovu. Jitafakari.
 
Hakuna mahali popote Jerry Silaa amefanya ionekane kuwa kazi yake ni "mbadala wa mahakama". Matatizo yote aliyoyashughulikia ni ya uonevu wa baadhi ya watu wanaojiona wao wana uwezo dhidi ya wengine wanaowaonea. Ni hawa hawa kila mara wanaoyatumia hayo mahakama kimakosa kuhalalisha uovu wao

Ukimwondoa Magufuli, na sasa Samia kwa njia tofauti anazotumia kulazimisha mahakama zifanye kazi zake kwa kuangalia wanayoyataka wao; hakuna viongozi wengine chini yao wanaoweza kulazimisha makhakama zifuate matakwa yao.

Haya mnayoyasisitiza hapa, ni yale yale ya utegemezi wa kufanyiana 'favor'. Hakimu anaamua kesi ili amfurahishe waziri, anayemtegemea naye arudishe 'favor' ile ile kwa hakimu katika mambo ambayo waziri anayasimamia.
Hapa mnahusisha hata mawaziri wasiopenda njia hizo, kwa sababu zenu mnazozijuwa wenyewe.
 
Marinda huna, unatembea mzigo unamwagika

Waziri anampamba tu, akienda mahakamani wanafuta, waziri hana maamuzi ya mwisho kuhusu haki, endelea kukenua masaburi tu

Achakukatisha tamaa watu wewe jamaa ndo Mana wazir anawachukua na kuwafungulia kes ya unyang’anyi wao mzee
 
Marinda huna, unatembea mzigo unamwagika

Waziri anampamba tu, akienda mahakamani wanafuta, waziri hana maamuzi ya mwisho kuhusu haki, endelea kukenua masaburi tu

Unaona mtu anashindwa kujieleza kiwanja kapataje mbele ya wazir sasa huko mahakaman anakwenda kueleza nn zaidi ya rushwa na uchawi we nae usipo angalia utakua mchawi ndan ya uzee wako aisee
 
Tanzania tunahitaji mawaziri kama hawa si watu kama January Makamba na Nape
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…