Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri
Ufundi una hela, hausubiri mwisho wa mwezi na hupo, hupigwi doro kila siku upo kazini labda upumzike inapobidi lakini usikimbie kazi. Wacheki mafundi umeme, mafundi aluminiamu, mafundi ujenzi, mafundi rangi, mafundi bomba kila siku wao ni kazi tu tena kazi zisizo na mipaka. Awali tulidharau sana vyuo vya NVTC/VETA kwa kuwa shauku yetu ilikuwa ni kuajiriwa tu na si kujiajiri, kuwa na kijiwe/ofisi yako ya ufundi. Soko la ufundi ni kubwa pamoja na kuwepo kwa teknolojia za kisasa kama Akili mnemba/undo, IA
 
Hawa bado hawaelewi tatizo hasa la msingi tulilonalo kama nchi, hao mafundi wenyewe wanalia njaa huku mtaani!
 
Kumpeleka mtoto chuo kikuu chochote hapa Tanzania ni kupoteza pesa... mtoto akimaliza Darasa la saba mpeleke chuo cha ufundi... Mwekee hiyo pesa ya chuo kwenye account ya bank itamsaidia kama mtaji wa kujiajiri baada ya kupata ujuzi kwenye chuo cha ufundi...
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungunza na wakazi wa Igunga, Tabora.

"Tumeendelea kuimarisha sekta ya elimu, Muheshimiwa mbunge ulisema unahitaji VETA tumeleta VETA, hizi VETA tumezijenga ili wewe ukasomee ufundi utusaide katika shughuli za ujasiriamali VETA ile sio tu ya kijana wa darasa la 7 hata wewe uliyemaliza Degree uwe mtaalamu wa Kompyuta nenda kajifunze kushona nguo, uwe fundi cherehani, nenda kajifunze ufundi umeme uwe fundi umeme kwahiyo hata mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kwenda kusoma VETA kwasababu pale unasemea ufundi"

View: https://www.instagram.com/p/DHG-kpjI_Zn/?igsh=MWJvaWRleXJvYXlwMg==


My Take
Broilers wamepewa mchongo wajiogeze.👇👇


View: https://www.instagram.com/p/DHG_Fqpgt68/?igsh=MW93ajllc28zeTZ3Nw==

Ni kweli ujuzi na ubunifu ndo kila kitu
 
Watu wanapenda kupindisha na kukuza vitu. PM amesema VETA ni kwa kila mtu sio darasa la saba tu, hata graduate anaweza kuja kupata ujuzi.

Hapo shida nini. Kwani wewe na degree yako napoenda kujifunza udereva VETA huwa unatafuta nini?

Mimi na degree zangu nikitaka kwenda kujifunza upishi ili nifungie mgahawa mkubwa, kuna shida gani?
Naona unajaribu kuzimua dilute ujumbe wa PM, pole sana, katika nazi TUI ni ile inayokamuliwa kwanza !🤔🤔🤣🤣
 
Mkuu kama upo na utaratibu wa kumuona Waziri mkuu nipe code in box,
Nitamwambia jambo la msingi na asipo nisikiliza nitaenda mshitaki ukweni Songea ,nakwambia uzuri napajua karibu na ofisi za Halmashauri fulani hivi mkabala na Peramio
Mkuu Sina channel, ndo maana nimetumia hili jukwaa kutuma ujumbe wangu,
 
Nina mashaka na taaluma ya mtoa mada! sauti yako inaashiria wazi unasukumwa na hisia za uchonganishi. Ikiwa una kili wazi kwamba ameshusha hadhi ya wasomi hiki ulichoandika kama utetezi ndicho ulichobeba kichwani au ndicho ulichoshibishwa?
Kuna haja kubwa kwa wenye uwezo wa kuchambua mambo watoe elimu nini tofaut ya elimu na Maarifa!
Kwa uwezo wangu mdogo nimegundua ipo haja tujifunze kuchambua maoni ya watu yanayotumwa kwa nyinyi wasomi.
Nimependezwa Sana kwa jinsi unavyoo onyesha jamii wewe ni mtu wa Aina gani na mwenye upeo wa Aina gani. Sijadharau wala kupinga Hoja yako, wasomi wanatetewa watumie elimu zao kupambana na Maarifa mengine wewe umegeuza Hoja kisiasa yenye lengo uchonganishi. Jitafakali Meza mate ya akili.
Naunga mkono hoja
Mkuu aksante sana kwa jibu lako Mujarabu kuhusu Uzi wangu.

Mosi mimi siongozwi na hisia, wala hisia za uchonganishi, isipokuwa statement yenyewe ndiyo Chongamishi YA WENYE DEGREE kusoma VETA mambo ya ufundi.

Pili nilichoandika sio nilichojazwa kichwani, hapana hii ni Pato la akili yangu baada ya kutafakari statement ya Waziri Mkuu.

Kazi ya akili ni kutafakari vitu, kuviangalia kwa jicho angavu, kuona ukweli wake, au namna kilivyopotoshwa!!

Natumain una ndugu zako wamehitimu Shahada vyuoo vikuu, wengine hawana ajira, basi Anza nao waambie waende VETA.
Yote katika yote ,nikushukuru kwa reply yako.

Mtindo wako wa uandishi umenitambulisha na kunijulisha jina na mahali unapotoka 🤣🤣🤣😂😂🤣 aksante sana kiongozi,Jipange jaribu Tena bahati Yako wakati ndo huu,mwaka ndo huu🙏🙏
 
Engineer Noel Ngowi asems mfumo umeamua kuwadharau watu wa FTC vyuo vya ufundi (full technician Certificate) na pia wale wa VETA, wakati kufanya hivyo ni makosa makubwa sana.... Degree ikiongezwa baadaye na FTC au VETA basi humfanya mhitimu wa degree kuwa na ufahamu mpana zaidi kwa kuongeza vitendo na ujuzi wa kiufundi juu ya nadharia ya kisayansi aliyohitimu katika digrii
Nilisema hivi miaka 5 nyuma.....

1741813825571.png
 
Back
Top Bottom