Waziri Mbarawa: Mlango wa ndege ulifunguliwa na mhudumu

Kwamba Majaliwa wa Mchongo ndie aliefungua mlango au?

Majaliwa ni shujaa

Nyie endeleeni kukalia politiki

Maana mwanasiasa akikuambia nje kuna nyesha…toka mwenyewe uloe ndio utaamini…
 
Kamwambie Waziri Mbawara atakupa majibu ungeweza ungetokea kwenye ile press release umtwange hayo maswali yako, yeye kaona chenye umuhimu ni kujua nani shujaa halisi alieufungua ule mlango na kuokoa watu 24 kutoka kwenye ndege? Jibu: wahudumu wa ndege, na ndilo jibu alilokuja nalo
 
Kwa hiyo tuache kujadili kwa nini serikali ilichelewa kuokoa watu tujadili mlango ulifunguliwa na nani?

Tuache kujadili mabehewa mtumba kununuliwa kwa bei ya mapya?
 
Nimeshawahi kupanda ndege mkuu…huo mlango watatoa Loki kwa ndani lakini kupush lazima nguvu nyingine kwa nje isaidie
Mlango wa ndege hauhitaji nguvu nyingine kutoka nje ili ufunguke. Tuliowahi kufanya kazi viwanja vya ndege siku zote tulikuwa tunaona na kusimama kwa mbali mara baada ya ndege kutua. Milango mara zote ilikuwa inafunguliwa kutoka ndani, bila usaidizi au nguvu yoyote kutoka nje. Labda kama ndege zinatofautiana au kwa sasa utaratibu umebadilika wa kufungua milango ya ndege.
 
Majaliwa ni shujaa

Nyie endeleeni kukalia politiki

Maana mwanasiasa akikuambia nje kuna nyesha…toka mwenyewe uloe ndio utaamini…
Wavuvi wenzie wamemkataa, ndio maana Waziri Mbarawa kam-disqualify, na ukweli umejitenga na uongo that's how it's
 
Ni upepo utapita!
 
Umeambiwa mlango wa dharura
 
Kwani nani anayebisha?... Mbona hata sisi tunafahamu hivyo.
 
Imekuwa kinyume, kwa sasa serikali ndio inaongoza kwa uongo. Na tabia hii ya serikali kusema uongo ilishika kasi sana awamu ya tano ili kusaka sifa za kijinga.
Awamu ya tano ahijawahi kukuacha salama lazima ikubutue hata kama haipo
 
Imekuwa kinyume, kwa sasa serikali ndio inaongoza kwa uongo. Na tabia hii ya serikali kusema uongo ilishika kasi sana awamu ya tano ili kusaka sifa za kijinga.
Siyo Bure, awamu ya Tano, awamu ya Tano, awamu ya Tano. Lazima Kuna kitu Cha ajabu sana walikufanyizia, vinginevyo huwezi kila wakati kushughulika na kitu ambacho Kwa sasa hakipo. Shughulika na mambo yanayotrend Kwa sasa.
 
Msingi wa hoja ni kwamba tunakataa kwamba huyu shujaa wa mchongo hakufungua mlango.

Kama ni miongoni mwa waliotoa msada wa maboya kwa abiria hiyo ni issue nyingine probably hiyo kazi aliifanya na wenzake Sasa kwa nn hizo sifa apewe yeye? Kwa manufaa ya Nani na walikuwa wanamdanganya Nani?
 
Kamuulize Kassim Majaliwa.
 
Kwa Nini muhudumu asihojiwe na waandishi wakati anafungua mlango Majaliwa alikuwa wapi. Ukute alizimia alipoona ndege inaanguka
 
Suala ni mlango tu kwann imeanguka hamna au ndio report yake iyo ya baada miaka 2
 
Ni wapuuzi wanaoamini mlango ulivunjea kwa kasia la mtumbwi... hata ukoingia youtube unakutana na mashahidi ambao ni survivor walikua abiria wanasema mhudumu ndio alifungua mlango huo...
Nchi hii ina mambo ya hovyo Sana! Waokoaji wanamaji hawana oxygen kwenye mitungi halafu Mwigulu ananunua v8 za serikali za bil 500 kila moja ni mil 450 hadi 500! Tuko serious kweli! Ccm ni laana kubwa!
 
Kwahiyo unakubali kuwa mlango ulifunguliwa na Majaliwa?
Awamu ya nne, tiba ya kikombe cha Babu wa Loliondo

Awamu ya sita, wokovu kupitia pigo la kasia kwenye mlango wa ndege iliyopata ajali ziwa Victoria.

Huku hadithi za vijiweni zikibamba kila kona, kule ukweli wa kisayansi unazidi kujitambulisha wenyewe, lakini bado unatiliwa mashaka. Dogo inabidi sasa auchune tu na kuendelea kula kwa urefu wa kamba yake.

Dogo Majaliwa tayari zali la mentali limeshamuangukia, kapata fedha, kapata ajira, yupo mafunzoni kwa sasa, bungeni kaalikwa na kutambulishwa kama shujaa wa taifa, na hata pia kapata ujiko wa kuongea na Mkuu wa Nchi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…