Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri
Wewe jamaa mnamponda mwanakijiji mwenzako

Wewe jamaa unaponda mawazo ya mwanakijiji mwenzako
Mkuu samahani sana,🤔🤔 hili ni jina tu, mi sio mwanakiji wa anapotoka PM, naomba sana usinasibishe jina la JF, content na jina la Kijiji Cha PM.

Aksante kwa kunielewa!!🙏🙏🙏
 
IMG-20250303-WA0003.jpg


Soli za viatu zitaisha, You Know #BongeLaNdula 😂​
 
Huyo bado mnasikiliza na kumuamini, alisema tena msikitini Magufuli yuko imara na anachapa kazi kumbe anapigania uhai wake Mzena kwa siku ya sita mfululizo.
 
Kama huyu PM anajua kuwa elimu ya VETA inamwezesha mtu wa degree kujiajiri...kwa nini basi wasibadili vyuo vikuu viwe vyuo vya VETA ila kuongeza wigo wa upatikanaji wa hiyo elimu?
Kwa maneno mengine anachosema anamaanisha kuwa vyuo vikuu vyote vinavyotoa degree vifutwe vibaki vyuo vya VETA tu

Kuwa hata akiumwa atibiwe na mtu aliyesoma VETA
 
Kumpeleka mtoto chuo kikuu chochote hapa Tanzania ni kupoteza pesa... mtoto akimaliza Darasa la saba mpeleke chuo cha ufundi... Mwekee hiyo pesa ya chuo kwenye account ya bank itamsaidia kama mtaji wa kujiajiri baada ya kupata ujuzi kwenye chuo cha ufundi...
Kwa hiyo hata ukiumwa utatibiwa hospitali na mtu wa darasa la saba aliyesoma VETA?
 
Nchi yetu bado Changa sana na wala huhitaji ufanisi mkubwa kivile,

Mfano, mdada anatengeneza lotion yake nyumbani, anatumia ndoo, wateja wamezidi kaongeza atatumia dishi kubwa, Wateja wamezidi zaidi, anatumia jaba ila hawezi tena kukoroga mkono inamuuma, anaenda SIDO ananunua machine ya kukoroga, haina kifaa chochote cha kisasa ni lipipipa tu kubwa lina nguzo katikati inasukumwa na mota inakoroga. Hili pipa linalokoroga lenye we ufanisi wake ni sawa na viwanda vya China? Hapana ila kwetu ni big deal.

Nchi hii ni rahisi kutoboa kwenye hizi elimu za ufundi zaidi kuliko chuo, 2025 hii bado asilimia kubwa ya wanaoenda vyuo wanafundishwa effect za colonialism na kwanini Wazungu walivamia Africa, masomo ya darasa la 5. Utegemee hawa watu kwa malaki wote waajiriwe?
Ajira haziwezi patikana kama elimu yenyewe sio bora.
Ajira haiwezi patikana wakati tumewekeza kwenye biashara ya uchuuzi na umachinga, kwa ufupi tupo kuwafaidisha wachina
 
Ndio kwani Kila mtu atafanya ubunifu na ugunduzi wake
Kwamba kilamtu akifikiria hivyo ni mtihani kwa taifa nikuulize ? Kuna shule za ufundi zaidi ya 20 Tanzania nzima Kuna vyuo vya veta inwezkn saivi vimefika kila wilaya impact yake ni ipi kwenye mchakato wa kumkwamua mtanzania maskini? SUA pale products zao zipoje kunusuru uchumi katk eneo la kilimo...nchi ambayo Haina sera Wala dira unahisi hat ukiend veta ndo utafanikiwa? Kama waowao wanakusomesha kwa mkopo then hawajui utaurudisha vipi then uende tu veta
 
Kwamba kilamtu akifikiria hivyo ni mtihani kwa taifa nikuulize ? Kuna shule za ufundi zaidi ya 20 Tanzania nzima Kuna vyuo vya veta inwezkn saivi vimefika kila wilaya impact yake ni ipi kwenye mchakato wa kumkwamua mtanzania maskini? SUA pale products zao zipoje kunusuru uchumi katk eneo la kilimo...nchi ambayo Haina sera Wala dira unahisi hat ukiend veta ndo utafanikiwa? Kama waowao wanakusomesha kwa mkopo then hawajui utaurudisha vipi then uende tu veta
Umeona wapi waliohitimu VETA wanalalamika Ajira? By the way Bado Wilaya 60 Hazina VETA,Mkoa 1 hauna Veta na zile zilizokamilika ndani ya miaka 4 iliyopita Bado hazijawa well equiped.

Mambo yakishachangabya huko Veta wahitimu watapewa mikopo ya bila riba na Serikali Ili wakafanye kile wanachoona kinaweza wapate Fedha.

Mwisho Hakuna shule za ufundi ziliuwawa ,Kwa Sasa Samia ndio anazifufua na zinajengwa upya
 
Huyo bado mnasikiliza na kumuamini, alisema tena msikitini Magufuli yuko imara na anachapa kazi kumbe anapigania uhai wake Mzena kwa siku ya sita mfululizo.

..labda na yeye alidanganywa na waliokuwa wakimuuguza Jpm.

..kuna rumours kwamba bwana mkubwa alitangulia muda mrefu ila kuna mipango ilikuwa inasukwa hivyo kuchelewesha taarifa kutolewa.
 
Naona umeshindwa kujibu hoja!!! Ujinga ni mzigo 🤣🤣🤣
Hoja gani uliyotoa hapo zaidi ya utoto?

Zunguka Sasa na bahasha ya degree uone ,haya ndio majibu kama huwezi nenda ukaombewe Kwa Mwamposa au nenda ukapewe maneno ya faraja Ufipa Kwa kibaraka
 
..kama ni hivyo vyuo vikuu vifungwe, au vibadilishwe kuwa veta.
Haviwezi kufungwa ila vinabadilishwa Mitaala.

Tena Vyuo Vikuu vitasajili watu wachache baada ya criteria kuongezwa Ili hao watu wachache wawe na uwezo wa kushindana ndani na Nje na pia wawe na uwezo wa kubuni Ajira.
 
Ujumbe wa waziri mkuu Kwa wahitim: ' mlichosomea vyuo vikuu ni takataka, kajifunzeni ushoni' !
 
Kama graduates wanaendesha boda na bajaji mitaani kuna shida gani mtu wa sociology akirudi VETA kusomea umeme wa majumbani kutokana na miradi ya REA kushika kasi.

Au udereva wa mitambo akakimbizana na wachina waliotapakaa kwenye miradi mbalimbali.
 
Back
Top Bottom