Waziri Katambi apiga marufuku mikutano ya siasa kwa vyama vyote
CCM hawaelewi washike wapi au waachie wapi..

Wamejifanya kuachia mikutano ili kuionyesha dunia kuna demokrasia matokeo yake CHADEMA nondo wanazopiga kwenye mikutano ni za moto sana, kiasi kwamba upepo unabadilika na watu wanaonekana kuelewa sana. CCM uvumilivu umewashinda na wamerudi tena kuanza kutumia mabavu.

Wakipiga marufuku mikutano ndio kama hivyo wanazidi kujichafua kwa uminyaji wa demokrasia, wakisimama ni mshale na wakikaa ni mshale.

Siku ya kufa nyani miti huteleza, by the way sina chama lakini huo ndio ukweli. asipo Polisi CCM hawana uwezo kupambana na CHADEMA.
Mimi nampongeza Sana huyu MTU ambaye amebuni haya maandamano ya 7/7 kwasababu hata kama hayatafanyika bado serikali itapata hasara kubwa Sana Kiuchumi, hakuna mtanzania atatoka na familia yake kwenda sabasaba maonesho

Nchi IPO kwenye Uzi mwembamba sanaa
 
Nakuuliza tena umeshalipwa? jibu swali acha kuongea kama umewekewa betri mpya
Gentleman,
huna haja ya kumbwelambwela vitu useless mezani,

huna point kaa kimya au kaa pembeni, acha wadau watoe maoni na fikra mbadala bora zaidi ya hoja au komenti zinazowasilishwa jukwaani.

unarukarukaruka tu huku ukiwa pointless na na verified baj 🤣
 
Kwa adilimia wanazodai wameshinda kwanini wanaogopa mikutano ya kisiasa
Teh teh teh 😃 😃 😃 wanadai Ili Wananchi Sasa wajenge nchi , Kumbe ni hofu ya Upinzani.. haaaaaaa haaaaaaa
Wanasema wamechaguliwa na wapigakura zaidi ya milioni 30; huu woga sijui unatoka wapi!
Hatari sana
 
Gentleman,
huna haja ya kumbwelambwela vitu useless mezani,

huna point kaa kimya au kaa pembeni, acha wadau watoe maoni na fikra mbadala bora zaidi ya hoja au komenti zinazowasilishwa jukwaani.

unarukarukaruka tu huku ukiwa pointless na na verified baj 🤣
Vip kichwani kwako unafunza wangapi??
 
Leo bungeni Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katamb ameagiza Jeshi la Polisi kusitisha vibali vya mikutano ya siasa kwa kipindi kisichojulikana.

Moto umekuwa mkali na uwanja umeinama kwa upande wa CCM hadi kuomba tena Msaada wa jeshi la polisi , ingawa wananchi tuliwaonya CCM kuwa vita hii ya kubishana na CHADEMA mtaangukia pua lkn walibisha.


Waziri wa Mambo ya ndani, akiwa bungeni amesema

''Kwa sababu ya taharuki hizi ambazo zimekuwa zikiendelea, nitatumia fursa hii pia, Mheshimiwa Spika, kwa sababu tumekuwa tukisikia majibizano ya hapa na pale, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ni custodian wa peace, order, and tranquility, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo tumepewa instrument na dhamana ya kusimamia amani, ulinzi na usalama, na kwa sababu chochezi wa mambo haya umeonekana zaidi kwenye maeneo ya kisiasa.

Ameongeza, kupitia Bunge lako tukufu, namuelekeza IGP Wambura asitoe vibali kwa kazi zozote zitakazokuwa zinahusiana na kufanya mikutano ya hadhara katika kipindi hiki kwa chama chochote, iwe Chama cha Mapinduzi, iwe chama chochote kile kwa kipindi hiki.

Amemalizia kwa kushauri 'Ni vizuri turudi katika kuwaruhusu wananchi wajenge uchumi wa nchi yao. Ni katika kipindi ambacho tunahitaji kufanya kazi kwa ajili ya kuhakikisha kila Mtanzania, wafanyabiashara, wawekezaji, wanafanya kazi yao kwa amani na utulivu. Nafanya hivi, Mheshimiwa Spika, kwa sababu katika mazingira haya, tutakapokuwa tunawatafuta wahalifu, ni ngumu kuchambua wahalifu kwenye mkusanyiko ya watu wengi."
Yeye anadhani ni ishara ya nguvu kumbe ni ya udhaifu.

Amandla...
 
Ninaakili kubwa kuliko wewe
Yes,
ni sawa kabisa kwamba una akili kubwa kuliko yangu na pengine kuliko hata wadau wote wa humu JF,

Lakini ingependeza zaidi ukawa unaitumia akili kubwa hiyo uliyonayo kutoa mawazo mapya na fikra mbadala bora zaidi ya komenti za wengine humu jukwaani na itapendeza zaidi, kuliko kumbwelambwela mambo useless,

okay?šŸ’
 
Mwenye uelewa na waziri mwenye dhamana na vyama vya siasa atusaidie hapa.
Na kama ni huyu Katambi basi tujue sheria, kanuni na utaratibu uliomwongoza au unaotakiwq kufuatwa kabla ya kutangaza zuio.
Na je, ni sahihi kwenda mahakamani kudai haki ya kufanya siasa wakati wowote na mahali popote bila vikwazo vyovyote?
Nyongeza ya hayo, huyu waziri haoni kama anahamasisha maandamano ya 7/7 na au kayapiga pini kiana kwa hilo zuio lake?
 
Yes,
ni sawa kabisa kwamba una akili kubwa kuliko yangu na pengine kuliko hata wadau wote wa humu JF,

Lakini ingependeza zaidi ukawa unaitumia akili kubwa hiyo uliyonayo kutoa mawazo mapya na fikra mbadala bora zaidi ya komenti za wengine humu jukwaani na itapendeza zaidi, kuliko kumbwelambwela mambo useless,

okay?šŸ’
Una hoja gani zaidi ya useless IQ yako ndogo,upeo mdogo point huna kama Samuya
 
Back
Top Bottom