Hao wasomi wanatakiwa waandaliwe mapema kwa ujasiria Mali, sio kwa mfumo huu wa hati ya dharula!!
Tunajifunza Nini Katika Udahili Wa Engineer Noel Ngowi UDSM


View: https://m.youtube.com/watch?v=8PrIpQnASmM
Engineer Noel Ngowi asems mfumo umeamua kuwadharau watu wa FTC vyuo vya ufundi (full technician Certificate) na pia wale wa VETA, wakati kufanya hivyo ni makosa makubwa sana.... Degree ikiongezwa baadaye na FTC au VETA basi humfanya mhitimu wa degree kuwa na ufahamu mpana zaidi kwa kuongeza vitendo na ujuzi wa kiufundi juu ya nadharia ya kisayansi aliyohitimu katika digrii
 
Watu waende kwa hiari yao, kauli ile ni kuonesha dharau kwa taaluma za vyuo vikuu!!!
 
Chukueni hii wadogo zetu,tengenezeni ajira wengine
 
Nawaza tu msomi mwenye degree au masters anaingia Veta kusomea ufundi baiskeli au ufundi carpenter ajifunze kuchonga majeneza huku anakutana na sisi tuliofeli darasa la nne miaka hiyo tukaingia mtaani kupiga dili za wizi wa mafuta ya transformer na ukabaji kisha tukastaafu na kujifunza ufundi mtaani halafu tukaanza kupiga hela halafu msomi wa chuo anakuja kusoma veta kisha aje mtaani tumfundishe mbinu za kupiga hela kwenye ufundi😂😂😂hii nchi ngumu sana
 
Vyuo vikuu vianze kutoa shahada/degree za amali..!

Wasome nadharia kwanza kisha baada ya kuhitimu degree waende VETA au FTC wawe wabobezi wa vitendo na ubunifu utakaopelekea kujiajiri au kuwa mahiri wakiajiriwa

NOEL NGOWI - ELIMU YETU INAANDAA WATAWALA BADALA YA WANA TEKNOLOJIA

View: https://m.youtube.com/watch?v=9w4QzgQ4WtgAnafafanua engineer Noel Ngowi.. uzoefu wa miaka 45 wa ujuzi kwa vitendo ndiyo utakaoleta ....
 
Nina mashaka na taaluma ya mtoa mada! sauti yako inaashiria wazi unasukumwa na hisia za uchonganishi. Ikiwa una kili wazi kwamba ameshusha hadhi ya wasomi hiki ulichoandika kama utetezi ndicho ulichobeba kichwani au ndicho ulichoshibishwa?
Kuna haja kubwa kwa wenye uwezo wa kuchambua mambo watoe elimu nini tofaut ya elimu na Maarifa!
Kwa uwezo wangu mdogo nimegundua ipo haja tujifunze kuchambua maoni ya watu yanayotumwa kwa nyinyi wasomi.
Nimependezwa Sana kwa jinsi unavyoo onyesha jamii wewe ni mtu wa Aina gani na mwenye upeo wa Aina gani. Sijadharau wala kupinga Hoja yako, wasomi wanatetewa watumie elimu zao kupambana na Maarifa mengine wewe umegeuza Hoja kisiasa yenye lengo uchonganishi. Jitafakali Meza mate ya akili.
Naunga mkono hoja
 
Kwan tokea lini kura ya mtanzania ikawa na nguvu ya kuchagua kwenye uchaguzi mkuu!
 
Kwa kauli hii napendekeza vyuo vikuu vifungwe ,maana uwezo wa kuwahudumia wahitimu wa vyuo vikuu tumeshindwa .

Why usianzishwe mfuko maalum wa wahitimu kwamba wakopeshwe mitaji badala yake tunataka waende veta, hivi nchi hii inashindwa kweli kumpa kila mhitim m20 baada ya kuwakilisha proposal yake kama hajapata ajira ili kujiajiri kweli kama mkopo ? ili pale apatapo ajira anaanza kukatwa kidogodogo kama ilivyo mkopo wa elim ya juu?

kauli ya Waziri mkuu wenda alikua na nia flani nzuri ila hakufikiria kwa mapana yake.

Tz hili linawezekanika ,chukulia tuna mv8 mangapi na kama moja ni m400 na kuendelea hapo unakua umetoa mkopo kwa watu wangapi?

waziri mkuu nataka kuonana na wewe nikueleze jambo muhim juu ya vijana hawa so nipe utaratibu wa kukuona ,hope upo humu naomba unijibu
 
Mzee acha siasa za kipuuzi tupo huku mtaani hali halisi tunaiona huu unao andika ni upuuzi mwingine kama aliosema katelefoni huwezi tatua tatizo la ajira kwa kuongea kirahisi rahisi tu hivi mnavofanya
Naifahamu vizuri hiyo kazi ya ushonaji kazi nyingine informal na zimeajiri maelfu kwa maelfu ya watu, siongelei hata mafundi wa mtaani wanaopinda Suruali na Shati, naongelea mafundi ambao wanapata hela kushinda 99% ya hao wafanyakazi wa wa Ofisini.

Nimekupa tu mfano nenda CBE Cabs pale uone mafundi wanavyopiga kazi, Shuka na foronya 2 wanashona kwa 2000. Ama nenda Kkoo Swahili Plaza na Maeneo ya karibu tembelea jamaa wanaoshona vijora, Nenda Kkoo Mitaa ya Qiblatain msikitini uone watu wanavyopiga Pazia, Fundi kakosa sana ataondoka na 20,000 ila fundi mzuri anaweza pata hadi 50K-200K kwa siku kutegemea na speed yake.

So siongei kwa kuhadithiwa nipo kwenye hio field anayoongelea Pm, issue za kuajiriwa nishakimbia siku nyingi tu.

Toka mtaani, hizo kazi huzipati kitaa kajichanganye kkoo, Mjini, field kwengine.
 
Upo sahihi Mkuu

Muhimu tuchukue njia sahihi Kwa mustakabali wa Vijana wetu
 
Acha kuleta blah blah nyingi za kijinga katika suala serious hili linalolikumba taifa kwa sasa kuhusu huu ukosefu wa ajira kwa kuleta mifano ya kipuuzi kama njia ya kuondokana na shida hii.

Unaandika kirahisi rahisi tu
 
Ufanisi wake umewahi zingatia?
Nchi yetu bado Changa sana na wala huhitaji ufanisi mkubwa kivile,

Mfano, mdada anatengeneza lotion yake nyumbani, anatumia ndoo, wateja wamezidi kaongeza atatumia dishi kubwa, Wateja wamezidi zaidi, anatumia jaba ila hawezi tena kukoroga mkono inamuuma, anaenda SIDO ananunua machine ya kukoroga, haina kifaa chochote cha kisasa ni lipipipa tu kubwa lina nguzo katikati inasukumwa na mota inakoroga. Hili pipa linalokoroga lenye we ufanisi wake ni sawa na viwanda vya China? Hapana ila kwetu ni big deal.

Nchi hii ni rahisi kutoboa kwenye hizi elimu za ufundi zaidi kuliko chuo, 2025 hii bado asilimia kubwa ya wanaoenda vyuo wanafundishwa effect za colonialism na kwanini Wazungu walivamia Africa, masomo ya darasa la 5. Utegemee hawa watu kwa malaki wote waajiriwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…