Ukweli ni mchungu lakini utafanyaje sasa na ni ukweli. Unapaswa kuukubali.
Kwa sasa degree si deal tena hasa kama huna other skills na connection. Mimi cheti changu hata sijawahi kwenda kukichukua ukizingatia gpa yenyewe ya 2...
Hamna Cha ukweli mchungu jamaa kachemkaa bhana,kapotosha
 
Hiyo haina shida kada ya mafundi mchundo, ipo kabisa toka siku nyingi, Logic ni kwamba wataalamu wa amaeneo mbalimbali wa vyuo vikuu waende VETA?? as general advice??

Wanatakiwa wafanye hivyo kwa utashi wao, other wise vyuo vikuu vifutwe, au udahili upungue the rest wote waende VETA.
 
Ujerman lazima upitie technical college miaka miwili ndio unaruhisiwa kwenda kusoma degree unayoitaka , mbongo anahisi degree ni issue kubwa wakati hauna ujuzi wowote, hapo majaliwa kashauri vizuri sasa kazeni mashingo yenu
 
Ujerman lazima upitie technical college miaka miwili ndio unaruhisiwa kwenda kusoma degree unayoitaka , mbongo anahisi degree ni issue kubwa wakati hauna ujuzi wowote, hapo majaliwa kashauri vizuri sasa kazeni mashingo yenu
Mitaala ya elimu Tz Huwa inachezewa sana, all in all Majaliwa kakosea sana, namna nyingine vyuo vikuu vifungwe tuu, udahili upunguzwe ili watu wengi waende VETA, kuliko kupoteza muda mwingi ,Kisha eti warudi VETA, huo ni uzwazwa LOGIC inakataa hapo, wewe upo wrong na Waziri Mkuu Majaliwa yupo wrong!!!🤔🤔🤔🚴🚴🚴
 
Mayor Quimby punguza gubu na povu!!!
 
Mimi nilistukia mchongo mapema kila ndugu anayenihusu alikua akifika form four natupa kwenye fani atajiendeleza mwenyewe baadae na wote now wako poa, advance na chuo kikuu niliona kitambo sio deal na soko la ajira linabagua Sana , angalia mechanical mwenye Diploma aliyepitia tech colleges Arusha Tech, DIT, MUST anaajiriwa chap kuliko wewe mwenye degree yako ya fani moja , sasa njoo kwa kozi za Mungu nisaidie sheria, elimu, sayansi ya jamii, maendeleo ya jamii huyu atakufa njaa, Nakuru Pana project ukifika na cheti cha tech ajira chap iwe kwa main contractor au sub , hapo majaliwa kaeleza ukweli japo inauma waliostuka mapema wala hatumshangai maana tuliyajua kitambo.
 
Hii ndio fact ya dunia ndio maana Kenya na Uganda budget zao kwa sasa sio kujenga vyuo vikuu Bali technical schools na colleges na hadi Forex na crypto wanafundisha kwenye vyuo vyao vya Kati
 
Hapo umejibu na kuandika kitu Cha maana sana!!!

Hawa watu wanaoenda vyuo labda waache waende technical schools, na sio vyuo vikuu, sasa pm anashauri waahitimu waende VETA!! Kwanini wasiandae mfumo wa kuwapeleka Moja kwa moja kuliko , waende wakapotezen muda then warudi VETA 🤣🤣🤣😂😂💪
 
kisha wamuuzia nani?
 
Mayor Quimby punguza gubu na povu!!!
Kama nilivyoandika huko nyuma.

Kuna watu ni kuwavaa tu ‘liwalo na liwe’.

Lakini wewe kwa hizi mada żako, Ruangwa ushindi miaka 800, una nidhamu.

Kitu ambacho CCM, aiwezi vumilia ni watu wasio na nidhamu.

Moves żako sio nonchalant, unataka kuanza kutembeza hongo kwa wajumbe. Uoga wako ni Majaliwa iwapo atagombea unaogopa hela yako itapotea.

You are not that clever, hiyo motive yako mimi; binafsi nilikwambia toka post yako ya kwanza ya kujifanya unatoa ushauri PM ajishauri.

Unavyozidi kwenda hii mikakati ingekuwa ya siri labda ungeweza fanikiwa. Lakini CCM aipendi dharau yaani hata Majaliwa asipogombea take my word hilo jimbo awakupi kamwe kwa tabia żako.

Kitu ambacho CCM awawezi vumilia ni dharau kwa viongozi wao wakuu.
 
msemaji wa serikali majuzi alisema kua serikali haina uwezo wa kuajiri wahitimu wote wa vyuo vikuu huo ni ukweli sasa waanajaribu walau kuokoa jahazi vijana wasife njaa, serikali inafahamu watanzania wako zaidi ya 60milioni, kwa mwaka wahitimu wa vyuo vikuu wanazidi 30k serikali binafsi imeajiri watumishi wake wote hawazidi laki Saba idara zote na taasisi zote sasa unatarajia mtaani wako wangapi, na hawana ajira jawabu ni wapate fani wakapambane mtaani kuliko muhitimu kutegemea betting au miujiza ya maombi afadhali akasomee hata umeme WA magari au kuziba hata pancha akiingia kitaa atapata chochote kwa fani yake
 
Inabidi tuende na wakati sasa watu wafahamishwe kwamba nafasi za kazi kwa watu wenye madigirii imekuwa ni bahati nasibu, yaani unaweza ukapata lakini kukosa ndio asilimia kubwa !

Kwahiyo wanafunzi badala ya kutafuta digirii waende technical schools wakasomee skills !

Hata Nchi kama Japan na China pia walizuia watu wasizae zaidi ya mtoto mmoja lakini baadaye walipoona nguvu kazi inapungua na badala yake Wazee ndio wanakuwa wengi kwenye Nchi zao sasa wameruhusiwa kuzaa zaidi na motisha wanapewa 🤣😅👍

Tuwe tunakwenda na wakati , tusipotezee muda watu tuwe tunafahamishana mambo muhimu kama hayo mapema !
 
Kweli hiyo ni changamoto inayotakiwa ifanyiwe kazi mapema!
Swala jingine ni ufanisi wa hizo mashine.
Ufanisi ni mdogo sana, na kingine ubora wake mashakani.
Unaweza taka galvanized, fundi anapaka rangi, mwisho unakutana na kutu.
Utataka SS S316 unapewa S304 ya mm ndogo sana.
Motor inanunuliwa used inapakwa rangi

Alignment inazingua sana hivyo wajikuta unanunua bearing kila mara
 
Why huko vyuo vya degree wasiweke na mchepuo wa VETA ili mwanafunzi asome kama optional course ambayo atapata cheti cha veta na degree yake?
Hili wazo zuri sana. Kama kuna watu wa elimu hapa naomba walibebe wakalijadili na kuliangania zaidi kwa maslahi mapana ya jamii na nchi kiujumla.
 
Huwa nachek Huwa nacheka sana, aina yako ya uandishi, na mawazo yako!! Yaani wewe ndio "THINK TANK" wa kujibu mada hii?? 😂😂😂🤣🤣🤣.

Kuandika hujui ,unaandika " una nidhamu" badala ya"

huna nidhamu"🤣😂🤣😂, hustahili kuendelea kujibiwa, maana hata kichwani umebakiwa na........ZA KUVUKIA BARABARA "

Naona mpo kwenye woga wa kisiasa zaidi,kila critism mnaangalia kwa political perspective 🤔🤔🤔

Mtoa mada mimi, Sina nia na jimbo, sina political ambitions, kama umetumwa mwambie "Mjomba" DIBRO awe na amani!! Wanaotaka jimbo watajitokeza, lakini sio mimi!!!

Mimi nimepost thread kufanya reaction ya alichokiongea kuhusu vijana wahitimu wa vyuo vikuu waende VETA kupata skills,sikubaliani na hilo jambo.

Mwisho Mwishoni Ruangwa huijui vizuri, Ruangwa ni Jimbo rahisi sana kwa opossition kushinda hasa kinachofanyika ni hujuma za kupita bila kupingwa.

Naomba rudi kwenye mada kuu,kauli ya PM Tabora, sio vinginevyo.
 
Ujerman lazima upitie technical college miaka miwili ndio unaruhisiwa kwenda kusoma degree unayoitaka , mbongo anahisi degree ni issue kubwa wakati hauna ujuzi wowote, hapo majaliwa kashauri vizuri sasa kazeni mashingo yenu
Na VETA ilivyoanzishwa ile idea ilitoka ujerumani..na VETA Imesaidia sana
Wataalam wetu wengi tz hawana technical skills kabisa
Injinia mzima hawezi hata ku operate forklift nk
Ila mbona mainjinia enzi za mwalimu waliyosomo moshitec nk
Walikuwa vzr sana ila hawa wa sasa sjui ni elimu kuchezewa au

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…