Nadhani watatia mkopo wa kusoma VETA!!! Hivi wote waliomaliza VETA wameajiriwa/ wamejiajiri?
Na nani??, Veta inatakuwa kichaka cha serikali kujifichia kushindwa kutengeneza mazingira wezeshi kwa vijana kuajiriwa au kujiajiri!!.
 
Mkuu elimu sio shida,shida ni elimu ulio nayo inakuletea ugali nyumbani?
Nakumbuka nchini Norway watu hujifunza carpentry welding,painting ili wakiamua kujenga nyumba wapunguze gharama za kuajili mafundi.

Mfano mwingine ni mtu kujifunza kutengeneza bidhaa kama sabuni n.k
Au kupata mafunzo ya kulea watoto wadogo hizo zote zitakuingizia kipato.

Degree itabaki kuwa degree.
 
Ulichoandika mfano wake kwenu muwe hamna uwezo hata wa kupata mlo alafu unasema hautafanya kazi ya kubeba tofali hadi uone mtoto wa Waziri mkuu na Rais na wao wanabeba matofali ndo wewe utabeba.

Sasa unamkomoa nani?
 
Mbona mh. Majariwa yupo sahihi, sema hamtak kuambiwa ukwel.. Koz mambo mengne bdo mnalinganisha kisiasa..
~ mh. Kaona kabxa tatzo la ajira nchin na wasomi ni wengi wahtaj ajira. Wasomi wajiongeze kwa mambo mawili kupitia msemo wa wazir mkuu.
1.- waende VETA wapate ujuz waje wajiajiri wapate pa kujishkiza wakiwa wanasubir ajira za madgree.
2.- wajiajiri wastegemee kuajiriwa pekee, mitaan fursa ni nyingi.
 
 
Acheni ujinga nyinyi mnaorukia kauli za viongozi pasipo kutafakari na mihemuko yenu. Mheshimiwa waziri Mkuu yuko sahihi.
mbona leo tunaona hao waliomALIZA DEGREE ZAO WANAENDESHA BODA? mbona hilo hamjalilalamikia? hiyo leseni ya uendeshaji wa vyombo vya usafiri inapatikana wapi? kama sio VETA? mbona wanaenda kusoma VETA kupata Leseni? Au unadhani kupata degree ndo umemaliza maisha? Pata Ujuzi mbalimbali ili uwe marketable kwa fursa pia nyingi nyingi,
 
Wewe umejiajiri au umeajiriwa?
Uwen umeajiriwa au la, kasome VETA acha Uvivu, Soma tafuta kazi zinazotokana na mafunzo ya veta utakuwa na fursa ya kutengeneza Fedha. Tatizo ni kukariri ukoloni wa Kuajiriwa
Naunga mkono kauli ya Mheshimiwa waziri mkuu, Mwezi Julai 2025 tukutane VETa, mimi naingia darasa la VETapamoja na kuwa na Masters.
 
Mkuu kama unaona PM kaongea point basi utakuwa ni mtu uliyekata tamaa ya maisha kabisa. Vijana wa Tanzania wanahitaji sheria na sera bora zaidi kuweza kuwa na mifumo imara ya kuwasaidia kufanya shughuli zao. Kuendesha bodaboda sio jambo la kufurahia. Kauli ya PM inamfanya awe level moja na kina Msukuma au Babutale.
 
Kwaiyo mzee ukishakosa kazi serikalini ndo basi tena?
 
Sikuelezei tena. Kama hujaelewa.
 
Hivi degree ni kitu gani kwani mtu anamaliza na hajui chochote hadi aelekezwe tena.

Waziri Mkuu yuko sawa kama hawataki wakae nyumbani wazeeke na degree zao.
Wqziri Mkuu inawezekana kakosea kuwasilisha hoja, inawezekana hakuiwasikisha vizuri.

Lakini hoja hii si mpya. Rais Nyerere kaisema sana, mpaka kuna wakati aliiandika katika vitabu kama "Elimu ni Kazi". Watu wamesahau tu au hawakufuatilia.

Aung San Suu Kyi kashalisema hili Myanmar.

Jamii imeweka msisitizo sana kwenye elimu ya chuo kikuu na kudharau elimu ya ufundi, wakati elimu zote mbiki zinatakiwa kwenda pamoja.

Ila, viongozi nao wanasema maneno bila kuweka mikakati ya hayo maneno kutimia.

Mfano, kumwambia kijana ajifunze kushona nguo VETA wakati serikali inaruhusu uingizaji wa mitumba mingi ya bei nafuu bila hata regulation ni kum set huyu mwanafunzi wa VETA for failure.

Ona hapa Aung San Suu Kyi aliongelea suala hili.


"Daw Aung San Suu Kyi urged youth to “open their eyes and ears for more opportunities” and to develop the capacity to handle many other jobs.” The State Counsellor promoted vocational education, telling the public in Kalay that university education and vocational training are equally important, and that her government is doing its best to reduce unemployment."

Nyerere pia kaongea sana kuhusu Education for Self Reliance.
 
Fahamu Kuna kitu kinaitwa retrain or upgrade skills to enhance your chances of either employment or self employment.
Enzi za serikali kuajiri na kuajiri imepitwa na wakati. Tumia elimu yako uliopata kufungua njia upate maisha.
Bado Tanzania Kuna Fursa za kujiengea maisha bila kukaa kulia Lia na kulaumu serikali.
 
He was right though simkubali huyu jamaa ni very low education personnel to hold such power
 
Huu Uzi hauna mudaa wata ufutaa...Jana nilikutana na huu Uzi nikajikunja kuchangia baada ya muda ukafutwa.

Niliumia kupoteza muda kuandaa point zangu na click batan nikazinguka opppsss something went wrong..🏃🏃🏃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…