Waziri Nape Nnauye asema bei ya internet imeshuka wakati wa Rais Samia ukilinganisha na Machi 2021

Waziri Nape Nnauye asema bei ya internet imeshuka wakati wa Rais Samia ukilinganisha na Machi 2021

Habari wakuu?
Hii ni habari njema wadau wenzangu, twaisubiri kwa hamu.


20220819_192315.jpg


Ahsanteni wananzengo
 
"Haya mambo nyie acheni tu."ni msela wangu mmoja mpole sana,kila akichanganywa na jambo huishia kusema hivi!
 
Watende sasa, na sio kutufanya wapumbavu.
haya makampuni nao wameona serikali ni ya oya oya ,ingekuwa kipindi cha Magufuli haya mabadiliko yasingekuwa yanafanyika hovyo
 
Sijawahi kuwaelewa Nape na Mwigulu, nadhani watu wenye roho mbaya ya kichawi, kiburi na wabinafsi ,hawafanyi mambo kwa ajili ya wananchi wanafanya mambo yanayowafaidisha wao na watawala.

Hawa majamaa heri hata Mungu awatangulize mbele ya haki hasa Mwigulu
 
Kufuatia mjadala wa kupanda kwa gharama za vifurushi kwa watumiaji wa Data kwenye mitandao ya kijamii, Waziri ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kupitia Ukurasa wake wa Twitter ametoa ufafanuzi kwamba baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani, alichukua hatua ya kushusha gharama za data.

Waziri Nape amesema mwezi Machi 2021 bei ya juu ilikuwa ni Tsh. 40.04 kwa MB 1, lakini ilipungzwa na kufikia Tsh. 9.35 kwa MB 1 mwezi Agosti 2022.

Kumekuwepo na mjadala kupitia mitandao ya kijamii hususani Twitter, JamiiForums na kwenye kurasa nyingine kuhusu kupanda gharama za vifurushi vya mitandao ya simu ikiwemo gharama za Data (Internet) bila utaratibu ambao ni shirikishi wa watumiaji.

Kwa mujibu takwimu Watumiaji wa Internet kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) ripoti ya robo ya nne ya mwaka 2021 zinaonesha Watumiaji wa intaneti walifikia milioni 29.8.

=======================
Kweli nyie serikali mko makini sana kuwajali watu wenu maana kabla ya serikali yenu ya awamu siita buku nilikuwa napata 1GB VIP kwa sasa imekuwa kiasi gani ndg Nepi nahuye
 
Back
Top Bottom