Waziri Katambi apiga marufuku mikutano ya siasa kwa vyama vyote
Naona tunafunga tena madirisha na milango na kuna watu wameshiba maharage.

Kwangu mimi, hizi siasa siku mbili tatu ziliwafanya watu watoe ya moyoni, hiyo ni tiba nzuri.
Sasa kuna sehemu watatafuta ya kuhemea, hope serikali ipo makini na udhibiti na elimu tusije kuja na maelezo kuwa walishawishiwa na wanaharakati baada ya madhara makubwa.
Serekali ya CCM na umakini wapi na wapi?
 
Leo bungeni Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katamb ameagiza Jeshi la Polisi kusitisha vibali vya mikutano ya siasa kwa kipindi kisichojulikana.

Moto umekuwa mkali na uwanja umeinama kwa upande wa CCM hadi kuomba tena Msaada wa jeshi la polisi , ingawa wananchi tuliwaonya CCM kuwa vita hii ya kubishana na CHADEMA mtaangukia pua lkn walibisha.


Waziri wa Mambo ya ndani, akiwa bungeni amesema

''Kwa sababu ya taharuki hizi ambazo zimekuwa zikiendelea, nitatumia fursa hii pia, Mheshimiwa Spika, kwa sababu tumekuwa tukisikia majibizano ya hapa na pale, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ni custodian wa peace, order, and tranquility, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo tumepewa instrument na dhamana ya kusimamia amani, ulinzi na usalama, na kwa sababu chochezi wa mambo haya umeonekana zaidi kwenye maeneo ya kisiasa.

Ameongeza, kupitia Bunge lako tukufu, namuelekeza IGP Wambura asitoe vibali kwa kazi zozote zitakazokuwa zinahusiana na kufanya mikutano ya hadhara katika kipindi hiki kwa chama chochote, iwe Chama cha Mapinduzi, iwe chama chochote kile kwa kipindi hiki.

Amemalizia kwa kushauri 'Ni vizuri turudi katika kuwaruhusu wananchi wajenge uchumi wa nchi yao. Ni katika kipindi ambacho tunahitaji kufanya kazi kwa ajili ya kuhakikisha kila Mtanzania, wafanyabiashara, wawekezaji, wanafanya kazi yao kwa amani na utulivu. Nafanya hivi, Mheshimiwa Spika, kwa sababu katika mazingira haya, tutakapokuwa tunawatafuta wahalifu, ni ngumu kuchambua wahalifu kwenye mkusanyiko ya watu wengi."
#SamiaMustGo 77
 
ila chadema wajinga sana, wanapeleka moto balaa

waliona wakimfunga TL wamemaliza changamoto imeibuka mashine nyingine

hakuna siku nilicheka kama alipo sema kama shule aliyo soma ingekuwa ya CCM angeacha shule

yule dogo anaye omba mdahalo na heche aaambiwe kabisa wakubwa zake wametupa taulo mapema kabisa kabla jamaa ajamaliza ziara
 
Je anayo hiyo Mamlaka ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa? Wanasheria tunaomba majibu yenu tafadhali. Huu moto anaouwasha Heche mawaziri kama hawa machawa, wanashindwaje kuchanganyikiwa? Hii Dunia ina vituko sana ety mtu kama huyu ety ni kiongozi wizara nyeti kama hii alafu Heche ambaye ni genius yupo mtaani.
 
Patrobas katambi kunani kaka
GhfJRpEacAEgTRK.jpeg

Hii takataka meno kama anakula mavi ya ng'ombe.
 
Huyo katambi kapigwa biti na heche kuwa hamuwez na hata muweza kwa lolote naona limemuingia katambi kakimbilia mtutu sasa.

Tunarud kule kule tulichokosea kipindi kile kuminya watu wasiongee imerud tena. Hili bomu ni kubwa kuliko litakalo kuja
dogo alitaka kubato na heche kapigwa spana mbili kakimbilia kujitutumua hata kwa kitu hana mamlaka nacho

spana atapigwa tu hata kwenye mitandao
 
Kwahy waziri anavunja katiba huku akishirikisha na jeshi la polisi liingie kwenye vitendo hivyo kupitia mamlaka aliyonayo! Aiseee mbona mambo yapo wazi sanaa, tunapoelekea "SIO" pazuri.
 
kweli....(Hatutaki CCM,wala chadema,wala chama chochote kile kufanya shughuli za kisiasa)
NI HATARI SANA KUIGA MFANO WA SIASA ZA KENYA SIASA MIAKA YOTE MINNE MPAKA KUANGUKIA UCHAGUZI,NO TUSIFANYE HIVI,
Mnataka siasa zifanyike kipindi cha uchaguzi tu.

Kwani kazi za vyama vya siasa ni nini?, nyie Ccm mtaweza kutekeleza hilo?...

JPM alitangaza hilo zuio pia, ila tulishuhudia chama chake pekee kikifanya siasa huku wengine wakipigwa 'stop', naona mmeamua kurudia hilo.
 
Back
Top Bottom