Waziri Mkuu Majaliwa, pokea makadirio yangu kibanda cha VETA Tabora

Soma vizuti hiyo BOQ, na hapo ndio vilaza wasiojua maana ya ujenzi mnapokwama.
Bei ya cement ni kwa wote, iwe serikali mtu binafsi au kilaza yeyote.
Hivyo hivyo bei ya mbao na mabati.
Tatizo ni kuelewa namna ya kujenga.
Kwa mikataba ya serikali na viwango vyake, unajenga kwanza na kulipwa baadaye, UNAKOPWA!

Ukikopwa kuna riba.
Malipo ni baada ya urasimu mwingi, miezi minne au mitano baadaye.
Mswahili mtaani unanunua vifaa cash na kujenga!
Elewa hilo toka mwanzo, ujenzi wa kikandarasi si lelemama.
Kama wewe unaweza kujenga bure, tena bila faida kazi za kiserikali, ingia mchezo uanze kucheza ngoma hiyo.
Na pengine hata Waziri Mkuu angeweza kujenga majengo yote ya serikali, bure kabisa.
 
Kwa ufupi mleta mada hajawahi kujenga, hakuna gharama za namna hiyo huo ni wizi wa mchana labda kama unajenga mbinguni au baharini, nipe milioni nne nikupe kibanda bora zaidi ya hicho
 
Kitu ambacho watu hawaelewi hapo ni kwamba mkandarasi vifaa kanunua mwenyewe na kivisafirisha, lakini pamoja na hayo bado amelipa Kodi Vat 18% na kabla ya kupata hiyo kazi kina gharama za kuipata, stationary nauli nk, japo bei bado imechangamka. Kwa hesabu zangu ni milioni 8.7. Mimi ni mkandarasi pia.
 
Lakin
Lakini kitu ambacho umetudanganya kingine umesema kupiga branderling ni m2 25 na kufunga gipsum board ni m2 25. Kwa wasiojua m2 ni square MITA yaani Upana mara urefu Kwa jinsi umbo la kinanda lilivyo. Sasa jamaa ana maanisha hicho kibanda kina urefu MITA 5 na Upana MITA 5 ndani Kwa ndani, kitu ambacho sio kweli. Sana sana kina m2 9 au 12.
 
 
Mkuu mahesabu ya BOQ yapo hapo.
Wewe yapitie uone cha kupunguza.
Ni kweli wasiojua ujenzi wanafikiri mkandarasi ndiye mwenye gharama, hawajui kuwa specifications ndio zinaelekeza kitasa , mbso na madirisha ya aina gani kufunga kwenye jengo.
 
Itabidi Waziri Mkuu atoe hadharani uchunguzi wake kuondoa aibu hii inayomkabili.
 
2.5sqmm kwa Sheria ipi ya IEE? kwamba hiyo DB ya kibanda Ina breaker ya 13A au kibanda ikiwa ndogo ndo Sheria isifuatwe? Kusema kweli wakati mwingine tunapotoshwa tu. Kwa maana hiyo unasema plumbing system isifuatwe...shimo la maji taka ichimbwe kila karibu na nyumba ili kubana bajeti? Tusijenge taasisi Kama tunavyojengwa majumbani kwetu.
 
2.5sqmm kwa Sheria ipi ya IEE? kwamba hiyo DB ya kibanda Ina breaker ya 13A au kibanda ikiwa ndogo ndo Sheria isifuatwe?
Umekisoma ulichokiandika ? Usiwe unakurupuka katika kuuliza maswali. Hakiki swali lako Kisha uliza swali kwa usahihi.
 
Nashindwa kuelewa watu wanakubishia kwa sababu ipi hasa.

Hata ujenzi wa binafsi, vifaa vinatofautiana ubora...sio wire, sio PVC, sio vyoo, sio rangi, sio mabati..kila kitu unaulizwa unataka ubora upi? Hata mafundi, kama ana jina kidogo mjini bei zake huwa juu tofauti na hawa wa papatu papatu.

Sasa hapo PM angekuwa amecheck ubora na quality assurance processes kama zilifuatwa na wataalam wake, kabla hajamsweka ndani mkandarasi.
 
Umekisoma ulichokiandika ? Usiwe unakurupuka katika kuuliza maswali. Hakiki swali lako Kisha uliza swali kwa usahihi.
Rejea post no.135 nilikua najibu hoja yako ya kuwa hicho kibanda hakiwezi kuchukua waya ya Armoured zaidi ya 2.5sqmm 3C au 4C...ukimaanisha kuwa ndiyo itakuwa waya wa kuleta umeme hapo.

Sasa rejea kwenye jibu lako la post no.136.
Nakuuliza ni Sheria gani ya IEEE inayoruhusu supply cable iwe ya 2.5sqmm? either iwe ya 3C or 4C? Nyie ndo mnazidi kupotosha viongozi wetu kuhusiana na standard za kufanya kazi za ujenzi alafu mnasema gharama ipo juu.

Kwamba utembeze 2.5sqmm umbali wa mita 100 na ukaipeleka kwenye kibanda Kama supply cable kisa unataka kubana bajeti Kama nyumbani kwako...alafu baada ya miezi mitano mnataka kuweka geti yenye motor na vitu vingine Tena muanze kulaumu kuwa hamkushauriwa vizuri umeme uliopo kwenye kibanda hakitoshi kuendesha motor.

Tupunguze ujuaji.
 
Mwivi wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…